Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari za wakati huu ndugu zangu wa bara na visiwani, mashariki ya mbali na magharibi pia...
Mara nyingi nimekuwa nikilisikia hili swala kuwa wanawake wengi huvutiwa na wanaume wanaonukia zaidi kuliko wale wanaopendeza.
Suala hili imepelekea kunipa maswali mengi. Je, ukiwa umevaa nguo kuu kuu lakini ukawa unanukia zaidi kuliko yule aliyevaa nguo mujarabu zinazovutia na amepakaa mafuta yake ya mgando au hajapakaa kabisa uturi au manukato ya aina yeyote wewe ndio utakuwa mashuhuri kwa wanawake na kuwavutia zaidi kuliko aliyependeza?
Swala hili nalileta kwenu watu wa jukwaa hili la urembo na mitindo tujaribu kulifafanua kama litakuwa na ukweli wowote.
Pia dili zingine zinakuja tokana na u smart.We pendeza halafu uwe unatoa harufu ya hovyo hovyo tu na mijasho uone kama kuna demu atakusongelea, kwa kifupi hakuna mtu anaevutiwa na uchafu, vaa smart, kuwa msafi, pendeza watakuja wenyewe wala huna haja ya kutumia nguvu kubwa
Pia dili zingine zinakuja tokana na u smart.
Nakazia.Hata connection na marafiki wa maana unapata ukiwa smart
Harufu nzuri ni moja ya utambulisho wa mtu mstaarabu hata kama sio mstaarabu ataonekana mstaarabu. Utambulisho mwingine ni ukimya na kuongea maneno machache kwa utaratibu yasiyokwaza, mwingine ni kuwa mtoaji na kusaidia pale unapoombwa msaada, lakini pia tabasamu wakati wa kumtazama mtu.Habari za wakati huu ndugu zangu wa bara na visiwani, mashariki ya mbali na magharibi pia...
Mara nyingi nimekuwa nikilisikia hili swala kuwa wanawake wengi huvutiwa na wanaume wanaonukia zaidi kuliko wale wanaopendeza.
Suala hili imepelekea kunipa maswali mengi. Je, ukiwa umevaa nguo kuu kuu lakini ukawa unanukia zaidi kuliko yule aliyevaa nguo mujarabu zinazovutia na amepakaa mafuta yake ya mgando au hajapakaa kabisa uturi au manukato ya aina yeyote wewe ndio utakuwa mashuhuri kwa wanawake na kuwavutia zaidi kuliko aliyependeza?
Swala hili nalileta kwenu watu wa jukwaa hili la urembo na mitindo tujaribu kulifafanua kama litakuwa na ukweli wowote.
Duh!!,Kwapa je?.Mimi najali zaidi hali ya usafi wake kwa ujumla na sio kunukia koti soksi inatoa uvundo,.mwingine ananukia juujuu ukimvua vest tuu unapata pumu na kifaduro..[emoji21]
Kitu cha kutoka kwapani au siyo?!!.Ni kweli hata wanasaikolojia wamekiri hilo..mwanamke anavutiwa zaidi na harufu yako kuliko mwonekano.tens ile harufu ya asili sio ya kujaza mipafyumu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah we mwanamke umetuchoka sie 😂😂😂 aya ngoja nitafute pafyumu ya moka sahivi!Mimi najali zaidi hali ya usafi wake kwa ujumla na sio kunukia koti soksi inatoa uvundo,.mwingine ananukia juujuu ukimvua vest tuu unapata pumu na kifaduro..😣