Gumilapua
JF-Expert Member
- Sep 13, 2011
- 855
- 591
Mimi ni mmoja wa wapenzi wa boxing, nashangaa na kusikitishwa na jinsi mchezo wa boxing ulivyoshuka hapa nchini kiasi cha mashabiki wa mchezo huo kuanza kupungua.
Miaka ya 80-90 mchezo wa ngumi nchini ulikuwa uko juu sana, nakumbuka hata michezo ya hata ya ngumi za ridhaa ilikuwa ikijaza watu katika kumbi kama Diamond jubilee, DDC kariakoo, imasco center nk. Na kulikuwa na mabondia wengi wazuri ambao walikuwa maarufu achilia mbali wa ukoo wa matumla. Kulikuwa na majina makubwa kama David Mwaba, Anthony Mwang'onda, Benjamin Mwangata, kina Isangura, Koba kimanga, JumaBugingo, issack Mabushi, Neva Mkadalla, Nassor Michael, Rajab Hussein, Rashid janja, Mambeya Bakari, mzonge hassan, na wengine wengi!!!
Kwenye ngumi za kulipwa nduo usiseme, mapambano yake yalikuwa ni gumzo jijini wiki nzima kabla. Majina kama Stanley Mabesi, John Hugo, Lucas Msomba, Bruno Mwemezi, Charles Mhilu spinks, Emmanuel Mlundwa, Habib kinyogoli, Abdallah Mgeni, Emmanuel Kimaro " sugar ray", Mzaire Somwe Patauli, na wazambia Charles Libondo na David 'teacher' Chibuye. Majina yao yalikuwa ni household names. Sasa najiuliza kimetokea nini?
Boxing imekwenda wapi? Leo utasikia majina machache Dulla mbabe, mfaume mfaume, kiduku, kina Cheka lakini ukienda kuangalia wanachofanya ulingoni ni madudu! Niliowataja enzi zile walifananishwa na mabondia tuliowata novice kama kina Bakari Mwalyego, George sabuni, Tyson sichana n.k ambao hawakuweza kupata namba national boxing team.
Leo walau Mwakinyo anajaribu jaribu ingawa enzi zile hata national team angekuwa anaisikia kwenye bomba.
What has gone wrong in boxing?
Maana zamani zile hata mapambano ya nje tulikuwa tunafuatilia Leo, ni wachache wanamjua bingwa wa dunia uzito wa juu. Majina kama Anthony Joshua, Tyson Fury, Andy Ruiz Jr, Deontay Wilder ni wachache wanaowajua labda Mayweather Nate ni kwa sababu ya shobo zake na sio boxing. Kipindi kile tulikuwa tunafuatilia kwa karibu mapambano ya ubingwa wa dunia. Nakumbuka tuliamka alfajiri ili tuone Tyson fights, majina kama Marvin Hagler, tommy hearns, sugar ray, evander, mzee foreman, azuma nelson, nk yalikuwa ya kawaida.
Leo wachache wanaowajua Daniel Dubois, Lomanchenko, gervonta davis, Terrence Crawford, Dilian whyte, nk.
Kilichotokea sikijui ila nashangaa ghafla bin vuu boxing imesepa....
Inasikitisha sana na inaniuma sana.