Hivi ni kweli wasanii wengi wa Tanzania baba zao waliwatelekeza?

Hivi ni kweli wasanii wengi wa Tanzania baba zao waliwatelekeza?

Yudatade Edesi Shayo

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2016
Posts
2,903
Reaction score
4,334
Imekuwa kama fashion, sasa sijuii ni kweli au ndo muendelezo wa kina baba kutengwa kwenyw kula mema ya watoto wao? jana nilikuwa na sikiliza kipindi cha the switch wasafi pale kwenye segment ya cha kijani mama wa msanii mario alikuwa ana hojiwa akasema amemlea mwanae peke yake baba yake alimtelekeza

Diamond naye baba yake alimtelekeza, Ommy dimpoz baba yake naye alimtelekeza, Mwana FA naye baba alimtelekeza, Ney wa mitego kila siku anamuonesha mama ake tu sijawahii kumuona baba, inatia mashaka kweli kama ni tabia zetu kweli wakina baba tuache aise
 
Mimi baba yangu alinitelekeza nikiwa chuo nilipambana still baadae nkampa nafasi yake kama baba..nadhani hii ni same na kinachotokea katika maisha ya hawa wasanii sidhani kama wanawatelekeza from day one kuna kipindi tu cha maisha kinatokea baba kashikwa na mwanamke nje anashindwa kukumbuka familia yake mimi baada ya kugundua hivyo niliamua kusamehe tu maana nkajua mzee hakuwa tena kwenye akili zake
 
Tatizo ni moja, wanawake mkishaachana wanatia chuki mbaya kwa watoto, Kuna siku niligindua hili hivyo nikarudi kwa Mzee Kama kawa, hata nikashangaa yaani kumsogelea tu , kila kitu akanisaidia shule, gharama za chuo, mpaka leo tuko close Sana, simu nikilishwa mapema but NASHUKURU God alinifumbua kwamba so kila Mara wazee hawatupendi but lipo lingine nyuma ya yote
 
Nawaza kati ya haya:
1. Wametoka kwa single mothers - ni kawaida kwa dunia ya sasa kumpa mimba binti na kusepa. Wadada wengi wanajali raha ya muda wasiwaze matokeo ya starehe hizi.

2. Mimba zenye utata - zamani hizo hakukuwa na DNA test, hivyo mwanamke akiwa mwingi wa habari alikataliwa na wote pale alipopeleka ujauzito. Hii inatokana na tabia mbovu ya mwanamke mwenyewe.

3. Kuzaa na mwanamume ambaye hakuwa tayari zaidi ya kutaka starehe tu. Baadhi ya wanawake hudanganywa kuwa wakibeba mimba ya mwanamume wataweza 'kupendwa na hivyo kujihakikishia ndoa.

4. Kuzaa na mume wa mtu. Hapa wanaume wengine hukataa katakata ili kunusuru ndoa zao halali. Wengi hutaka starehe za muda tukutokana na tamaa.

5. Mabinti wadogo kuangukia mikono mwa matapeli wa mapenzi, baadaye kuwakataa ama kuwakimbia.

6. Ndoa kuvunjika na mama kukimbia na mtoto, ama ndoa kuvunjika na mume kususa mke na mtoto. Pia mazingira ya hivyo ya siku hizi, mke kutumia mtoto kama njia ya kiuchumi dhidi ya baba wa mtoto pale wanapotengana.

Ukitaka kujua mazingira ya huu upupu tafakari ule mwito wa Ret.RC wa Dar kwa wajane na waliotoswa. Asilimia kubwa waliokwenda pale walikuwa na malalamiko ya kuzalishwa kisha kutoswa. Tazama aina ya wanawake waliokusanyika pale, wengi ni "watema shombo wakubwa." Mfano ni yule madame aliyemwanika mumewe mitandaoni kuwa hatunzi watoto wake, kisha akaibukia kwa RC.
 
Familia nyingi kina mama ndio wapambanaji,

Wazee wanahesabu mifugo, mazao na kupiga ulabu.

Mtoto anakua mtu wake wa karibu ni mama.

Wazee wajisahihishe.
 
Imekuwa kama fashion, sasa sijuii ni kweli au ndo muendelezo wa kina baba kutengwa kwenyw kula mema ya watoto wao? jana nilikuwa na sikiliza kipindi cha the switch wasafi pale kwenye segment ya cha kijani mama wa msanii mario alikuwa ana hojiwa akasema amemlea mwanae peke yake baba yake alimtelekeza

Diamond naye baba yake alimtelekeza, Ommy dimpoz baba yake naye alimtelekeza, Mwana FA naye baba alimtelekeza, Ney wa mitego kila siku anamuonesha mama ake tu sijawahii kumuona baba, inatia mashaka kweli kama ni tabia zetu kweli wakina baba tuache aise
Familia nyingi za kiafrica tuliokulia maisha ya tia maji tia maji ni single mothers!!
 
Familia nyingi kina mama ndio wapambanaji,

Wazee wanahesabu mifugo, mazao na kupiga ulabu.

Mtoto anakua mtu wake wa karibu ni mama.

Wazee wajisahihishe.
Nionyeshe msanii mmoja aliyetelekezwa na baba huku mama akiwa kwenye ndoa!! Hii ndio tofauti ya kuzaa kwenye ndoa na nje ya ndoa.
 
Tatizo ni moja, wanawake mkishaachana wanatia chuki mbaya kwa watoto, Kuna siku niligindua hili hivyo nikarudi kwa Mzee Kama kawa, hata nikashangaa yaani kumsogelea tu , kila kitu akanisaidia shule, gharama za chuo, mpaka leo tuko close Sana, simu nikilishwa mapema but NASHUKURU God alinifumbua kwamba so kila Mara wazee hawatupendi but lipo lingine nyuma ya yote
Mie mtoto kaambiwa nimekufaa ..
 
Nikitazamaga watu wengi waliofanikiwa mfno ktk utajiri mkubwa, vipaji vya michezo au uimbaji, soccer na wengineo wengi ni watu waliotelekezwa na BABA zao,,

akina mama mtuambie kuna siri gani mtoto akilelewa na mzazi mmoja hasa MAMA uwa ndio vinara ktk sehemu nyingi tofaut tofaut
 
Mimi baba yangu alinitelekeza nikiwa chuo nilipambana still baadae nkampa nafasi yake kama baba..nadhani hii ni same na kinachotokea katika maisha ya hawa wasanii sidhani kama wanawatelekeza from day one kuna kipindi tu cha maisha kinatokea baba kashikwa na mwanamke nje anashindwa kukumbuka familia yake mimi baada ya kugundua hivyo niliamua kusamehe tu maana nkajua mzee hakuwa tena kwenye akili zake
Hii ipo anaenda kuoa nje
 
Back
Top Bottom