Habari za wakati huu ndugu zangu wa bara na visiwani, mashariki ya mbali na magharibi pia...
Mara nyingi nimekuwa nikilisikia hili swala kuwa wanawake wengi huvutiwa na wanaume wanaonukia zaidi kuliko wale wanaopendeza.
Suala hili imepelekea kunipa maswali mengi. Je, ukiwa umevaa nguo kuu kuu lakini ukawa unanukia zaidi kuliko yule aliyevaa nguo mujarabu zinazovutia na amepakaa mafuta yake ya mgando au hajapakaa kabisa uturi au manukato ya aina yeyote wewe ndio utakuwa mashuhuri kwa wanawake na kuwavutia zaidi kuliko aliyependeza?
Swala hili nalileta kwenu watu wa jukwaa hili la urembo na mitindo tujaribu kulifafanua kama litakuwa na ukweli wowote.
Mkuu hivi vitu viwili kupendeza na kunukia vinakwenda sambamba,,,mfano perfume wenzetu wanaichukulia kama ni nguo,,,na ukizoea sn kunukia harufu nzuri,, siku ukiwa huna manukato basi utajiona kama una mapungufu Fulani...mkuu naunga mkono hoja kwamba kunukia harufu nzr kunakaribisha na kuvutia wanawake wazuri sana,,,mimi mwenyewe ni Chizi perfumes mkuu,,,kwa kifupi najipenda na napenda kunukia tena harufu nzuri sana...nishabahatika kupata wasichana tofauti tofauti tena baadhi yao ni wake za watu,,,siku nikauliza nini kiliwafanya wanikubali,,,,kwa muda tofauti kila mmoja alisema kwanza najipenda,,,napendeza,,nanukia vizuri sana...kwahyo mkuu kunukia harufu nzr kunavutia zaidi warembo na kunapandisha status yako...hata msichana anayenukia harufu nzr,,,aisee ni hatari sana,,she is so romantic and sexy..