Hivi ni mimi tu ndio nakereka na hii tabia au tupo wengi

Hivi ni mimi tu ndio nakereka na hii tabia au tupo wengi

Nikiangalia movie nakua peke yangu. Maana kama kuna pronounciation wameongea na sijasikia vizuri basi narudisha nisikilize tena
 
Habari wanaJf, poleni na mapambano dhidi ya corona.

Kwa wale wenzangu na mimi wapenda movie/ tamthiliya mnaweza kuwa mmekaa mnaangalia movie yenu anakuja mtu ambae tayari alishaiangalia anaanza 'hao wanaopigana hapo baadae watakuja kupatana' au ' huyo hapo baadae atakufa'

Hii tabia kiukweli inakera sana unatamani umtie vibao huyo anayeongea maana mimi ukishaniambia hivyo hamu yote ya kuangalia movie inakata. Nianze kuangalia nini tena wakati nimeshajua mbele kinatokea nini?

Halafu hii ipo sana kwa watu wa uswahilini sijui tupoje yaani
Unajifanya hupendi lakini ninyi ndio mabingwa wa kuangalia Movie za LUFUFU.

Sioni tofauti yoyote
 
Mi pia hua sipendi. Anaeniletea huo ushamba kama ni mtu mzima hua naondoka namuachia movie aangalie ntarudi ikiisha ila kama ni rika langu hua nazima tunachotumia kuangalia then namwambia asimulie
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nikiangalia movie nakua peke yangu. Maana kama kuna pronounciation wameongea na sijasikia vizuri basi narudisha nisikilize tena
Mkiwa wawili mnaulizana hapo kasemaje??
 
Back
Top Bottom