Hivi ni wapi wanapoweza kushitaki endapo waajiri wao hawawatendei haki?

Hivi ni wapi wanapoweza kushitaki endapo waajiri wao hawawatendei haki?

xuxumeyu

Member
Joined
Mar 15, 2015
Posts
59
Reaction score
7
Hivi ni wapi mfanyakazi anaweza kwenda kushitaki ikiwa hatendewi haki na mwajiri wake au ikatokea wakashindwa kuelewana au mfanyakazi akaachishwa kazi na bila kipewa hakiyake inayo stahili wapi kesi hizi hupelekwa nifahamisheni jamani
 
......migogoro na malalamiko yote ya kiajira yanawasilishwa kwenye ofisi za Tume ya Usuluhishi na Uamuzi(CMA) au Ofisi za Idara ya Kazi zilizoko kwenye eneo husika kuhusiana na malalimiko yalipo au mgogoro ulipotokea.
 
Ila kwa mfanyakaz ambaye ni mwanachama wa chama cha wafanyakazi kimbilio lake ni kwenye chama, huko atapata msaada wa uwakilishi mahakamani au cma, mf wa vyama vya wafanyakazi ni tuico, tughe, talgwu nk
 
Hivi ni wapi mfanyakazi anaweza kwenda kushitaki ikiwa hatendewi haki na mwajiri wake au ikatokea wakashindwa kuelewana au mfanyakazi akaachishwa kazi na bila kipewa hakiyake inayo stahili wapi kesi hizi hupelekwa nifahamisheni jamani

Ikiwa mfanyakazi anaona kuwa hatendewi na mwajiri wake..haki ambayo imetajwa au kuzungumzwa na sheria za kazi za Tanzania (Employment and Labour Relations Act & Labour Institutions Act na nyinginezo) kama ni haki ya mwajiriwa basi anaweza kuwasilisha malalamiko yake hayo katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ambao watausuluhisha na ukishindikana watauamua..

Kama ni masuala ya kuripoti ajali kazini na malipo yanayohusiana na ajali hiyo basi atawasilisha mgogoro au malalamiko kwa Kamishna wa Kazi ambae kwa mikoani anawakilishwa na Afisa wa Kazi (Labour Officer)...
Kwa suala la kuachishwa kazi bila kupewa haki yake, kwanza ni kosa kwa mwajiri kwani anakuwa amevunja mkataba kati yake na mwajiriwa ambapo mwajiriwa anaweza kufungua kesi ya madai katika mahakama za kawaida kutokana na kuvunjwa kwa mkataba au kupeleka malalamiko yake katika Tume ya usuluhishi na uamuzi(ingawa mikataba mingi ya ajira huweka kifungu kinachoeleza usuluhishi wa mgogoro utakaotokea katika mkataba huo - hivyo ni vizuri kufuata usuluhishi ulioainishwa na mkataba japokuwa ukiachishwa kazi automatically mkataba unakua umevunjika hivyo not necessary kufuata usuluhishi ulioanishwa humo).

Kwa mtumishi wa umma (wao wana sheria yao maana Employment and Labour Relations Act inawahusu sana watumishi wa private organizations) huwezi kufukuzwa au kuachishwa kazi bila kufuata hatua zilizoorodheshwa na sheria yao, kama ikitokea mwajiri akakiuka hatua hizo basi mwajiriwa atawasalisha malalamiko au rufaa yake mbele ya Tume ya usuluhishi wa Umma. Ingawa nae technically anaweza kufanya kesi ya madai kwa kuvunjiwa mkataba wake.
 
Back
Top Bottom