Hivi ni Sahihi Kumpa Mpenzio Shikamoo?

Hivi ni Sahihi Kumpa Mpenzio Shikamoo?

Status
Not open for further replies.

Regia Mtema

R I P
Joined
Nov 21, 2009
Posts
2,970
Reaction score
866
Wakuu habari zenu!
Hili jambo limekuwa likinitatiza sana tena sana...Utakuta binti au mwanamke aliyeolewa anamwamkia mume wake eti kwakuwa mwaume ni mkubwa kiumri kuliko mkewe,mimi hii sielewi kabisa..What I know mke na mume ni mtu na rafiki yake tena ndio best friends na kwaninavyofahamu maana shikamoo naona haistahili kufanyika kwa wapendanao..mimi kwangu naona haina maana kabisa kumpa shikamoo mumeo hata kama amekuzidi miaka 40! Lakini kila kukicha nasikia watu wakiwaamkia waume zao..Jamani hivi hii imekaaje?je ni sawa?
 
kwa mimi kwa kweli hainiingii akilini....hata anizidi miaka 90 simpi shikamoo
 
shikamoo muhimu hasa kama amempata kwa hela!! huyo hawezi kupata jeuri ya kulonga vingine

kwani ni nsiri kuwa majority hukimbilia wenye michuzi!!!!!!!!!!
 
shikamoo muhimu hasa kama amempata kwa hela!! huyo hawezi kupata jeuri ya kulonga vingine

kwani ni nsiri kuwa majority hukimbilia wenye michuzi!!!!!!!!!!

Ina uhusiano gani na shikamoo,kivipi?hebu tufafanulie.
 
mhhh mi nina kabinti kule vikindu kananimwagia shikamoo kila dakika.Shkamoo inahusika sana
 
Kwani maana ya shikamoo ni nini?.achilia mbali mke na mume,mimi hata kwa mtoto kumwamkia mkubwa shikamoo pia siielewi,sasa jamani kama kuna mtu anajuwa maana ya shikamoo tafadhari aiweke wazi hapa
 
Shikamoo kwa wapenzi, yaani mume na mke hainiingii akilini. Shikamoo kwa yule anayeitoa itakuwa ishara ya kumwogopa yule anayepewa hiyo shikamoo na hivyo kufanya asiwe huru sana. Nadhani kwa wapenzi si vizuri kuitumia.
 
Kwani maana ya shikamoo ni nini?.achilia mbali mke na mume,mimi hata kwa mtoto kumwamkia mkubwa shikamoo pia siielewi,sasa jamani kama kuna mtu anajuwa maana ya shikamoo tafadhari aiweke wazi hapa

shikamoo ilitumika enzi za utumwa za mwarabu.....maana yake ni" niko chini ya miguu yako"
 
shikamoo ni mojawapo ya eshima

Nope Sis! Hivi wajua maana ya shikamoo?

Mie hata katika mazingira ya kawaida inanitoka mara chache sana;

Ni slamu ya kitumwa; maana yake NIKO CHINI YA MIGUU YAKO
Enzi hizo watumwa akisalimia "Shikamoo Bwana!"😡
 
In a serious tone....mpenzi kumwambia mwenza wake shikamoo ni uenda wazimu!
Yani inakuwaje vile!!! unakuwa safari unarudi anakwambia shikamoo au unaamka asubuhi sana, unapata kie cakula then ukitoka kitandani anakwambia shikamoo au???
 
Shikamoo ni salamu ya watumwa waliotakiwa kuwaamkia mabwana zao. Essentially inamaanisha "niko chini ya miguu yako"

In my opinion, haifai kutolewa na mtu yeyote kwa mtu mwingine yeyote, sembuse mtu kwa mumewe, kwa sababu ina degrade utu wa mtu.

Ndiyo maana wenzetu wana salamu zilizojikita katika kutakiana mema zaidi ya kuonyeshana nani mkubwa.Good Morning, good afternoon, how do you do. Hata salamu zao zinaonyesha wamepita hii medieval stage ya serfdom.
 
Yakhe, shikamoo ni hishma kwa mume bila kijali umri haswa kwetu wa mwambao. Mkeo asipokuamkua basi ujue huyoo keshaanza ustaarabu wa bara au wa kimagharibi kusikokuwa na salamu ya mkubwa wala mdogo. Shkamoo ni shurti itolewe na mke.
 
kusema ukweli ukweli sijawahi kumuamkia mme wangu shikamoo,tukiamka asubuhi namuuliza umeamkaje ......
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom