loosimingori
JF-Expert Member
- Oct 30, 2017
- 920
- 1,145
Kuna usemi huwa unasemwa na baadhi ya wanawake kwamba ili mwanamke udumu kwenye mahusiano basi mwanamke anapaswa yeye asimpende huyo mwanaume isipokuwa mwanaume ndio anapaswa kumpenda mwanamke.Binafsi nipo kwenye ndoa takribani miaka 6 sasa.Ninaishi na mwenzangu bila kuwa na serious conflicts ukiondoa changamoto za kawaida ktk mahusiano.Nimekuwa nikijiuliza kwa muda huu tuliodumu kwenye ndoa na mwenzangu inamaana yeye hanipendi ila ni mimi ndio nampenda ndio maana hadi leo nipo pamoja na yeye?kifupi ni kwamba naomba nieleweshwe hiyo nadharia kwamba ili mahusiano ya dumu basi mwanamke asimpende mwanaume ila kinyume chake