Hivi ni sawa marais wote kutokea upande mmoja?

Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inayotawaliwa na marais wawili kwa wakati mmoja, mabunge mawili, nyimbo za taifa mbili, majaji wakuu wawili, katiba mbili, bendera mbili, maspika wawili, makamu wa rais sasa hivi watatu, marais wanaopigiwa mixinga 21 wawili nk

Zamani ilikuwa Rais akitokea Zanzibar, makamu anatokea Tanganyika. Rais akitokea Tanganyika, makamu anatoka Zanzibar. Wakati wa Mwinyi kulikuwa na makamu wa kwanza wa Rais ambaye alikuwa ni jaji Warioba kwakuwa marais wote walikuwa ni wazanzibari na rais wa Zanzibar akawa makamu wa pili wa rais.

Kwa mfumo wa muungano huu haitatokea kamwe kuwa na marais wote kutokea Tanganyika kwakuwa Tanganyika ilikufa hivyo haiwezekani kamwe kwa mtanganyika kuwa rais wa Zanzibar.

Sasa hivi nchi inatawaliwa na wazanzibari watupu. Je wakiungana kupanga lolote kuhusu Tanganyika tutapona? Je hamuoni wanagawa vyeo visivyo vya muungano kwa wazanzibari wakati watanganyika zaidi ya milioni 60 wanaangalia tu? Huku kuna wazanzibari wanashika uDC na uwaziri wakati hazipo chini ya muungano lakini hakuna mtanganyika anaweza kupewa hata usheha huko Zanzibar.

Katiba iandikwe upya kuondoa kasoro kama hizi sema kikwazo kikubwa ni watanganyika wenyewe hawaitaki nchi yao eti jitu zima utalisikia linasema katiba haileti maji, barabara, umeme ... wakati wenzetu wazanzibar hawazidi milioni 2 lakini huwezi kuwaambia lolote kuhusu nchi yao.
mbona nimeshikwa na simanzi baada ya kusoma huu uzi
 
Kinachoendelea hivi Sasa ndio kipimo changu. Kuna mtu aliwahi sema Kikwete nafasi ambayo ingemstahili ni kuwa waziri wa michezo na utamaduni. Unakumbuka huyo!?
mimi nataka twende specifically,kipimo chako ni kipi?
 
Warioba anauma na kufumba macho. Kama amekubali juu ya majimbo (states) marekani kuwa na bendera zake kwanini asimalizie kuwa kuna sheria tofauti kati ya jimbo mpaka jimbo. Kuna sheria ambayo jambo ukilifanya jimbo moja si kosa lakini jimbo jingine ni kosa. Kama yeye anaumizwa na sheria ayaeleze na hayo pia.
 
Tanzania ndiyo nchi pekee duniani inayotawaliwa na marais wawili kwa wakati mmoja, mabunge mawili, nyimbo za taifa mbili, majaji wakuu wawili, katiba mbili, bendera mbili, maspika wawili, makamu wa rais sasa hivi watatu, marais wanaopigiwa mixinga 21 wawili nk

Zamani ilikuwa Rais akitokea Zanzibar, makamu anatokea Tanganyika. Rais akitokea Tanganyika, makamu anatoka Zanzibar. Wakati wa Mwinyi kulikuwa na makamu wa kwanza wa Rais ambaye alikuwa ni jaji Warioba kwakuwa marais wote walikuwa ni wazanzibari na rais wa Zanzibar akawa makamu wa pili wa rais.

Kwa mfumo wa muungano huu haitatokea kamwe kuwa na marais wote kutokea Tanganyika kwakuwa Tanganyika ilikufa hivyo haiwezekani kamwe kwa mtanganyika kuwa rais wa Zanzibar.

Sasa hivi nchi inatawaliwa na wazanzibari watupu. Je wakiungana kupanga lolote kuhusu Tanganyika tutapona? Je hamuoni wanagawa vyeo visivyo vya muungano kwa wazanzibari wakati watanganyika zaidi ya milioni 60 wanaangalia tu? Huku kuna wazanzibari wanashika uDC na uwaziri wakati hazipo chini ya muungano lakini hakuna mtanganyika anaweza kupewa hata usheha huko Zanzibar.

Katiba iandikwe upya kuondoa kasoro kama hizi sema kikwazo kikubwa ni watanganyika wenyewe hawaitaki nchi yao eti jitu zima utalisikia linasema katiba haileti maji, barabara, umeme ... wakati wenzetu wazanzibar hawazidi milioni 2 lakini huwezi kuwaambia lolote kuhusu nchi yao.
Hujui chochote kati ya uliyoandika. Lakini usijali. Wajuvi wa mambo wapo watakusaidia.
 
Tafuta maisha yako mzee ili ujipate kwaajili ya familia yako hao walitafuta hizo nafasi kwaajili ya familia zao,fanyakazi zako hii nchi haina mwenyewe ati!!
 
Back
Top Bottom