Hivi ni nini kimedhoofisha boxing hapa nyumbani?

Gumilapua

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2011
Posts
855
Reaction score
591
Mimi ni mmoja wa wapenzi wa boxing, nashangaa na kusikitishwa na jinsi mchezo wa boxing ulivyoshuka hapa nchini kiasi cha mashabiki wa mchezo huo kuanza kupungua.
Miaka ya 80-90 mchezo wa ngumi nchini ulikuwa uko juu sana, nakumbuka hata michezo ya hata ya ngumi za ridhaa ilikuwa ikijaza watu katika kumbi kama Diamond jubilee, DDC kariakoo, imasco center nk. Na kulikuwa na mabondia wengi wazuri ambao walikuwa maarufu achilia mbali wa ukoo wa matumla. Kulikuwa na majina makubwa kama David Mwaba, Anthony Mwang'onda, Benjamin Mwangata, kina Isangura, Koba kimanga, JumaBugingo, issack Mabushi, Neva Mkadalla, Nassor Michael, Rajab Hussein, Rashid janja, Mambeya Bakari, mzonge hassan, na wengine wengi!!!
Kwenye ngumi za kulipwa nduo usiseme, mapambano yake yalikuwa ni gumzo jijini wiki nzima kabla. Majina kama Stanley Mabesi, John Hugo, Lucas Msomba, Bruno Mwemezi, Charles Mhilu spinks, Emmanuel Mlundwa, Habib kinyogoli, Abdallah Mgeni, Emmanuel Kimaro " sugar ray", Mzaire Somwe Patauli, na wazambia Charles Libondo na David 'teacher' Chibuye. Majina yao yalikuwa ni household names. Sasa najiuliza kimetokea nini?
Boxing imekwenda wapi? Leo utasikia majina machache Dulla mbabe, mfaume mfaume, kiduku, kina Cheka lakini ukienda kuangalia wanachofanya ulingoni ni madudu! Niliowataja enzi zile walifananishwa na mabondia tuliowata novice kama kina Bakari Mwalyego, George sabuni, Tyson sichana n.k ambao hawakuweza kupata namba national boxing team.
Leo walau Mwakinyo anajaribu jaribu ingawa enzi zile hata national team angekuwa anaisikia kwenye bomba.
What has gone wrong in boxing?
Maana zamani zile hata mapambano ya nje tulikuwa tunafuatilia Leo, ni wachache wanamjua bingwa wa dunia uzito wa juu. Majina kama Anthony Joshua, Tyson Fury, Andy Ruiz Jr, Deontay Wilder ni wachache wanaowajua labda Mayweather Nate ni kwa sababu ya shobo zake na sio boxing. Kipindi kile tulikuwa tunafuatilia kwa karibu mapambano ya ubingwa wa dunia. Nakumbuka tuliamka alfajiri ili tuone Tyson fights, majina kama Marvin Hagler, tommy hearns, sugar ray, evander, mzee foreman, azuma nelson, nk yalikuwa ya kawaida.
Leo wachache wanaowajua Daniel Dubois, Lomanchenko, gervonta davis, Terrence Crawford, Dilian whyte, nk.
Kilichotokea sikijui ila nashangaa ghafla bin vuu boxing imesepa....
Inasikitisha sana na inaniuma sana.
 
tatizo mabondia viwango vyao vibovu, Mwakinyo alipata nafasi nzuri ya kurudisha mashabiki , lakin alichokifanya ulingoni, alitukatisha tamaa,
 
Dah.....Kumbukumbu adimu umeleta..! Maisha yanasonga kwa kasi. Somwe Patauli ' Okapi ' sasa ni mchungaji huko Kigamboni, Enzi zake walisumbuana sana na Stanley Mabesi 'Ninja'
 
Tatizo la mabondia wa kibongo usela mwingi na kutokujitambua .

Mabondia wa kibongo kuuza mechi kwao ni jambo la kawaida sana .

Kingine kukosa kazi nyingine ya maana ya kuwaingizia kipato ,wengi wanategemea boxing tu iwaingizie pesa.

Mbali na hayo, mabondia wengi hawana wasimamizi wa kuwasimamia kazi zao.
 
Enzi izo heavyweights ni kweli 'heavyweights' unakuta mijitu kama Foreman,Evander,Tyson,Linnox na kadhalika, Ndonga ndonga kweli....! Sasa siku izi vijitu kama ' Manipakiyao' na 'Meiweza' navyo ni heavyweights vya dunia
 
Hao uliowataja sio heavyweight ni kina Anton Joshua na Wilder ndio mabondia wa uzani wa juu
 
Enzi izo heavyweights ni kweli 'heavyweights' unakuta mijitu kama Foreman,Evander,Tyson,Linnox na kadhalika, Ndonga ndonga kweli....! Sasa siku izi vijitu kama ' Manipakiyao' na 'Meiweza' navyo ni heavyweights vya dunia
Hahaha dah kwahiyo Mayweather na PacMan ni heavyweight? Hahaha we jamaa bwana.

Anyway, boxing ilizikwa na chama chake chenyewe, pia boxing unachukuliwa ni mchezo wa kihuni. Wacheza boxing wengi ni Keko, Tandale, Manzese, Mabibo, Mwananyamala na wengi wanahusishwa na wizi.

Hata marehemu Mashali kifo chake kimetokea mikononi mwa wananchi kwa kesi ya udhulumaji au wizi.

Media zikaupa mgongo huu mchezo zikaukumbatia mpira, muziki na maigizo.

Boxers pia hawajitambui. Dula alipata udhamini mzuri tu, akapangiwa nyumba Bagamoyo na gari za kutembelea ila unaambiwa, nyani utamtoa msituni ila hautautoa msitu kichwani mwake, huyu angekua serious angetisha.

Now hii tasnia haina wadhamini, pia serikali bado haijafanya iwe ni salama kujiajiri katika mchezo wowote.

Leo ndiyo tupo hapa mtu anakwambia Mayweather na Pacquiao ni heavyweights.
 
Marvin Hagler alikasirika media haimtambulishi kwa nickname aipendayo ya 'Marvelous' akaenda mahakamani akaliadopt hili jina so watu wakawa wanatakiwa kumuita Marvin Marvelous Hagler kilazima.

Sweet science
 
Ni kweli vyama vya ngumi pia vimechangia sana kudorola kwa mchezo huu hasa hapa Tanzania. Viongozi wao ni mizozo ya kugombea madaraka tu.badala ya kubuni mbinu za kuurudisha mchezo kwenye ramani. Mchezo umekosa hamasa kiasi watu hawajui nini kinaendelea.
Wanahabari pia wanaonekana kuupa kisogo huu mchezo.
I wish ningepata maono ya nini cha kufanya kuufufua mchezo huu.
 
Marvin Hagler alikasirika media haimtambulishi kwa nickname aipendayo ya 'Marvelous' akaenda mahakamani akaliadopt hili jina so watu wakawa wanatakiwa kumuita Marvin Marvelous Hagler kilazima.

Sweet science
Hahaaa!!
Jamaa ilikuwa ni machine ile. Nakumbuka alivyomsambaratisha Thomas Hearns.
 
Hearns ile siku nahisi ilikua ni siku yake tu hat watangazaji wakawa wanasema kua leo Hearns anaonekana ana weak chin, nafikiri round ya 3 au 4 alipigwa bomba akajaribu kubob and weave wee miguu ikamkatalia akawa kama ana miguu ya big g
 
Sio bongo tu, tuseme duniani kabisa, boxing inaenda kwa nguvu za media.

Tatizo mabondia, mabondia wengi wa siku hizi viwango kawaida, tunakosa ile burudani haswa.
Leo duniani bondia mwenye kulipwa zaidi ama mwenye mpunga mrefu sio wa uzito wa juu, nahisi hii ni mara ya kwanza tangu boxing ianze.
 
Dah.....Kumbukumbu adimu umeleta..! Maisha yanasonga kwa kasi. Somwe Patauli ' Okapi ' sasa ni mchungaji huko Kigamboni, Enzi zake walisumbuana sana na Stanley Mabesi 'Ninja'
Kumbe! Sikujua kama yule mzaire 'okapi' aliamua kuzamia mojakwa moja bongo.
Mbabe wao kina Mabesi alikuwa mzambia Charles Libondo, na kuna siku ilikuwa acheze na mmoja wao kati ya akina Mabesi au Emmanuel kimaro, si wakashindwa kuafikiana dau, ikabidi promoter atafute replacement. Wakampata dogo mmoja Anthony Ndaki. Dogo alikula za mbavu balaa knock out akatolewa ulingoni kwa machela kupelekwa Muhimbili usiku huo huo dogo akafa. Toka siku hiyo watu walimuogopa yule Mzambia balaa
Ilikuwa ni mmoja ya vifo kwenye boxing nilichoshuhudia pale DDC kariakoo!
Ila baadae kina Mabesi wakamzoea na kuanza kumtwangwa!
 
Acha kbs...!! Okapi alipata mke mTz ,watoto ,familia . Ashakuwa mTz mwenzetu..Ila hawa mabondia wazamani wanaiona hali ya ndondi kwa sasa bila shaka wanapata simanzi sana....! Sio hapa hata huko nje mambo ni hovyo sana...sijawai ona pambano bovu la kutafuta bingwa wa heavyweight kama lile kati ya Deontay Wilder na Fury Tyson.
 
Ni kweli kabisa hata Mimi nilikuwa nashangaa hata kabla ya wilder vs fury I, inakuwaje bondia kama Deontay Wilder ambae kimsingi ni novice mwenye nguvu anakuwa undefeated. Na hata fury alipo draw na Wilder pambano halikuwa na msisimko wala tactics za maana. Huwezi hata kulinganisha mpambano kama wa Riddick Bowe vs Evander Holyfield.
Hata tukija kwa Huyu Anthony Joshua nae hamna kitu. Joshua huyu naamini kabisa angekutana hata na Andrew Golota angekaa.
Lakini yote kwa yote hapa kwetu ngumi zimekufa, vipaji hakuna walau kwa wenzetu ushabiki bado upo, na walau weight za chini kuanzia middle weight kushuka chini kuna mabondia wazuri kama kina GGG, Gervante Davis, Canello Alvarez, Terrence Crawford, Amir Khan, ,Lomachenko, Chris Eubank Jr, Kelly Brook etc bado wana vipaji.
 
Wakienda nje wanauza mpambano kwa € 5000
 
Back
Top Bottom