The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
1. Ni kwanini kama nchi tunaingia gharama mara mbili kufanya zoezi Moja linalofanana? Hii tunayoambiwa kuwa ni Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa (INEC) waliandikisha/fanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura nchi nzima wiki chache zilizopita.
2. Cha ajabu TAMISEMI ya Mchengerwa na Samia Suluhu Hassan nayo imeanza kufanya zoezi hilohilo la eti kuandikisha wapiga kura walewale tena ktk, vituo vilevile vilivyotumiwa na INEC na ktk maeneo yaleyale na watu walewale...!
3. Kwanini tusumbiliwe kuandikishwa kwa mara ya pili tena...?
4. Vitambulisho vya mpiga kura vya Tume ya uchaguzi ya Taifa vina kasoro gani kutumika kuchagua viongozi wa vijiji, mitaa na vitongoji..?
5. KASORO KUBWA KTK UANDIKISHAJI WA TAMISEMI:
#Kwanza uandikishaji unafanyika kienyeji sana na ni rahisi sana daftari kuwa forged kwa kuingizwa kwa majina bandia na siku ya kupiga kura yakapiga kura pia...
#Kinachofanyika kwenye vituo vya uandikishaji wapiga kura wa TAMISEMI ya Mchengerwa (Mkwe wa Samia Suluhu Hassan) kila mtu akifika kwa mwandikishaji
✓ Kutaja majina yake matatu
✓ Umri wake
✓ Sahihi yake, basi
#Hakuna cha picha wala nini japo maeneo mengine nasikia waandikishaji wanaomba ID za NIDA...
KWA MAONI YANGU:
Hii haikustahili kufanyika hivi. Hakuna shida wala ubaya kutumia daftari la kudumu la wapiga kura la INEC na watu tukapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa...
Hii ingeokoa gharama ya mabilioni ya pesa yanayotumika sasa na pesa zingeweza kutumika kwa shughuli zingine za MAENDELEO...