Habari wanaJf, poleni na mapambano dhidi ya corona.
Kwa wale wenzangu na mimi wapenda movie/ tamthiliya mnaweza kuwa mmekaa mnaangalia movie yenu anakuja mtu ambae tayari alishaiangalia anaanza 'hao wanaopigana hapo baadae watakuja kupatana' au ' huyo hapo baadae atakufa'
Hii tabia kiukweli inakera sana unatamani umtie vibao huyo anayeongea maana mimi ukishaniambia hivyo hamu yote ya kuangalia movie inakata. Nianze kuangalia nini tena wakati nimeshajua mbele kinatokea nini?
Halafu hii ipo sana kwa watu wa uswahilini sijui tupoje yaani