Hivi ni nani mshauri wa Rais Kikwete?

Hivi ni nani mshauri wa Rais Kikwete?

Kwani mnadhani huyu rais wetu anashindwa kujishauri mwenyewe?

He is a semi-genius, huyo mshauri wake kawekwa pale ili nae apunguze mitatizo yake tuu, kwani mnadhani rais anashindwa kupuuzia ushauri, hata kama ni productive kiasi gani?
 
Naam,

Mwandishi nadhani kuna kipengele aidha kakiruka kwa makusudi ama hajui au hata ameandika na wachapishaji wakaona wakiweke kapuni.

Katika kundi la Sita basi kasahau kitu. Basi mimi nitaliita kundi la saba.

Kundi la saba na la ajabu ni la waganga wa kienyeji na wapiga ramli. Rais wetu ni mwafrika halisi kwa hiyo hajakumbatia kikweli kweli dini yoyote ya kigeni. Kwa hali hiyo, si vibaya nikisema, kwa uafrika wake ni mfuasi wa siri wa dini za jadi. Hili si tusi, dhambi wala dharau. Nimemshuhudia mwenyewe kwa mazungumzo ya ana kwa ana akihangaika na kulalamika juu ya mnyukano wa dini mbili kubwa hapa nchini (Uislamu na Ukiristo) na kweli haumpi raha hata kidogo.

Anajua jinsi dini hizi mbili zinavyotuhumiana juu ya maamuzi ya rais na serikali yanayozigusa dini hizi mbili. Wakiristo wanadai kwa wazi na sirini kuwa rais anawapendelea waislam wakati waislam nao wakidai wakiristo wanapendekelewa sana na serikali ya rais wetu. Matokeo yake ni rais kukosa msimamo na kubaki kulalamika na kutilia shaka kila ushauri anaopewa na watu watokao pande hizi mbili.

Kuna “uvumi” wa muda mrefu sasa kuwa rais wetu anapata faraja pale anaposhauriwa na waganga wa kienyeji kwa sababu anaamini hawana mgongano wa maslahi katika dini hizi mbili kuu! Kimantiki na kimsingi hii ni njia nzuri ya kutatua mnyukano wa dini kubwa pale unaposhauriwa na mtu wa tatu au wa katikati.

"Uvumi" huu umeendelea kueleza kuwa katika harakati za kuwasikiliza hawa waganga, rais amejikuta njia panda katika maamuzi mbalimbali. Ushauri wa waganga humfikia rais ama moja kwa moja au kupitia wapambe maalum, lakini utekelezaji wa ushauri huo huonekana kwa njia mbalimbali kama vile tabia sugu ya rais kuchelewa katika matukio mbalimbali na tabia ya rais kutoroka na kwenda sehemu huria kama michezoni. Mara kadhaa ndani na nje ya nchi, rais amekutwa katika maeneo yasiyo rasmi bila maandalizi wala kuwamo katika ratiba. Najua rais ana maisha binafsi lakini ni ruksa kuyahoji hasa yanapoonekana kuwa rasmi kwa kuwa yanatokea mara kwa mara.

Inasemekana kuwa kwa ushauri wa waganga rais pia amejikuta katika misiba, mazishi, kutembelea wagonjwa nyumbani na hospitali, sherehe za harusi, na hafla za asasi za kiraia zenye utata. Imesikika pia waganga hawa ndiyo wanaosikilizwa hata katika masuala ya afya yake kuliko hata madaktari wa ndani na nje ya nchi.

Eneo hili limejaa “uvumi”, umbeya na maneno ya mitaani yanayochangamsha mabaraza na vijiwe, lakini cha msingi na kinachogomba ni pale yanayosemwa yanapofanana na yanayosemwa. Ikiwa uvumi huu au sehemu yake ina ukweli, basi kundi hili ndilo pekee linalomshauri mheshimiwa rais katika mambo mengi na kwa hiyo ndilo limeshikiliwa mustakabali wa taifa letu kwa sasa.

Katika mazingira ambamo makundi mengine yamenyamazishwa, salama yetu iko wapi tunapokuwa mikononi mwa hawa washauri ambao ushauri wao haujapimwa na chombo chochote kinachojulikana?

Pimbi
Mkubwa hii kali. Niliwahi kusoma kitabu kinaitwa Blood Rites, moja ya watu walioshukiwa kuwa walitumia sana ushirikina na matambiko ya kutoa watu kafara ni Idd Amini na Mobutu. Sijui viongozi wengine wanafanya nini ila waafrika hatuachi mila bwana.Pamoja na kuwa na dini zinazokataza ushirikina in secrecy tunaufanya kweli
 
Kusoma hadi Havard maana yake nini?? Hivi Mzee wa Vijisenti si naye alipitia huko na alikuwa mshauri wa Raisi na serikali kwa ujumla kwa masuala ya sheria. Sasa as Taifa tulifaidika nini kutoka huko Havard zaidi ya kulaghaiwa na kuibiwa????????? What the f`~^&%*k is Havard???
Hakuna cha Havard, Makelele, UDSM and whatever, SISIEMU na serikali yake have to go coz wamesahau mwajiri wao ni nani.

u said it all ndume! kusoma oxford na ujinga wanaoufanya havina uhusiano wowote, washauri wa rais ni wale wanywa Gahawa chini ya miti huku wakicheza bao, sidhani kama ana washauri wanaojua hali ya mambo yanavyoenda globally na kusoma alama za nyakati kwamba dunia inaelekea wapi. washauri wake ni wale wenye upeo mfupi size ya zakayo wa biblia ili waone mbele wanahitaji kupanda mnarani! 🙄😡🙁
 
Mchambuzii amefanya upembuzi yakinifuu na anastahilii pongezi.

Nimeipenda makala kwa kuelezaa kwa mapana jinsi RAIS wetu alivyojitengenezea mazingira mabovu ya USHAURI.

Kuwa kiongozi katika mazingira yenye umaskini wa kipato kwa mwananchi mara nyingi huwezesha wenye nacho kuupata. ila kikubwa katika uongozi ni tabia/hulka (character) ya mtu katika kutenda.

Tushukuru democracy as a govt by experimentation as it helps us to rectify where we failed. (Maisha bila CCM yanawezekana na demokrasia inasaidia katika hilo).
 
Washauri wa Kikwete wana uwezo mdogo sana wa kumshauri. Kwa kuwa so far hakuna lolote kubwa la maana ambalo tunaweza kusema limefanikishwa na utawala wa JK.

Ukiangalia kwa upande wa uchumi, nothing much to report, mambo ya jamii nothing much to report on, siasa kila mtu anona kuwa ni kama sandakalawe, ulinzi ndio hata usiseme, rushwa ....oh God hata kuongea haiwezekani. Sanasana tunaweza kusema amepata mafanikio ya kuridhisha kwenye timu ya Taifa.

Kwa hiyo washauri wa mambo michezo (soka) huenda ndio wamefanya kazi nzuri kwa kuwa hata matokeo katika miaka hiyo mitano yameonekana.
 
Mwandishi Maalum

Septemba 23, 2009


kikwete_2.jpg

Rais Jakaya Kikwete


Kundi la tatu la washauri

Kundi la tatu ambalo humshauri Rais kwa masuala mazito ni Idara ya Usalama wa Taifa. Tangu Rais Kikwete aingie Ikulu idara hii imekumbwa na matatizo makubwa mawili. Kwanza, historia yake na Rais huyu ni ya shaka, kwa sababu inadaiwa kuwa idara hii "haikumtaka" kuwa kati ya wagombea.

Kuna madai kwamba taarifa maalumu iliyoandaliwa na Idara kuhusu mgombea ambaye ni Rais wa sasa, haikuwa "nzuri" japo haikufuatwa na vikao vya chama.

Wengine wamedai kuwa hayo madai si chochote bali ni uzushi tu, lakini wengine wanahoji kuwa kama ni uzushi, basi hiyo ni hatari zaidi kama Idara hii haikuandika taarifa hiyo kwa jinsi ambavyo wana Mtandao walikuwa wanafanya rafu za awali katika mchakato.

Kuna uwezekano kuwa veterans ndani ya idara walikuwa wanajua wananchozungumza na kuna uwezekano mkubwa kuwa some of what we see today is the retaliation. They did not expect their "holly" suggestion to be turned down.
 
Dah jamaa kachambua kweli kweli wapambe wa January mwambie alitafute gazeti hilo alisome.
 
Dah jamaa kachambua kweli kweli wapambe wa January mwambie alitafute gazeti hilo alisome.
hivi January Makamba zaidi ya kuaandaa hotuba za raisi anayo kazi pia ya kumshauri muungwaana???

Navyojuaa muungwanaa ushaurii kwake taabu saana kwanii huwaa anawaambia alijiaandaa zaidi ya 10yrs kuwa hapo alipo na malengo anayooo...
ukiweka na matani yake ya kuumbua....vipi wewe unapenda sana takwimuuu enheeee..???
 
Naam,

Mwandishi nadhani kuna kipengele aidha kakiruka kwa makusudi ama hajui au hata ameandika na wachapishaji wakaona wakiweke kapuni.

Katika kundi la Sita basi kasahau kitu. Basi mimi nitaliita kundi la saba.

Kundi la saba na la ajabu ni la waganga wa kienyeji na wapiga ramli. Rais wetu ni mwafrika halisi kwa hiyo hajakumbatia kikweli kweli dini yoyote ya kigeni. Kwa hali hiyo, si vibaya nikisema, kwa uafrika wake ni mfuasi wa siri wa dini za jadi. Hili si tusi, dhambi wala dharau. Nimemshuhudia mwenyewe kwa mazungumzo ya ana kwa ana akihangaika na kulalamika juu ya mnyukano wa dini mbili kubwa hapa nchini (Uislamu na Ukiristo) na kweli haumpi raha hata kidogo.

Anajua jinsi dini hizi mbili zinavyotuhumiana juu ya maamuzi ya rais na serikali yanayozigusa dini hizi mbili. Wakiristo wanadai kwa wazi na sirini kuwa rais anawapendelea waislam wakati waislam nao wakidai wakiristo wanapendekelewa sana na serikali ya rais wetu. Matokeo yake ni rais kukosa msimamo na kubaki kulalamika na kutilia shaka kila ushauri anaopewa na watu watokao pande hizi mbili.

Kuna “uvumi” wa muda mrefu sasa kuwa rais wetu anapata faraja pale anaposhauriwa na waganga wa kienyeji kwa sababu anaamini hawana mgongano wa maslahi katika dini hizi mbili kuu! Kimantiki na kimsingi hii ni njia nzuri ya kutatua mnyukano wa dini kubwa pale unaposhauriwa na mtu wa tatu au wa katikati.

"Uvumi" huu umeendelea kueleza kuwa katika harakati za kuwasikiliza hawa waganga, rais amejikuta njia panda katika maamuzi mbalimbali. Ushauri wa waganga humfikia rais ama moja kwa moja au kupitia wapambe maalum, lakini utekelezaji wa ushauri huo huonekana kwa njia mbalimbali kama vile tabia sugu ya rais kuchelewa katika matukio mbalimbali na tabia ya rais kutoroka na kwenda sehemu huria kama michezoni. Mara kadhaa ndani na nje ya nchi, rais amekutwa katika maeneo yasiyo rasmi bila maandalizi wala kuwamo katika ratiba. Najua rais ana maisha binafsi lakini ni ruksa kuyahoji hasa yanapoonekana kuwa rasmi kwa kuwa yanatokea mara kwa mara.

Inasemekana kuwa kwa ushauri wa waganga rais pia amejikuta katika misiba, mazishi, kutembelea wagonjwa nyumbani na hospitali, sherehe za harusi, na hafla za asasi za kiraia zenye utata. Imesikika pia waganga hawa ndiyo wanaosikilizwa hata katika masuala ya afya yake kuliko hata madaktari wa ndani na nje ya nchi.

Eneo hili limejaa “uvumi”, umbeya na maneno ya mitaani yanayochangamsha mabaraza na vijiwe, lakini cha msingi na kinachogomba ni pale yanayosemwa yanapofanana na yanayosemwa. Ikiwa uvumi huu au sehemu yake ina ukweli, basi kundi hili ndilo pekee linalomshauri mheshimiwa rais katika mambo mengi na kwa hiyo ndilo limeshikiliwa mustakabali wa taifa letu kwa sasa.

Katika mazingira ambamo makundi mengine yamenyamazishwa, salama yetu iko wapi tunapokuwa mikononi mwa hawa washauri ambao ushauri wao haujapimwa na chombo chochote kinachojulikana?


Pimbi

Hii kali na kubwa kuliko zote!!!!
 
pimbi ni pimbi kweli lakini umesahau kwamba mwalimu nae alikuwa anasehemu yake ktk dini za jadi.
 
Makala yake iliyopita:
-------------------------------------------------------------------------
Kunyamazisha viongozi wa dini ni tambiko la ombwe la uongozi

Mwandishi Maalumu
Septemba 16, 2009


RAIS Jakaya Kikwete aliingia madarakani kwa ridhaa ya Watanzania wengi, mtaji wake ulikuwa mkubwa ukijumuisha wanazuoni, wana habari, viongozi wa dini, bunge, na hata baadhi ya vyama vya upinzani.

Kile kilichoitwa ushindi wa tsunami, kilikumba na kusomba kila aina ya upinzani uliokuwa njiani kujaribu kuchelewesha azma ya Kikwete kuingia Ikulu. Mhanga wa kwanza wa nguvu ya tsunami alikuwa Rais Benjamin Mkapa aliyeondoka kwenda Dodoma kushuhudia anguko la Kikwete akaishia kumtawaza madarakani huku roho ikimuuma.

Kwa kuwa ushindi wa Kikwete ulishadidiwa na mikakati ya ushindi kuliko ya kuongoza, katika miaka minne ya uongozi wake, tumeshuhudia mambo makuu mawili. Kwanza, ni ombwe la uongozi linaloonekana kwa njia ya yeye binafsi kutokuwa na maamuzi kwa hofu ya kuwaudhi marafiki zake waliowezesha ushindi.

Msimamo wake maarufu anaowaambia wanaomwendea kumshauri juu ya kufanya maamuzi umekuwa ni “ukiona mtu anajimaliza, usihangaike naye”. Hii pia ndiyo aliyoiita “ajali ya kisiasa” pale swahiba wake alipokumbwa na kashfa ya Richmond.

Pili, Serikali yake na chama chake vimegubikwa na makundi ya kimaslahi. Makundi haya yalianza wakati wa kampeni na yameendelea mpaka sasa na kuifanya Serikali yake itumie muda mwingi na rasilimali nyingi kutatua migogoro badala ya kuongoza.

Nyufa hizi mbili, zimemfanya Rais Kikwete hivi karibuni kufanya jambo la kihistoria pale alipozuia viongozi wa dini kutoa miongozo kwa waumini wao kwa hofu ya kuwa wanaigawa nchi. Napenda katika makala hii, nijadili zuio hili la kihistoria.

Hapana shaka sasa kuwa pale Kingunge Ngombale Mwiru alipolikemea Kanisa Katoliki kwa kutoa waraka au mwongozo wa elimu ya uraia alikuwa ametumwa. Kingunge, mshauri wa siasa wa Rais Kikwete alikuwa anakariri yale aliyokuwa ametumwa. Alipopuuzwa ndipo Rais kaja na zuio. Lakini huyu ni Rais aliyeungwa mkono na viongozi wa dini wakati wa kampeni na baadaye kiasi cha kuitwa “chaguo la Mungu”.

Wakati huo hakuona kuwa wanaigawa nchi, lakini sasa wanapotoa elimu ya uraia ili lipatikane “chaguo la Mungu” jingine ya hili la sasa liendelee kuongoza, Rais anaona nongwa.

Katika hali ambayo imekuwa ikitafsiriwa kuwa viongozi wa dini wanaziba ombwe la uongozi katika nchi, ni rahisi mtu kudhani kuwa Rais ametambua ombwe hilo la kuamua kuwanyamazisha ili aonekane kuwa bado anaongoza nchi. Njia hii ya kuongoza kwa kunyamazisha haina tija, inaweza kunyamazisha hata sauti za kumwambia yeye mwenyewe hatari inayomkabili.

Katika kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa njia ya televisheni wiki iliyopita, Rais kwa namna ya pekee amegusia mazuio kwa makundi makuu matatu. Magazeti ya Serikali kwa umakini mkubwa yaliripoti mazuio hayo huku magazeti yasiyo ya Serikali yakipuuza mazuio hayo. Kundi la kwanza ni la viongozi wa dini pale Rais aliposema madhehebu ambayo hayajatoa matamko yasifanye hivyo.

Hii ina maana yale matamko yaliyo tayari kwenye mzunguko ama hayana maana au ndiyo pekee yaruhusiwe kutumika. Kundi la pili, ni la wabunge wapinga ufisadi. Rais alishindwa kushawishi wasikilizaji kuwa Halmashauri Kuu ya CCM haikuwazuia wabunge hao kuendelea na harakati zakupinga ufisadi. Zuio la Rais kuhusu wabunge hao ni pale anapowataka wabunge kuangalia maslahi ya chama badala ya maslahi ya nchi.

Kwa kuwa ni wazi sasa kuwa minyukano iliyo ndani ya CCM si ya kiitikadi bali ya kimaslahi, zuio la NEC na Mwenyekiti kwa wabunge linasimika rasmi ufisadi ndani ya CCM. Kinachogombaniwa ndani ya CCM si kama CCM ni chama cha kijamaa au kibepari, bali ni mgongano wa nani kala nini na wapi? Kama wabunge wote wangepata mgawo wao sawasawa tusingeona minyukano inayoendelea ndani ya chama hicho kikongwe.

Kundi la tatu lililoguswa na zuio la Rais ni la wana habari. Akijibu swali kuhusu uhuru wa vyombo vya habari, Rais kwa uswahili na kwa mizaha ya hapa na pale kama ilivyo kawaida yake aliwatisha waandishi wachokonozi kuwa “wakidiriki” kuchokonoa na kutikisa mustakabali wa nchi na maslahi ya watendaji wake watakiona cha mtema kuni.

Kwa mtu yeyote anayeitakia mema nchi hii, hawezi kupuuza mazuio haya ya Rais kwa makundi tajwa kwa sababu yakitekelezwa hata Rais mwenyewe hawezi kuwa salama. Usalama na ustawi wa Rais kama taasisi, ni pale uhuru wa kutoa maoni unaposhamiri, si unapofinywa kama ambavyo Rais anaelekea kuelekeza.

Nikirejea tena katika zuio la Rais kwa viongozi wa dini, napenda nisajiri masikitiko yangu juu ya sababu aliyoitoa Rais kuhusu zuio hilo. Alisema kuna hatari kuwa Watanzania wataenda kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwakani kufanya uchaguzi wa maelekezo ya dini zao.

Mtu aweza kufikiri Mheshimiwa Rais alisoma nyaraka hizo na kubaini hatari hiyo ndipo akaweka zuio la nyaraka zaidi kutoka madhehebu mengine. Na dawa ya hatari hii, Rais anaona ni kuwaita viongozi wa dini na kukutana nao ili “kuwafundisha” namna nzuri ya kutoa nyaraka zao au “kuwafundisha’ wasiwafundishe waumini wao namna ya kupiga kura.

Ikiwa hili ndilo kusudi la Rais kuwaita viongozi wa dini, tukubaliane mambo machache kabla ya mkutano huo unaosubiriwa na wachache. Jambo la kwanza, upo uwezekano Rais hajasoma nyaraka hizo na hivyo kutegemea maelezo ya wasaidizi wake. Hili si jambo la ajabu kwa sababu si mara ya kwanza kumwona Rais akizungumzia mambo anayoonekana hayaelewi sawasawa.

Mathalani katika kujibu swali la makundi ya CCM, Rais anakataa kuwa hakuna makundi bali uhasama uliopindukia. Kutokujua kuwa kuna makundi ndani ya CCM ni hatari kuliko makundi yenyewe; hali hii ikiendelea uhai wa CCM u shakani.

Jambo la pili, yawezekana Rais ameusoma waraka wa Kanisa Katoliki ambao umehaririwa na vijana wake wanaopenda usomeke kama Rais alivyousemea mbele ya Watanzania usiku ule. Kwamba, kuna njama za makusudi kumpotosha Rais kwa makusudi ya kumchonganisha na viongozi wa dini, maana waraka ule tumeusoma na hakuna mahali unasema Wakatoliki wachague Wakatoliki au Wakiristo.

Je, Rais kweli amechukia waraka unaoelekeza watu wasichague mafisadi? Na je, mafisadi wako CCM tu? Mbona ni CCM inayoonekana kuupigia kelele waraka huu? Jambo la tatu, Rais anafikiri kimya cha viongozi wa dini kuhusu hali ya nchi kinaweza kuongeza udhibiti wake katika hatamu za nchi- yaani kelele za viongozi wa dini zinapunguza mamlaka na madaraka yake kwa nchi?

Kwa Mheshimiwa Rais, madaraka na mamlaka ni bidhaa adimu ambayo hataki kuigawana na viongozi wa dini kwa kuhofia itaisha? Madaraka na nguvu ya ushawishi katika nchi hii ni kwa mgawo kama umeme wa Tanesco! Rais hana mshauri au muonaji wa kumjulisha kuwa kuongoza Taifa lenye viongozi wa dini walio kimya ni mzigo mzito usiobebeka?

Hata Bwana Yesu (Nabii Issa) aliwahi kuwaambia Wayahudi waliokerwa na kelele za wafuasi wake, kuwa “hawa wakinyamaza, mawe yatapiga kelele”. Siku za karibuni tumeona wanafunzi wakipiga kelele, walimu wakipiga kelele, watumishi wa reli, madaktari, watoto wa shule za msingi, wamasai wa Loliondo, wana habari, viongozi wa dini, na wabunge wa kweli. Taifa lililo hai ni lile linalopiga kelele. Zuio la Rais kwa viongozi wa dini ni la hatari sana na halina wema ndani yake.

Mheshimiwa Rais anapaswa ajue kuwa Tanzania ni kubwa sana na hatari ya Watanzania wengi kutotendewa haki ni wazi. Uwezo wa Rais kujua kila mara nini kinaendelea pembezoni mwa nchi achilia mbali hata katika baadhi ya maeneo yaliyo ndani ya Dar es Salaam si mpana kiasi hicho.

Rushwa na ufisadi ni mtindo wa maisha ya kila siku katika maeneo mengi. Taasisi za kiserikali na hata vyombo vya dola na vya utoaji haki vimevuka viwango kwa vitendo vya rushwa na hali ya kukata tamaa miongoni mwa Watanzania wengi inaongezeka kila siku.

Mtindo wa kushughulikia matatizo ya watu kwa njia ya operesheni haukidhi mahitaji. Matokeo yake ni misururu ya watu kuelekea Ikulu kueleza matatizo yao moja kwa moja kwa Rais kana kwamba watendaji wengine wa ngazi za chini ya Rais hawapo.

Mtu masikini wa kipato na asiye na jina hana uwezekano wa kupata haki. Tumeona wenyewe siku za karibuni kuwa ili kesi yako isikilizwe haraka inabidi uwe na fedha au uwe unajulikana. Mifano ni mingi: Ditopile Mzuzuri (marehemu) Abdallah Zombe, Costa Mahalu, Basil Mramba, Daniel Yona, na Grey Mgonja.

Tumesikia pia habari ya Mbunge mmoja mkoani Morogoro anayetuhumiwa kumpiga mtumishi wa Idara ya Maji jalada la uhalifu wake likipelekwa kwa DCI Robert Manumba badala ya Polisi kumpeleka mahakamani moja kwa moja.

Ni kana kwamba tuna mifumo miwili ya kisheria katika nchi moja. Mfumo mmoja kwa watu wanaopelekwa mahakamani bila kibali cha DCI na wale ambao wakifanya uhalifu inabidi kwanza iombwe ruhusa kabla ya kuwafikisha mahakamani.

Kutokuwa na haki sawa mbele ya sheria kunaleta mbinyo na msongo wa mawazo kwa Watanzania wengi. Mbinyo huu unapoendelea kwa muda mrefu, ndio unaowapa viongozi wa dini jukwaa la kusemea, ndio unaowapa wana habari uwanja mpana wa kuchambua jamii na ndio unaowapa wabunge nguvu ya dhamiri kusemea kile kisichopendwa na chama chao.

Masikini wa Tanzania husemewa na viongozi wa dini, wana habari na wabunge wenye dhamiri safi. Kwa zuio la mheshimiwa Rais, masikini wa Tanzania wasiwe na msemaji wala mtetezi maana kufanya hivyo ni kuhatarisha umoja wa kitaifa.

Umoja wa kitaifa ni ule wa kutowasumbua mafisadi na kuwachagua kila baada ya miaka mitano bila kuwadai uwajibikaji. Mpaka hapa natamani Mheshimiwa Rais aondoe zuio lake kwa viongozi wa dini, wana habari na wabunge wapingao ufisadi, na badala yake ajiunge nao kutetea wanyonge hawa na kuwarudishia heshima yao.

Kinachoendelea ndani ya Taifa ni zaidi uwepo wa ombwe la uongozi kama ambavyo imenukuliwa mara kwa mara na watu mbalimbali. Kwangu mimi, ombwe linakuwapo pale ambapo kwa sababu za kimfumo, uongozi uliochaguliwa unakosa haiba na ujasiri wa kuongoza taifa kutokana na mazingira yanayounyima uongozi huo fursa ya kufanya hivyo.

Ombwe la namna hiyo huzibwa ama pale uongozi huo unaposema “sasa basi” na kujikomboa kikweli kweli kutoka katika makucha ya wale waliouweka rehani au kelele zinapojitokeza za kuutaka usome alama za nyakati.

Kinachoonekana katika taifa letu kwa sasa, ni uongozi unaohofia kisichokuwapo bado huku ukipuuza kilichopo tayari. Mathalani, Serikali kupitia kwa Rais inahofia viongozi wa dini kujihusisha na utoaji elimu ya uraia kuwa watahatarisha umoja wa kitaifa, huku Serikali hiyo hiyo ikipuuza hatari ya ujinga wa wananchi wengi kuhusu elimu ya uraia.

Kwa maana hiyo, tunajivumia mamilioni ya Watanzania wanaobaki gizani bila kujua haki zao katika kushiriki michakato mbali mbali ya kidemokrasia. Lakini ujinga unaoshangiliwa sasa kesho unaweza kugeuka kuwa silaha ya maangamizi ya taifa.

Kule bungeni aliyetangaza zuio kwa viongozi wa dini kutokutoa nyaraka au kuondoa zile zilizo katika mzunguko alikuwa mzee Kingunge. Mzee huyu baadaye alisikika akisema kwamba wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, hali hii isingeruhusiwa kuendelea. Sijaona popote mzee huyu alipokosolewa juu ya tamko lake hili lisilo na ukweli wote.

Mwalimu Nyerere aliipenda Tanzania na hata maadui wake walimheshimu kwa hilo. Walimsema mengi yasiyopendeza, lakini hawakutilia shaka uzalendo wake kwa taifa hili wala upendo wake kwa Watanzania.

Nadiriki kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliipenda Tanzania kuliko familia yake, dini yake na hata chama chake. Tulimwona akiwatosa marafiki zake walipopingana na msimamo wa kujenga jamii ya Kitanzania isiyovumilia aina yoyote ya ufisadi.

Wakati fulani tulishuhudia hata Mwalimu Nyerere akitofautiana na Mama Maria pale alipobaini au kuhisi masuala ya familia yanaanza kuingilia masuala ya kitaifa. Kwa hiyo, kama ilitokea Mwalimu akawakaripia viongozi wa dini (kama aliwahi kufanya hivyo), alifanya hivyo ili kulinda maslahi ya Taifa na si pungufu ya hilo.

Sasa tujiulize, zuio la Rais kwa viongozi wa dini kutokutoa tena nyaraka za kuelimisha waumini juu ya elimu ya uraia lina manufaa kwa Taifa? Je, umoja anaodai kuulinda Rais bado upo?

Siwezi kudai kujibu maswali haya mawili kwa usahihi, lakini itoshe kusema ya kuwa zuio hili linawanufaisha mafisadi na viongozi miungu-watu. Linawanufaisha watu wachache waliozoea kupata uongozi wa kuchaguliwa kwa njia ya kununua kura na kulaghai wananchi wasioelewa.

Zuio hili linalenga kuimarisha tabaka la watawala (CCM) dhidi ya watawaliwa (Watanzania masikini wa vijijini). Ni hawa watawaliwa waliolengwa kuelimishwa na nyaraka za viongozi wao wa dini na elimu hii ilikuwa ni ukombozi kwao. Rais wao waliyemchagua kwa kura nyingi amezuia wasipate elimu hii wasije wakaasi na kuanza kuhoji.

Kuhusu ikiwa umoja anaoulinda Rais kwa kuweka zuio la kutokutoa nyaraka nyingine, nachelea kusema haupo kwa sasa. Tanzania ya sasa imegawanyika katika matabaka makubwa manne ya kiuchumi, kijamii na kimaeneo.

Tabaka la kwanza ni la watu wa mijini dhidi ya watu wa vijijini. Ukikutana na Mtanzania siku hizi ni rahisi kujua huyu wa mjini na yule wa kijijini kwa jinsi anavyofikiri, anavyoamua na hata kutembea. Mgawanyiko huu ni mtaji mkubwa wa wanasiasa kwa sababu tofauti yake kubwa iko katika uelewa (knowledge).

Tabaka la pili ni la kipato, yaani kati ya walio nacho na wasio nacho. Umasikini wa kipato umeigawa Tanzania katika makundi haya mawili, moja likizidi kuwa dogo kueleka juu, na jingine likiongezeka kwa kasi kuelekea chini. Sihitaji kulisemea sana hili maana Mwalimu Nyerere alilisemea katika uhai wake, na hivi karibuni mzee mmoja mashuhuri, mfuasi wa Mwalimu Nyerere, Ibrahimu Kaduma ameliandikia kitabu.

Tabaka la tatu ni lile la wanawake na wanaume. Haishangazi sana kuona kuna mafisadi wanawake wachache, na pia kuona kuwa mafisadi huwakimbilia sana akina mama wakati wa uchaguzi wowote. Kundi la akina mama lina masikini wengi wa kila sura na pia kwa wingi wao hugeuka kuwa mtaji wa kisiasa.

Katika hali ambayo tumeruhusu rushwa iamue nani achaguliwe, tabaka hili ni nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kweli.

Tabaka la mwisho kwa mtizamo wangu, ni lile linaloibuka kwa kasi kati ya vijana wanaosoma Shule za Kata na wale wanaosoma shule binafsi za watakatifu. Shule aliyosoma mtu inaanza kuamua aina gani ya kazi apate na shirika gani afanyie kazi.

Sijatoka nje ya mada yangu kwa kuchambua matabaka haya nikijaribu kueleza kuwa umoja wa kitaifa anaodai kuulinda Rais kwa kuwaziba midomo viongozi wa dini, wana habari na wabunge wapinga ufisadi haupo kabisa.

Kilichopo kwa sasa ni harakati za matabaka na minyukano ya kimaslahi iliyosababishwa na tabia ya tabaka moja kula bila kunawa. Baada ya miongo kadhaa ya matabaka haya kusigana kimya kimya kama alivyobaini Profesa Issa Shivji (Silent Class Struggle), kwa sasa matabaka haya yananyukana waziwazi ili kunyakua kombe moja la thamani.

Kombe hilo linaloshindaniwa si jingine bali Mheshimiwa Rais mwenyewe. Kila tabaka linadai Rais yuko upande wake huku naye akipata kigugumizi kujitambulisha na kundi lolote na hali hii kwa maoni yangu ndiyo inayotishia umoja wa kitaifa – si nyaraka za viongozi wa dini.

Mzee mmoja ninayemheshimu sana ndani ya Serikali, baada Rais kutamka kuwa hakuna makundi ndani ya CCM ameniambia kuwa “Rais asiye na kundi kwa sasa hatufai”.

Viongozi wa dini wanaozuiwa kutoa nyaraka nyingine walikuwa wanajaribu kusemea na kutetea maslahi ya tabaka la wanyonge. Uamuzi huu haukumpendeza Rais na akaamua kuwazuia. Kwa kuwa madaraka (mandate) ya viongozi wa dini haitokani na Rais, nabakia kuamini kuwa viongozi hawa hawatakaa kimya na kuusaliti utii wao kwa Mungu.

Sasa tumeanza na kuzuia nyaraka za kichungaji, kesho tutataka mahubiri ya viongozi wa dini yapelekwe Ikulu kabla hayajasomwa, keshokutwa tutataka viongozi waongezewe idadi ya nadhiri wanazoweka kwa kumtii Rais wa Jamhuri.

Hatimaye siku moja mtu anaweza kutaka kichwa cha kiongozi kwenye sahani. Mnashangaa? Hii haitakuwa mara ya kwanza, Herode alikwisha kutangulia!

Ukiona kuwa ilani mbalimbali za vyama vya siasa, tena zilizo tofauti kabisa, hazigawi watu, lakini ukaona miongozo ya dini ni ya hatari, wewe ni wa hatari kuliko hatari yenyewe.

Namheshimu sana Rais Kikwete lakini kwa hili natamani kabisa avunje kabisa mpango wake wa kukutana na viongozi wa dini kuwafundisha wajibu wao. Kama ana la kusema, atoe mwongozo ulioandikwa kama viongozi wenyewe walivyofanya, na awaachie wananchi waamue lililo jema kwa mustakabali wa Taifa. Mkutano wa Rais na viongozi wa dini utamvunjia heshima yake iliyobaki.



Mwandishi wa makala hii amejitambulisha kuwa ni msomaji mzuri wa Raia Mwema na mmoja kati ya viongozi wa Ukiristo nchini. Barua Pepe: msomajiraia@yahoo.co.uk, Simu: 0712881704
 
Huyu mchungaji nimesoma makala zake zote mbili lakini kuna wakati anatawaliwa na jazba kidogo kwa mfano anaposema Mheshimiwa Raisi anauswahili na mizaha ya hapa na pale, sikubaliani naye.

Nafikiri mwandishi ni mchambuzi mzuri sana wa mambo lakini anapaswa kujitahidi kutokutoa maneno yasiyo na staha kama vile hapa chini, namnukuu:

"Rais kwa uswahili na kwa mizaha ya hapa na pale kama ilivyo kawaida yake..."
 
Mwandishi Maalumu
Septemba 30, 2009

WIKI iliyopita niliahidi kuwa makala ya wiki hii itahusu ugumu wa kumshauri Rais Jakaya Kikwete katika mazingira ya sasa yaliyofanywa kuwa magumu kama nilivyobainisha katika makala mbili zilizotangulia.

Utete wa mahusiano kati ya Rais Kikwete na viongozi wa dini, wanaharakati, wana habari na wapinga ufisadi ni sehemu ya ugumu wa kumshauri.

Lakini pia kama tulivyoona, fursa ya makundi mbalimbali kumshauri imeteleza upesi na kutokomea kutokana na sababu za kihistoria na ki-haiba (personality) ya Mheshimiwa Rais mwenyewe. Kana kwamba hiyo haitoshi, ziko sababu nyingine kadhaa zinazofanya mazingira ya kumshauri Rais yawe magumu. Nitataja chache katika makala hii.

Baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kustaafu urais na kubakia kuwa mwenyekiti wa chama, nilipata bahati ya kutumwa naye na wenzangu wawili, kwenda kumjulia hali rafiki yake mmoja aliyekuwa anaumwa, lakini wakati huo akiendelea kuongoza chombo muhimu cha dola katika taifa moja la Afrika.

Tulipofika, tulikuta ugomvi ambao hata mkuu wa nchi ile alikuwa amejaribu kusuluhisha bila mafanikio.

Ugomvi ulihusu nafasi ya waganga wa kienyeji katika kumshauri mkubwa yule juu ya afya yake. Mara mbili alipelekwa hospitalini Ulaya na Marekani, na madaktari walishauri afanyiwe upasuaji lakini kila alipoandaliwa kwa ajili hiyo, alibadili mawazo dakika za mwisho na madaktari waliheshimu uamuzi wake.

Kisa cha kubadili kilikuwa ni ushauri wa waganga wa kienyeji kuwa wazungu wanataka kumuua kupitia upasuaji huo. Mkubwa yule aliendelea kudhoofu kwa kuchelewa kufanyiwa upasuaji kwa sababu tu waganga wa kienyeji wametoa ushauri na ukaheshimika.

Hatimaye waganga hao walihamia nyumbani kwa mkubwa yule, wakapewa gari lao maalumu katika misafara ya mkubwa yule. Washauri na wasaidizi wakapuuzwa na hata ushauri wa marafiki kama Mwalimu Nyerere haukufua dafu.

Nalisema hili kusisitiza jambo moja muhimu kuwa, viongozi wengi wa Kiafrika wanajiweka katika mazingira magumu ya kushauriwa pale hofu inapowatawala na hatimaye kujisalimisha kwa washauri wasio rasmi kama hawa.

Tulipomweleza Baba wa Taifa juu ya yaliyotukuta alicheka sana na kutukumbusha kuwa “Waswahili” hawaachani na jadi yao. Akatukumbusha kuwa hata yeye alipokutana na wazee, lilikuwa halianzi jambo mpaka tambiko lifanyike! Siamini kwamba katika hofu iliyogubika makundi ndani ya chama na serikali kama kweli hatujafika huko.

Hofu ya namna hiyo, haiwezi kuruhusu Rais apate ushauri usio na shaka.

Siku moja nilifuatana na mtu mmoja kwenda Ikulu kuomba kuonana na Mheshimiwa Rais ili amshauri Rais juu ya jambo ambalo mpaka wakati huu hakupata kuniambia.

Nilikubali kumsindikiza baada ya yeye kuzungumza na maofisa wa Ikulu na kuwaambia kuwa angekwenda na mtu mwingine ambaye ni mimi.

Kwanza nilishangaa kuona kuwa hata kuweka miadi ya kuonana na Rais ni lazima mtu aende mwenyewe kuonana na maofisa. Nilidhani kwa ujinga wangu, angepewa siku au kunyimwa bila kulazimika kuambiwa aende kwanza Ikulu.

Tukiwa ofisini kwa ofisa wa kutoa miadi hiyo, alifika ofisa mwingine na baada ya kuambiwa kuwa ndugu yangu niliyefuatana naye alihitaji kuonana na Rais ili ampe ushauri fulani, aliulizwa swali “Wewe unataka kumshauri Mheshimiwa Rais, lakini wewe umejishauri”?

Swali hilo lilinitesa sana siku hiyo. Nikahisi kuwa mazingira ya kumshauri Rais ni magumu ikiwa wasaidizi wake wanafanya mizaha katika wajibu wao kiasi hicho. Linapofika suala la mwananchi kupenda kumpa ushauri mkuu wa nchi, mizaha na kejeli vingewekwa pembeni na kuwa makini kusikiliza watoa ushauri. Mpaka leo naamini, kumshauri Rais Kikwete inabidi ujishauri mara mbili kwa sababu zifuatazo:

Rais Kikwete

Rais Kikwete

Kwanza, Rais Kikwete anaongea sana kuliko kusikiliza. Tabia hii pia ilionekana siku alipozungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kwa kujibu maswali ya papo kwa papo.

Ilibidi wakati fulani, Tido Mhando ajaribu kuingilia kumsimamisha au kumshtua lakini akafanya kwa woga na Rais hakushtuka.

Rais mwongeaji sana kama yeye anapoteza fursa nyingi za kushauriwa kwa sababu badala ya kushauriwa, yeye ndiye anatoa ushauri. Tabia hii pia anaiendeleza anapoongoza vikao vya chama na hata baraza la mawaziri.

Baadhi ya mawaziri wake wamesikika wakilalamika kuwa vikao vya baraza haviishi wala kumaliza agenda kwa sababu Rais anazungumza muda wote na wao wanalazimika kurudi wizarani kwao na madokezo kutoka kwa makatibu wakuu wao.

Wengine wamedai Rais ana mawaziri vipenzi wake ambao anakuwa amekwisha kuzungumza nao na wakifika kwenye baraza wao husimama na kusema “Mheshimiwa Rais kama niliyokwishakudokeza”.

Hali hii huwafanya mawaziri ambao ni washauri wakuu wa Rais wabakie kumskiliza Rais awaambie kile alichodokezwa na waziri wake kipenzi. Matokeo yake, mawaziri hurudi wizarani kwao na ushauri wao kwa sababu tu, Rais anaongea sana kuliko kusikiliza.

Pili, Rais hasomi ripoti au hana muda kabisa wa kuzisoma. Washauri wengi wa Rais hutoa ushauri wao kwa njia ya maandishi (ripoti maalumu au madokezo).

Ni wachache wanaofanya kwa kutumia maneno matupu (umbeya na udaku).

Kwa hiyo Rais hana budi kuwa msomaji mzuri wa ripoti. Rais asiyesoma hutegemea “briefings” au “executive summaries” na hii ni hatari sana kwani si ukweli wote waweza kuwekwa katika briefings. Ukitilia maanani kuwa Rais wetu ni msafiri na imeonekana wazi akiwa safarini pia hasomi kazi za ofisini, basi anakatisha tamaa washauri wanaotumia muda mwingi kuandaa ripoti hizo.

Uwezekano wa kukasimu madaraka ya kusoma na kufanyia kazi ripoti hizo ni mgumu kwa sababu kinga ya maofisa hao si za uhakika endapo utekelezaji wake utaleta mgogoro au kashfa baadaye.

Tatu, timu ya washauri wa Rais katika masuala mengi yaliyo nyeti imejaa watu ambao uwezo wao unatia shaka (mediocres).

Hii ni kwa sababu ama Rais hakuwa makini katika uteuzi au washauri hao walisukumizwa kwake na marafiki kama njia ya kulipa fadhila.

Tumewaona hawa washauri na wasaidizi wa Rais katika matukio mengi ya kimataifa na kitaifa na utendaji wao unazua maswali.

Kuna wakati tumemwona Rais mwenyewe akilazimika kuingilia hata masuala mengine hasa ya kiitifaki kwa lengo la kuepusha aibu na fedheha kwa nchi.

Tabia moja kubwa ya “mediocre” huwa ni kushauri kwa kuigiza mambo waliyoyaona sehemu nyingine, na mara nyingi hupenda fitna ili Rais asishawishiwe na ukweli aliousikia kwa watu wengine.

Mifano halisi ya maamuzi ya Rais na Serikali yanayotokana na ushauri usiotokana na weredi wa washauri ni kama vile uamuzi wa kupitia upya mikataba ya madini, ufutaji wa misamaha ya kodi kwa taasisi zisizo za kiserikali, kubadilika badilika kwa taratibu za utoaji mikopo ya elimu, ugawaji wa mamilioni ya JK, umeme wa dharura la kashfa ya Richmond, n.k.

Nne, Rais wetu ana marafiki wengi wa sasa na wa zamani. Marafiki wengi huongeza ugumu wa kumshauri rais yeyote kwa sababu ya ugumu wa kubaini mambo binafsi ya kiofisi. Hali hii ikitokea humchanganya rais na washauri wake.

Inapotokea kuwa rais mwenyewe hapendi kuwahudhi marafiki zake, basi marafiki hao hugeuka kuwa marafiki wa taifa badala ya kuwa marafiki binafsi wa rais.

Najua na nimemwona Rais akikana na kuwaonya wote wanaotumia jila lake kwa maslahi binafsi, lakini anapofanya hivyo hata yeye mwenyewe haamini kama anafanya kweli.

Anapokuwa mikoani hujiatahidi sana kukumbuka kila mtu aliyewahi kukutana naye, na pia marafiki zake wa zamani huingilia ratiba ili kuonana na Rais.

Madhara ya tabia hii si tu yanawachanganya washauri, bali pia yanamweka Rais mwenyewe katika wakati mgumu anapolazimika kutoa ahadi zilizo nje ya utaratibu kama vile kusaidia gharama za matibabu, kurejesha kazini waliofukuzwa kazi zamani, kutoa ajira, kurudi kutembelea eneo hilo tena na hata kualika watu waje kumwona.

Kwa ufupi, marafiki wamekuwa wachafuzi wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Rais anaposhauriwa juu ya tatizo hili, yeye husema “marafiki wanaochafua kazi yake waache wajipoteze wenyewe”. Hayuko tayari kuachana nao japo yuko tayari wao ndio wamwache kama wamekata tamaa naye.

Katika kuhakikisha hili linafanyika, Rais huwajengea mazingira magumu marafiki zake ili wasikate tamaa haraka.

Njia anayotumia ni kuuma na kupuliza na wakati mwingine kuwatumia mawasiliano yanayopingana na alichokisema hadharani.

Baadhi ya marafiki zake wanatukuza mawasiliano hayo na kuyaenzi kama alama ya urafiki wa kudumu na Rais.

Katika mnyukano wa makundi unaoendelea bungeni, baadhi ya wabunge wanaokerwa na tabia ya marafiki wa Rais, wamekuwa wakilalamika kuwa marafiki hao wa Rais wanawatambia kuwa watakufa na umasikini wao kwa sababu tu wamezubaa na ndiyo maana sasa wanawaonea wivu wenzao waliofanikiwa.

Siku Mwadhama Kardinali Policarp Pengo aliposema wanaopiga kelele za ufisadi wanaweza kuwa wanafanya hivyo kwa wivu wa wao kukosa kufisadi, marafiki wa Rais walifanya sherehe na kushangilia kuwa hatimaye hao wabunge wenye roho ya “korosho” wamepata vipande vyao.

Nihitimishe sehemu hii kwa kusisitiza tu kuwa marafiki wa Rais kwa idadi yao na tabia yao, ni kikwazo cha kumshauri Rais Kikwete.

Tano, ili kumshauri Rais ni vema ikafahamika kwa washauri wake walio rasmi kuwa anasimamia mambo gani ya msingi katika utawala wake.

Ni vigumu sana kumshauri rais ambaye kwake kila kitu ni cha muhimu, yaani hana vipa umbele na hajajipambanua kikweli kweli kuwa anasimamia mambo fulani. Kutofahamika kwa rais huitwa “kutotabirika”.

Lakini hili kwa Rais wetu ni dogo, kubwa zaidi ni kutoaminika kwa mambo ya msingi na kuaminika sana kwa mambo madogo ya kawaida.

Mathalani Rais huyu anaweza kuchelewesha kuamua jambo zito lenye maslahi kwa Taifa, lakini hawezi kuchelewesha kutimiza ahadi ya kutoa tiketi ya ndege ya rafiki yake kwenda India kwa matibabu.

Hili atalikumbuka na hata usiku litamuamusha kuwaagiza wasaidizi.

Hata kama unaoshughulikiwa ni uhai wa mtu, lakini pia inatia shaka mkuu wa nchi anapomsahau mshauri wake anayemsubiri sebuleni tayari kwa kumpa “briefing” ya maslahi ya taifa lakini rais huyo huyo akasimamisha msafara au kuchelewesha msafara ili atoe pongezi kwa mtoto wa rafiki yake aliyehitimu kidato cha sita.

Baadhi ya wasaidizi na washauri wa Rais Kikwete wanakatishwa tamaa wanapofika Ikulu kutoa ushauri au ripoti lakini wakaambiwa Rais hana nafasi, warudi siku nyingine, lakini wakaja kumwona Rais akitoa nafasi kwa marafiki au marafiki wa marafiki zake wamwone kwa mambo ya binafsi.

Baadhi ya marafiki zake hivi sasa wanatumia mwanya huo vibaya. Rais asiyetabirika wala kuaminika, huwaweka washauri wake katika mazingira magumu sana ya kazi yao.

Sita, taifa changa kama la kwetu linamhitaji rais aliyeiva katika itikadi fulani ili awe dira ya watu na taasisi zake.

Naelewa hili ni suala tata kwa sasa lakini utata wake haupunguzi umuhimu wake.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alijaribu kujenga Ujamaa na Kujitegemea. Waliofuata wakabomoa lakini hawakujenga kipya bali wakawa wajasiriamali na makuwadi wa soko huria.

Kipekee Rais Benjamin Mkapa alizungukwa na washauri waliouonea aibu Ujamaa na kuuonea fahari Ubepari wa soko huria.

Kwa hiyo, walimshauri rais waliyejua kwa hakika kuwa ameongokea Ubepari na kuachana na Ujamaa, na yeye hakuona aibu kusema na kutetea misingi ya dini yake mpya.

Mkapa atalaumiwa kwa mengine, si kwa kukosa msimamo katika masuala anayoyaamini na kuyatetea.

Rais Kikwete hajulikani kama ni mjamaa au ni bepari. Alifanya kampeini kwa lugha ya kijamaa, akitangaza ana nyumba moja, tena ya mkopo.

Walio karibu naye kuliko mimi wanasema siku ya kutangaza kugombea Urais alikuwa na hazina ya shilingi milioni mbili na nusu. Kilichotokea ni mabepari kuteka kampeini zake na hatimaye kumfanya abaki njiapanda ya itikadi.

Washauri wake wote wako njia panda maana hawajui Rais wao anapenda nini.

Amesikika mara kadhaa akisema nchi haiwezi kurudi katika enzi za mgawo wa colgate na sukari lakini wakati huo amesikika mara kadhaa akiomboleza juu ya umasikini wa Watanzania.

Rais anayeomboleza kwa kuwaona masikini wanaoongezeka wakati akiogelea katika utajiri usio na maelezo, anawajengea mazingira magumu washauri wake.

Yeye akiwa mchumi anapaswa ajue kuwa sehemu kubwa ya majibu ya umasikini wa Watanzania, yamo katika utajiri wa marafiki zake waliomzunguka.

Kukosekana kwa itikadi ya Rais kumezua mitafaruku mingi katika chama na Serikali anayoiongoza. Mpaka sasa Rais haaminiki na kundi lolote, liwe la mlengo wa kijamaa au kibepari, bali anakubalika na kuaminiwa na watu binafsi katika makundi hayo mawili. Kundi kama kundi halimwamini lakini watu binafsi wanaendelea kumwamini kwa shaka isiyotamkwa wazi.

Nilikuwa Dodoma usiku ule wa kumpata mgombea Urais kupitia CCM. Kila mtu anaweza kueleza kwa urefu mambo yaliyojiri huko Dodoma. Ni usiku wa kukumbukwa kwa mengi.

Baadhi ya wagombea urais, hawapendi kukumbushwa matukio ya juma lile na hasa usiku huo. Rais wetu hupenda sana kuyakumbuka na kuyazungumzia wakati anapokuwa anaongea na watu katika mazungumzo yasiyo rasmi. Yeye huita hayo kuwa ni “mchezo wa siasa”.

Nadhani haelewi jinsi mchezo huo ulivyoumiza wengi na kuiweka Serikali yake katika mazingira magumu sana kiushauri.

Walipobakia wagombea watatu wa mwisho – Salim Ahmed Salim, Kikwete na Profesa Mark Mwandosya na kisha wakapewa dakika chache za kuomba kura kwa mara ya mwisho, Profesa Mwandosya alisema maneno yaliyovutia usikivu pale aliposema, Rais atakayechaguliwa ni mtu wa muhimu sana.

Ni huyo anayeweza kuamua nchi iende vitani, ikaenda. Ni yeye anayeweka sahihi mtu anyongwe, akanyongwa.

Akawataka wajumbe wafanye uchaguzi wenye busara kwa sababu anayechaguliwa ana dhamana ya uhai wa Taifa na uhai wa watu.

Jirani yangu alininong’oneza kwa kusema, “nitampigia Kikwete, lakini naona maneno ya Mwandosya yamenigusa sana.”

Wako watu wengi pia walioguswa na maneno ya Salim na niliwashuhudia wakitoa machozi ya uchungu. Kilichofanyika Dodoma usiku ule, ndicho kwa mantiki ya makala zangu tatu, kimeleta linaloitwa ombwe la uongozi kitaifa, ndicho kinachomnyima Rais washauri wazuri, na ndicho kinachozidi kuharibu mazingira ya Rais kushaurika. Tufanye nini?

Rais ni alama ya mshikamano wa taifa. Rais ni msingi wa mwelekeo wa taifa. Rais ni afya ya taifa, ndiyo maana ugonjwa wa rais kimsingi ni ugonjwa wa taifa. Hii ni dhamana kubwa kupewa mtu mmoja aliyezaliwa na mwanamke.

Ni vema Watanzania wakatambua na kama wanaweza wakachukua hatua za haraka.

Chini ya utaratibu wa sasa, akitokea kichaa akakaa katika nafasi ya Urais, taifa letu litaangamia.

Mimi ni mwana CCM halisia, mzalendo kwa kujihukumu na kuhukumiwa.

Nawiwa kutoa tamko la gharama kwa sasa, kwamba, ili kukinusuru chama chetu kiweze kuongoza Taifa hili siku zijazo, ni sharti tukinyime kura.

Kuinyima kura CCM kwa sasa ni kujenga nchi na chama chenyewe. Chama imara katika wingi wa vyama tulio nao, sharti kiwe na wanachama wachache waaminifu kuliko utitiri wa mamluki tulio nao kwa sasa.

Najua msimamo huu haupendwi ndani ya chama chetu, na wakati unakaribia tutauweka hadharani ili hatima ya kila mmoja wetu ijulikane.

Katika TANU na CCM aliyoienzi Baba wa Taifa, chama kingeweza kutoa mwongozo na kuwajibisha watendaji.

Chama chetu kimekuwa chama cha viongozi na si cha wanachama.

Ukiona Rais mwenyewe anatilia shaka Ilani ya chama iliyomweka madarakani, ujue jahazi linaenda mrama.

Alianza Mkapa akasema Ilani haitekelezeki, tukakaa kimya. Amekuja Kikwete akasema Ilani alipewa Jangwani na hajui iliandaliwaje, waungwana tumekaa kimya.

Ni wajibu wa kila mwanachama kuona umuhimu wa kutilia shaka uongozi wa sasa wa chama chetu, na kama hawatatusikia, hatutahama chama bali tutawanyima kura tukiwa ndani ya chama chetu kilicholeta uhuru. Rais wetu ambaye ni Mwenyekiti wa chama afike mahali achague kati ya kutumikia marafiki au Taifa.

Mwisho niwashukuru sana wote walionitumia ujumbe kwa njia ya simu, barua pepe, na hata kupiga simu kutoa maoni yao kuhusu mada hizi.

Nimezingatia yote mliyonieleza na panapo majaliwa nitafikisha baadhi ya maoni yenu katika nafasi zake. Mimi si mwandishi wa habari, lakini napenda kusoma habari na vitabu.

Waliochukizwa na maoni yangu, nawashauri waandike tusome na kuudhika kama walivyoudhika. Mwisho wa siku, Tanzania ni yetu sote na walio madarakani twawangoja huku uraiani. Hakuna aliye na hati-miliki ya kutawala. Tukubali kukosolewa, na Serikali isiyopenda kukosolewa, haina haki ya kukusanya kodi zetu.



Mwandishi wa makala hii amejitambulisha kuwa ni msomaji mzuri wa Raia Mwema na mmoja kati ya viongozi wa Ukiristo nchini. Barua Pepe: msomajiraia@yahoo.co.uk, Simu: 0712881704
 
Excellent....! Huyu mwandishi wa hii makala anahitaji pongezi nyingi sana. Ameweza kuelezea chanzo cha matatizo mengi ya uongozi wa Kikwete!
 
Source: Raia Mwema

Ugumu wa kumshauri Rais Kikwete

Mwandishi Maalumu
Septemba 30, 2009

Muandishi kazungumzia mengi yenye maana kwa Taifa letu na ninampa hongera ya dhati kwa jitihada zake, though inaonesha pia muandishi is in his usual biblical mission trying to spread Christianity around!.

Ningelipenda kueleza pia kuwa huendi Ikulu na ukasema kuwa unataka kumshauri Rais. Such a statement is in itself a show of disrespect to that high post. Hata kama unajulikana vizuri huko Ikulu lakini huwezi kusema hivyo hata siku moja na ndio maana huyo rafiki yake aliulizwa vile vile in a disrespectful way, je, yeye mwenyewe keshajishauri?

Pia sioni kama kuna ubaya wowote kwa yule anaetaka kuenda Ikulu akawa-interviewed in-person na sio kwa simu. Jamani pale ni Ikulu ya nchi, security guys watajuaje kama wewe ndie huyo unaejisema kwenye simu kuwa ndie bila ya kukuona uso kwa macho?
 
Naam,

Mwandishi nadhani kuna kipengele aidha kakiruka kwa makusudi ama hajui au hata ameandika na wachapishaji wakaona wakiweke kapuni.

Katika kundi la Sita basi kasahau kitu. Basi mimi nitaliita kundi la saba.

Kundi la saba na la ajabu ni la waganga wa kienyeji na wapiga ramli. Rais wetu ni mwafrika halisi kwa hiyo hajakumbatia kikweli kweli dini yoyote ya kigeni. Kwa hali hiyo, si vibaya nikisema, kwa uafrika wake ni mfuasi wa siri wa dini za jadi. Hili si tusi, dhambi wala dharau. Nimemshuhudia mwenyewe kwa mazungumzo ya ana kwa ana akihangaika na kulalamika juu ya mnyukano wa dini mbili kubwa hapa nchini (Uislamu na Ukiristo) na kweli haumpi raha hata kidogo.

Anajua jinsi dini hizi mbili zinavyotuhumiana juu ya maamuzi ya rais na serikali yanayozigusa dini hizi mbili. Wakiristo wanadai kwa wazi na sirini kuwa rais anawapendelea waislam wakati waislam nao wakidai wakiristo wanapendekelewa sana na serikali ya rais wetu. Matokeo yake ni rais kukosa msimamo na kubaki kulalamika na kutilia shaka kila ushauri anaopewa na watu watokao pande hizi mbili.

Kuna "uvumi" wa muda mrefu sasa kuwa rais wetu anapata faraja pale anaposhauriwa na waganga wa kienyeji kwa sababu anaamini hawana mgongano wa maslahi katika dini hizi mbili kuu! Kimantiki na kimsingi hii ni njia nzuri ya kutatua mnyukano wa dini kubwa pale unaposhauriwa na mtu wa tatu au wa katikati.

"Uvumi" huu umeendelea kueleza kuwa katika harakati za kuwasikiliza hawa waganga, rais amejikuta njia panda katika maamuzi mbalimbali. Ushauri wa waganga humfikia rais ama moja kwa moja au kupitia wapambe maalum, lakini utekelezaji wa ushauri huo huonekana kwa njia mbalimbali kama vile tabia sugu ya rais kuchelewa katika matukio mbalimbali na tabia ya rais kutoroka na kwenda sehemu huria kama michezoni. Mara kadhaa ndani na nje ya nchi, rais amekutwa katika maeneo yasiyo rasmi bila maandalizi wala kuwamo katika ratiba. Najua rais ana maisha binafsi lakini ni ruksa kuyahoji hasa yanapoonekana kuwa rasmi kwa kuwa yanatokea mara kwa mara.

Inasemekana kuwa kwa ushauri wa waganga rais pia amejikuta katika misiba, mazishi, kutembelea wagonjwa nyumbani na hospitali, sherehe za harusi, na hafla za asasi za kiraia zenye utata. Imesikika pia waganga hawa ndiyo wanaosikilizwa hata katika masuala ya afya yake kuliko hata madaktari wa ndani na nje ya nchi.

Eneo hili limejaa "uvumi", umbeya na maneno ya mitaani yanayochangamsha mabaraza na vijiwe, lakini cha msingi na kinachogomba ni pale yanayosemwa yanapofanana na yanayosemwa. Ikiwa uvumi huu au sehemu yake ina ukweli, basi kundi hili ndilo pekee linalomshauri mheshimiwa rais katika mambo mengi na kwa hiyo ndilo limeshikiliwa mustakabali wa taifa letu kwa sasa.

Katika mazingira ambamo makundi mengine yamenyamazishwa, salama yetu iko wapi tunapokuwa mikononi mwa hawa washauri ambao ushauri wao haujapimwa na chombo chochote kinachojulikana?


Pimbi
Guys,

You thought I was wrong?
 
jamani ni kwa nini mnasema kana akili kuliko watanzania wote la hasha napinga tena napinga sana ,

Kuna baadhi hawajapata nafasi tu ya kuonyesha ukomavu wao wa mawazo

nimekubali mia kwa mia.

hao wanaosema makamba ana akili kuliko watanzania wote wajue kuwa labda na akili kuliko wao peke yao na si wote! au waangalie kamusi maana ya neno "wote"
 
Guys,

You thought I was wrong?

Dr. Pimbi, hayo yote uliyoandika juu ya imani za kishirikina za kiongozi wetu ni kweli kwani ushahidi wa dhahili upo. Juzi juzi tu muungwana alipotembelea jimbo la same lililopata dhahama ya lamdslide ambako alikuwa huko kuwapa pole waliopatwa na misiba, jeshi la polisi kwa kuhofia afya ya kiongozi wao hawakuona busara kwa yeye kusafiri kwa muda wa saa sita kwa gari toka huko Same hadi Arusha hivyo waliaandaa helicopter ya kuja kumchukua kumrudisha Arusha; kwa mshangao wa watu wengi hizo chopper zilipofika huko Upare kumchukua akakataa kupanda na akarudi kwa gari!! Inasemekana Sangoma walimshauri asipande helicopter wakati wa ziara yake!! Tukiendelea namna hii nchi yetu itaangamia.
 
Back
Top Bottom