Hivi ni lini?

Mbwilimbwili

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
183
Reaction score
282
  • Ni lini tutakua na taifa la watu ambao tupo concerned na nchi yetu, tunajadili mada nzito nzito?
  • Ni lini tutakua na mashindano like top ten ya uzalishaji kiviwanda kwa mikoa?
  • Ni lini waziri wa teknolojia atazindua gari la umeme kutoka kampuni ya kitanzania?
  • Ni lini vijana wataacha kukimbilia sauzi?
  • Ni lini kila mtu atakua proud kuitangaza bendera ya Tanzania?
  • Ni lini tutakua na taifa la watu shupavu tusiotetereka?
  • Ni lini mtu atatamani kuhama Dar aende Nambunjumbwilu au Vikumbulu?
  • Ni lini polisi watakua watu wa kawaida tu kama sisi beside yapower yao kisheria?
  • Ni lini madogo watashindana ku-code na kuja na mawazo makubwa?
  • Ni lini tuta-launch satellite yetu?
  • Ni lini wadada wengi watajitambua?
  • Ni lini Watanzania kwenda vacation haitakua kitu cha ajabu?
  • Ni lini rangi ya kijani itatoka?
HIVI NI LINI?
 
Za ndani nasikia kuna mwamba yupo ndani uko mda huu anakisuka kirusi kingine chenye maangamizi mara mbili ya Corona, stay tuned

Kwahio na wewe utaondoka kikija hiko kilusi au [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Labda tusubiri mwanakondoo atakapokuja mawinguni kuchukua wateule,nahisi watakaobaki wataweza hayo uyasemayo
 
Sasa mkuu kama mpaka leo hii bado kula yetu tu ni mtihani..hapo usiulize tunavaa nini na tunalala wapi..tunapigika haswa...! Kwa ground life ni tough sana..tutafika huko lakini kwa kuchelewa sana.
 
Sasa mkuu kama mpaka leo hii bado kula yetu tu ni mtihani..hapo usiulize tunavaa nini na tunalala wapi..tunapigika haswa...! Kwa ground life ni tough sana..tutafika huko lakini kwa kuchelewa sana.
mkuu tunaweza, sema tu kama tumekubali yaishe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…