Hivi nini kilimkuta Saida Karoli kimuziki?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Jamani huyu dada alivuma sana lakini sijui nini kilimkuta na ghafla akapotea na naskia hayuko hata vizuri kiuchumi. Nashangaa kwasababu alipiga sana show kubwa lakini bado hakuwa sawa kiuchumi.

Nini tatizo???
 
Ukifikiria tu kuwa nyimbo alikuwa anatunga na kuimba yeye lakini hazikuwa zake bali za meneja wake utaelewa zaidi nini kilimkuta mfano swala la Diamond kurudia wimbo wa Salome.
 
kilichomkuta ni kuwa badala ya yeye kuwa tajili mkubwa kuna mjanja flan alimtumia vema na huyo jamaa leo ni bonge la don hapa town hadi akabadili radio station yake tika jina la kiswahili na ikawa jina la kizungu na ndiye don ambae ukigombana nae kama ww mwanamuziki ujue ndo mwsho wako kimuziki!,dada komando wa plado alishituka akakimbia ila nae kamuwekea vizuizi vya kimuziki na maisha....jina simjui lakn
 

Duuuh,
Hivi hapa Tanzania kuna mtu ana nguvu kiasi hiki unachosema???
Kivipi anawaua wasanii wa muziki???
 
Ukifikiria tu kuwa nyimbo alikuwa anatunga na kuimba yeye lakini hazikuwa zake bali za meneja wake utaelewa zaidi nini kilimkuta mfano swala la Diamond kurudia wimbo wa Salome.

Kwanini jamani?
Meneja wake Saida ni nani???
 
Dada ameamua kupumzika kimziki jamani. Muacheni
Kapumzika au kachoka na muziki maana mpaka kesho akitoa nyimbo inakuwa sio yake ni ya meneja wake na yeye aambulii chochote
 
Walisema Wahenga 'Kila zama na kitabu chake'

Kilichomkuta yeye ndio kilichowakuta kina Kanda Bongoman, Naughty by nature, Mzee Zahiri Ally...hivi umewahi kuusikiliza vizuri ule wimbo wa 'Sakina' wa Mzee Zahiri Ally alafu uniambiae ni Msanii gani wa leo anaweza kufanya kazi kama ile?

Lakini ndio hivyo tena, Zama zimepita, tunaojua ladha nzuri tutaendelea tu kusikiliza kivyetu vyetu lakini hawa wa kizazi kipya wala hawana habari.
 
Msiwe mnaongea vitu msivyovijua, ukiendelea hivi ipo siku utakalia kitu cha ncha kali
 
Ndo maana wasanii wanasisitiziwa elimu hawataki.
Elimu ni tofauti na kipaji mkuu wengi wenye vipaji hawakujaliwa kuwa na elimu kubwa mkuu..

Diamond hana elimu kubwa kushinda Wakina Ben Pol,One incredible na wasanii wengine Kibao.

Kikubwa kinachotakiwa ni kujitambuwa na kujua unataka nini...uwe mjanja kwenye mikataba maana mikataba inaandikwa kwa lugha mama.

Na hata kama lugha inayotumika huijui kuna wanasheria kibao na Ofisi zao mitaani Tumia hao.

na hili swala la mikataba halipo kwenye muziki tu leo wakina Ibrahim Ajib wanalipwa mishahara midogo kuliko wachezaji wa kigeni wakati kiuhalishia wao ndio wanastahili mamilioni jinsi wanavyojitoa kwenye team kuliko wageni
 
duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuhhhhhhhhhhhhhhhh ni shidaaaaaaaaaaaaaah
 
Management yake ya hapo awali ndiyo iliyo mwangusha, ELIMU ELIMU ELIMU nayo kwake inakaa upande, zaidi ya yote kila Jambo na Zama zake. Walimzulumu kilicho chake na kumuacha mpofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…