Hivi ni kweli wanawake wanaodumu kwenye ndoa hawawapendi waume zao?

Hivi ni kweli wanawake wanaodumu kwenye ndoa hawawapendi waume zao?

loosimingori

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2017
Posts
920
Reaction score
1,145
Kuna usemi huwa unasemwa na baadhi ya wanawake kwamba ili mwanamke udumu kwenye mahusiano basi mwanamke anapaswa yeye asimpende huyo mwanaume isipokuwa mwanaume ndio anapaswa kumpenda mwanamke.Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka 6 sasa.Ninaishi na mwenzangu bila kuwa na serious conflicts ukiondoa changamoto za kawaida ktk mahusiano.Nimekuwa nikijiuliza kwa muda huu tuliodumu kwenye ndoa na mwenzangu inamaana yeye hanipendi ila ni mimi ndio nampenda ndio maana hadi leo nipo pamoja na yeye?kifupi ni kwamba naomba nieleweshwe hiyo nadharia kwamba ili mahusiano ya dumu basi mwanamke asimpende mwanaume ila kinyume chake
 
Chamsingi ni uvumilivu tu mkuu. Angekuwa hakupendi angeshaamsha popo mda mrefu maana hapo sio jela.

Kama maisha yanaenda vumilianeni tu mtashangaa mnaitwa bibi na babu soon.
 
Chamsingi ni uvumilivu tu mkuu. Angekuwa hakupendi angeshaamsha popo mda mrefu maana hapo sio jela.

Kama maisha yanaenda vumilianeni tu mtashangaa mnaitwa bibi na babu soon.
lakini umeshawahi kusikia hiyo dhana
 
kupenda ni wajibu wa mwanaume na mwanamke ni kutii tu, huwa siamini kama mwanamke huwa anapenda maana unaweza kuta una mwanamke na mnapendana sana ila ndani ya siku mbili akakubadilikia ghafla na wala yeye isimsumbue ila wewe ndio ukawa katika wakati mgumu na kuwaza imewezekanaje... lakini sisi wanaume sio rahisi kumsaham mwanamke ndani ya siku chache hata kama umeamua kumuacha
NAHUJA
 
mi naona tunapendana ila point yangu ni hiyo dhana kutoka kwa baadhi ya wanawake
dhana zipo nyingi sana humu duniani, sasa wewe hiyo dhana moja umeanza kumuwekea mashaka mkeo.

na yeye akisikia vice versa ya dhana yako na akaweka mashaka unatarajia nini kitatokea!!?
 
Back
Top Bottom