Nadhani hapa FaizaFoxy unataka kusema miaka 25 iliyopita uchumi ulikuwa umeshuka sana. Lakini kumbuka wakati huo Tanzania ilikuwa a closed economy na ulitegemea zaidi kilimo. Hata hivyo uchumi huo wa pareto, pamba n.k ulitosheleza kutoa huduma za afya bure, elimu bure, kujenga reli, kununua ndege, na mtu aliweza kuishi kwa mshahara wake. Na ni mara chache sana tulisikia viongozi wetu wakiongea ukuaji wa uchumu in statistical terms. Kwa mwananchi wa kawaida whether uchumi unakuwa kwa 1% au kwa 20% of no value kwake kama maisha yake ni duni na hana huduma muhimu i.e maji, matibabu, chakula na malazi bora.
Na hiki ndicho watu wanaongelea kwa sasa kwamba hizi number wanazotupa viongozi wetu wanatoa wapi hasa wakati in reality watu wanabangaiza maisha? Mara zote viongozi hawa wanaongelea GDP, lakini nadra kuongelea GNP. It will also be interesting kama wangeongelea Gini-coefficient (hii inaonesha gap kati ya maskini na matajiri).