Hivi ni ukoo wetu tu tuko hivi au na wengine mna experience upuuzi kama huu?

Hivi ni ukoo wetu tu tuko hivi au na wengine mna experience upuuzi kama huu?

Mkuu,usiogope fanya vile fikra zako zinavyokutuma lkn usivinje sheria!
 
Mkuu familia zetu ndivyo zilivyo...
Unawajali lkn usiwadikilize sana masna utakuja kuwatenga..
 
njoo unyamwezini uone ungekuwa ushakufa kitambo
Sio vijiji vyote nakataa, kwa Mara ya kwanza nimekwenda Mimi na ndugu zangu msibani ndugu karibu wote walikuwa hawatujui kabisa baada ya mazishi kabla wanakijiji hawajatawanyika kilifanyika kikao cha sisi kutambulishwa pale kijijini na baada ya hapo tuliagana nao na tuliondoka vizuri tu hakuna lolote lililotupata sio njiani wala makwetu nimefupisha. Hivyo mkuu usiseme unyamwezini sema Kijiji X... , ningekubaliana na wewe kama ungesema Kg kule kwa akina Mzito Kabwela
 
Tabora wanaweza kumsaidia mgeni ila sio mwenyeji huwezi kukuta kiongozi wakuchaguliwa mwenyeji wote ni wageni akijaribu mwenyeji hawampi hata kama anaelimu kiasi gani ndo maana maendeleo kwa Tabora sio Leo uswahili umekithiri
 
Daah pole sana mkuu itakuwa ni kwa upande wenu but kwetuu nijuavyo ni ngumuu sn
 
Miaka kadhaa iliyopita ndugu yetu katika ukoo alipata ajali mbaya ya barabarani na ilihitajika matibabu ya dharura lakini yenye umakini, na kama mnavyojua matibabu ya umakini kwa nchi hii ni yakulipia. Ndugu tulikusanyana ili kila mtu aweze kutoa mchango wake kufanikisha matibabu hayo.

Michango ilikua ya kusuasua sana, na kwakweli kasi ya utolewaji wake ilikua hailingani na mahitaji ya udharura ya mgonjwa, kwani baada ya muda mrefu wa kikao na kuhamasishana bado hela zilizopatikana zilikua kidogo na zisingeweza kufanya mgonjwa apelekwe theater.

Nilipoona mambo yako hivyo na hisia za maumivu anazopata mgonjwa nikaanza kujitolea kutangaza kuchangia kiasi kikubwa, baada ya sekunde chache nikaungwa mkono na ndugu wengine watatu waliochangia kiasi kikubwa na baada ya muda mfupi pesa ya matibabu ikapatika.

Siku ileile nikapata wito kutoka kwa mama yangu mzazi kua kesho yake niende kwake ananiita, na mimi nikaamua kwenda siku ileile bila kusubiri kesho. Nilipofika alinionya sana kwa kitendo nilichofanya cha 'kutangaza' kutoa pesa vile mbele ya kikao japo kilikua cha wanandugu. Akanambia watu sio wazuri mwanangu japo ni ukoo wenu, na maneno meengi ambayo niliona kama maneno ya kizee tu. Risala ilikua ndefu na yenye kunisisitiza lakini mimi nilimsikiliza Bi mkubwa kama ada tu huku yakiingia sikio moja na kutokea jingine

Wiki moja baadae nilishangaa baada ya kukutana hospitali(mgonjwa alikua kashafanyiwa oparation) na mmoja kati ya wale ndugu waliotoa mchango mkubwa, akaniambia baba yake hakufurahishwa na kitendo cha yeye kujitolea 'hadharani' kutoa mchango. Akamwambia bora angefanya siri au angelipa moja kwa moja hospitali kimyakimya. Japo sikumwambia kua na mimi nilikabiliwa na hali kama yake lakini wote tukakubaliana kua wazazi wanazeeka na visheria vyao ambavyo havisaidii jamii.

Miezi kama kumi na nane baadae nilipatwa na mshituko. Nilikua naongea na dada yangu binamu ambae alinimwagia maelezo meengi kuhusu tukio lile la kuchanga siku ile. Eti watu hawakulipokea vizuri japo walijifanya wameshangilia tulipokua tumetangaza michango yetu. Dada binamu akaanza kunitajia kwa majina ndugu ambao wanauwezo kuliko hata sisi tuliotoa michango mikubwa lakini kila mmoja alikua anasubiri atoe kiasi kilekile ambacho watu wote watapangiwa kutoa! Akanihadithia na maneno watu waliyokua wanayasema pembeni na baada ya kikao eti tunajifanya tunaazo na mengine mengi ya kebehi na kuvunja moyo sana!

Kipindi kirefu kilikua kimepita toka mchango ule na yale mazungumzo na dada binamu lakini kwakweli niliumia sana kwa maneno yale na nikiri yaliniathiri sana na yalinibadilisha kabisa mtazamo na approach yangu kwenye shughuli za kifamilia. Nilikua nahisi watu hawaoni mahitaji ya watu kwenye ukoo lakini unashangaa huyo unaedhani anauhitaji badala akufuata umpe ramani za michongo ya town yeye anakusema unapofanya kitu positive! Najiuliza hivi ni ukoo wetu tu ndio tuko hivyo au ndugu zangu nanyie mshawahi ku experince kitu kama hicho?
Nilichojifunza kwenye story yako na huenda ndo uhalisia ni kuwa: wazazi wako waliumia unamwaga pesa kwa "watu baki" ilihali wao nyumbani wanashindia dagaa... Yaani huwahudumii wakafurahia jasho LA kujinyima kwao usome au upate nafasi uliyopo.

Tujitoe kwa wazazi wetu jamani, tusiwaone wanazeeka vibaya!! Wanamahitaji mengi muhimu na hawawezi kuwa wanatuambia kila siku tuwatumie hela. Tunahitaji kuwa tunatuma tu bila kuombwa! Siku ikitokea jambo kama hilo la kujitolea kwenye jamii hawatanung'unika, maana watakuwa wameridhika na huduma tunazowapatia.
 
Bora kuishi Na watu baki Tu ndugu Ni masnitch Sana. Hapa nilipo nimezungukwa Na ndugu ugomvi hauishi. Nipo kwenye kampeni nikajenge mbali nimuhamishe na mama.
Mimi ilikuwa ni falsafa yangu, siwezi kuishi ama kufanya kazi nilipozaliwa!!! Kuna majungu na ujinga mwingi sana, huwezi kuendelea.
 
Mambo ya ukoo nlishakataa, I got family.
Ndugu wengine hata ciwajui na cijawahi kuwaona na sihitaji hata kuwaona,
Bora rafiki wa kweli atapenda ufanikiwe kuliko ndugu all tym hawataki maendeleo
 
Haya mambo yapo sana na hali hii inachagizwa pia na wazazi wetu.kwenye vikao vya kifamilia kama baba au mama ameshiriki huwa wakishajua kwamba mtoto wao ni mwenye moyo wa huruma wanajitahidi wakae nae karibu ili wampe ndogo ndogo kwamba asubiri wale wanafamilia wenye uwezo watamke kwanza ahadi zao ndo kisha yeye atamke.

So yule ambaye ni mambo safi sana akishasema na unfortunately akatamka kiasi kidogo itabidi utembee mule mule aliposema tena wanakushurutisha upunguze kiasi na obvious hawa wenye uwezo huwa wanatamka kiwango kidogo ili{kwa akili zao}ili kuepuka virungu vya wanafamilia kuwalilia shida hili likishapita.

Kwa siye tuliotoka vijijini,Kaskazini mwa nchi huwa tunakuwa na umoja wa ukoo ulio na katiba na sheria kamili wakati huo huo wazee pia vijijini huko wanakuwa na vikao vyao na katiba yao inayowaongoza.likija tatizo tunakaa vikao sisi kama vijana linawekwa mezani linajadiliwa kama ni lakutekelezwa kwa umoja{yaani papo kwa papo kwamba kila mwanaukoo atoe tuseme Tsh20,000/=}tunafanya hivyo laah halitekelezeki basi tutachangishana na kiasi kitachopungua kitatoka kwenye hazina ya ukoo inayotokana na michango yetu ya kila mwezi tuliyopangiana kutoa.

Matatizo huwa hayana hodi,matatizo sio harusi maana harusi hata ukiahidi miezi minne mbele hapana shaka yoyote shida ni pale utakapomshuhudia ndugu yako ktk kitanda cha mauti kwa kukosa japo 1mill kama familia ya kumfanyia kipimo fulani cha dharura ili doctor ajue amwandikie dawa ya aina gani,i swear to God hii picha itakusumbua maishani mwako maana unakuta huku unaogopa kutoa ili kuiridhisha jamii fulani huku ukitaka kutoa umuokoe nduguyo sasa muda wote huu unaoutumia kujitafakari Mungu nae anafanya yake.

Haya mambo huwa yanaandaliwa,cha kufanya wote kwenye koo zetu tuhamasishane tukutane kwa vikao japo mwezi mara moja kwa tunaokaa mji mmoja au hata miji mingine maana siku hizi huduma za SimuPesa zimerahisisha sana kufikisha amana kwenye mambo kama haya.tuwekeane kiwango kidogo tu cha ada kwa mwezi japo Tsh10,000= mkiwa 20 au hata kumi ndani ya mwaka mmoja mna bei gani?ikitokea tatizo la kutaka million 1 hakuna tena kutegeana yule aseme kwanza ndo mi niseme.

Yangu ni hayo wakuu......
 
Back
Top Bottom