Hivi ni sahihi watoto kutoa sadaka kanisani?

Hivi ni sahihi watoto kutoa sadaka kanisani?

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2021
Posts
4,134
Reaction score
10,644
Habari za leo ndugu zangu katika imani?

leo naomba kujua uhalali wa watoto kutoa sadaka unakujaje.

mtoto ana chanzo gani cha kipato mpaka atoe sadaka?

Maana halisi ya sadaka ni nini hasa?
Screenshot_20220508-110931.png

Mada yangu ni hio wazee
 
ni sahihi mzee watoto kutoa maana imeandikwa wafundishane watoto njia ilionjema na hawatoiacha hata wakiwa wazee.
akitoa sadaka akiwa bado mdogo unawekeza ht akiwa mkubwa ataona ni kawaida maana alianza akiwa mdg.
hivyo mfundishe kwenda msikitini /kanisani akiwa bado mdg utaona faida yake ht akiwa anakua hatoacha.
 
Tatizo ni user name unayotumia. Wafundishe wanao kutoa sadaka.
 
mtoto anatakiwa kulazimishwa kufanya mema kabla hajajua jema na baya
 
Ni muhimu watoto wafundishwe toka wakiwa wadogo ili wakue na kufuata misingi waliojengewa; otherwise hawataona umuhimu wa kutoa sadaka ukubwani. Mbali na kutoa sadaka kanisani wafundishwe kusaidia wenye uhitaji , kutembelea wagonjwa inapobidi na hata kusaidia wengine. Kiimani haya mambo mtoto akijengewa msingi mzuri tangu mwanzo anakuja kuwa mtu mwema baadae.
 
Ni sahihi! Kwa sababu mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo!
 
"Train up a child in a way he should go, when he is old he will not depart from it."
Kuna tishet nilkuwa navaa, iliandikwa maneno hayo na nukuu kutoka bibliani.
Sikumbuki kitabu.
 
Ni muhimu watoto wafundishwe toka wakiwa wadogo ili wakue na kufuata misingi waliojengewa; otherwise hawataona umuhimu wa kutoa sadaka ukubwani. Mbali na kutoa sadaka kanisani wafundishwe kusaidia wenye uhitaji , kutembelea wagonjwa inapobidi na hata kusaidia wengine. Kiimani haya mambo mtoto akijengewa msingi mzuri tangu mwanzo anakuja kuwa mtu mwema baadae.
I second you
 
M
Habari za leo ndugu zangu katika imani?

leo naomba kujua uhalali wa watoto kutoa sadaka unakujaje.

mtoto ana chanzo gani cha kipato mpaka atoe sadaka?

Maana halisi ya sadaka ni nini hasa?
View attachment 2216466

Mada yangu ni hio wazee
Umesema mtoto. Mtoto anajifunza kupitia kwako,ukiwa baba au mama yake,atafanya unachofanya wewe.

Uko mstari kwenye biblia unasema. Umfundishe mwanao njia imfaayo,naye hataiacha hata akiwa mzee. Sikumbuki ni wapi.
Bila ukiwa ni mzazi utamfundisha kitu/vitu unavyoamini vitamfaa,kwa hiyo ni wewe tu unajua nini kuhusu kutoa sadaka.
 
Mtoto kama Diamond Asitoe sadaka! Halafu hivi kuna sehemu marufuku kutoa hela
 
Mithali 22:6
Shukrani sana, imenibidi nifungue nisome.
Wakati nipo darasa la nne huko nilinunuaga tisheti mnadani Ludewa huko yenye hayo maandishi na nilikuwa sijui maana yake.

Kuna siku nilifanyaga kosa, nikahukumiwa na mzazi kutokana na maneno niliyoyavaa mwenyewe kwenye tisheti kwa kuyatafsiri.
Nikawa nimeyakariri kwa english hivyo hivyo.
 
Mimi kama mwalimu wa sunday school ya watoto umewekwa utaratibu wa kutoa sadaka kwa watoto na wao wenyewe wanazitunza, kama mwalimu wao kila jumapili wananipa data tu kwa ajili ya kurekodi na kutoa ripoti ya fedha idara ya watoto pindi ikihitajika kwa uongozi wa juu. Mapato na matumizi ni kwa manufaa yao watoto pekee kama wiki ya watoto kwa mwaka mara mbili. Sadaka wanakula watoto wao wenyewe
 
Back
Top Bottom