Hivi ni mimi tu au na wengine mnapitia ninayoyaona

Hivi ni mimi tu au na wengine mnapitia ninayoyaona

Mwizukulu mgikuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2021
Posts
5,715
Reaction score
13,739
Nipo likizo yapata wiki moja, ila nilisafiri kutoka kwangu kuja kwa huyu mzazi wangu.

Likizo imekuwa chungu natamani tu nirudi nyumbani kwangu kabla ya muda, kutwa nashinda naongea nampa ushauri namuelekeza kuna baadhi ya mambo naona kabisa anaharibu lakini ni mbishi kwelikweli.

Kazi kwelikweli!
 
Mimi nikajua anakulazimisha kuoa/ kuolewa au anataka wajukuu kumbe wewe ndio unang'ang'ana kumuelekeza
 
Nipo likizo yapata wiki moja ...ila nilisafiri kutoka kwangu kuja kwa huyu mzazi wangu.lakini likizo imekuwa chungu natamani tu nirudi nyumbani kwangu kabla ya muda,, kutwa nashinda naongea nampa ushauri namuelekeza kuna baadhi ya mambo naona kabisa anaharibu lakini ni mbishi kwelikweli.........kaaaazi kwelikweli
Ushauri wa nn unaompa
 
Mama ila nimekuja kugundua wababa wengi huwa na busara na hekima kadiri muda unavyozidi kusogea
😂kumbe! Kawaida hiyo mkuu,umri unaposogea nao wanazidi kuwa wabishi kweli.Nilikwambia uje tule parachichi Likizo hii but ukanigomea,🙋
 
Mapumzko ni siku 3 tu kwa sisi masikini.

Day1 unafka jion,
Day 2 unashnda maskan
Day 3 asbh unadandia lori unatembea ulikotoka.

Kama una hela haina tatzo. Kaa hata milele.

Nb. Mnatibuana na dingi xako kisa pesa. Ongeza bajeti.
 
Mtoto kwa Mzazi hakui, kw Mzazi wako wewe bado ni Mtoto tu.
 
Kuongea au kumrekebisha mtu mzima inahitaji akili na hekma nyingi sana maana unatakiwa kumfanya aone yupo sawa kutokana na situation yake na kumuonesha njia nyingine pasipo kuonesha kuwa wewe unajua zaidi au ni superior kwake..

Kumbuka ukimkosoa mtu lazma ajitetee ila ukimuelewesha mtu na kumpa njia nyingine pasipo kuwa dikteta kwa maamuzi yake, possibility kubwa atakuelewa na atabadilika maana hatohisi anaamrishwa

Yawezekana anakuelewa ila ile ego ya kuwa mzazi haiwezi kukubali approach uliyoitumia. Ni maoni tu
 
Back
Top Bottom