Hivi ni mkoa gani unaongoza kwa mapato Tanzania?

Hivi ni mkoa gani unaongoza kwa mapato Tanzania?

Iringa kwa vigezo vifuatavyo.
1. Mapato kwa ajili ya kiwanda cha karatasi.
2. Kiwanda cha majani chai bora.
3. Misitu ambayo unatoa mbao (TUICO). Nguzo za umeme, mbao kuelekea mikoa mingine.
4. Ruaha National park.
 
Wadau mwenye kujua hili tafadhali jiji au mkoa wenye mapato makubwa Tanzania ni upi.
Takwimu za mapato yatokanayo na kodi kuanzia July 2016-December 2016
TRA.png

Chanzo: Ripoti ya TRA 2016/17 kwa robo mbili za mwanzo.

The wonders of Mtwara ni kwamba mwezi Novemba na Desemba 2016 idara ya forodha imekusanya sana, nadhani ni kupitia bandari maana Dangote alishusha magari 600 mwezi Desemba, na kabla ya hapo alipitisha pia makaa ya mawe. Upelekaji wa korosho ghafi nje ya nchi umechangia kwa kuwa shughuli inakuwa kuanzia Oktoba. Kama utakumbuka kuwa Waziri Mkuu aliamrisha korosho kusafirishwa kwa bandari ya Mtwara pekee. Kwa miezi miwili tu wamekusanya milioni 68,208.69. Pia kuna idara ya Walipakodi Wakubwa (LTD) imekusanya milioni 2,756,417. Wengi wao wapo DSM, kwa hiyo ukipenda hiyo figure ijumlishe kwa DSM.

NB: Ni muhimu kuangalia na mapato mengine zaidi ya kodi.
 
Back
Top Bottom