Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Hivi nini kinaendelea kwa huyu bi dada loveness love a.k.a deeva wa clouds, kwasababu lately amekuwa akipost Instagram ujumbe ambao katika hali ya kawaida unaweza kuhisi kuwa hayupo sawa kabisa kwenye akili yake.
Ila kulingana na maneno aliyopost katika account yake ya Instagram ninaweza kulinganisha na kaulu zinazotolewa na baadhi ya wasichana wa kaliba yake mfano ni Johari wa bongo movie, faiza wa sugu, uwoya, wolper, wema sepetu, na wengineo. Hawa wamekuwa wakitoa kauli ambazo zinaashiria kuwa maisha yao ya kuishi kwa kujiachia na kufanya fujo za mjini yanaelekea ukingoni.
Wametumia usichana wao kufanya maisha ya uhuru uliopitiliza ambao haukujali kuwa wao kama wengine waliokuwapo kabla ya wao kuzaliwa wanawajibika kwa matumizi ya muda wao hapa duniani.
Kauli za hawa wadada zimejawa na hofu, wasiwasi, kukata tamaa, majuto, na simanzi. Wakiwatazama wenzao kama wao ambao nao walikuwa katika hali ya usichana sema waliamua mapema sana na kuamua kutazamia kuwa ujana ni maji ya moto na hakuna marefu yasiyokuwa na ncha na wakaamua kutulia na maisha na hatimaye kupotea katika media na habari za skendo na sasa wanaishi maisha ya kawaida ya utulivu, basi hii huwapa maumivu sana.
Hapa nawazungumzia wasichana waliowahi kuwa maarufu kama Jackline ntuyabaliwe, nancy sumari, Faraja kota, irene kiwia, nagris mohamed na wengineo wengi, ambao hivi sasa wanafamilia zao na wanamaisha mazuri tu ya utulivu kitu mambacho hawa wengineo imekuwa ni shaka kukipata.
Leo hii wamebaki kujinasibu na kutoa kauli za kujipa moyo ila ni wazi kuwa wamekwama na wanamajuto mengi sana na wanapata ukichaa wa hiyari. Imagine leo deeva anaanza kutafuta mwanaume, wa kupata nae watoto na kuanza familia serious anampataje?!
Hii kitu iwe fundisho kwa watoto wa kike ambao huwa wanahisi maisha ni mzaha mzaha na michezo ya mahusiano na kufanya wanachotaka.
Mambo ya kujiita sijui "slay queens", " independent woman" halafu kuishi maigizo mwisho wa siku wenzako uliokuwa unafanya nao upumbavu kumbe walikuwa na ramani za maisha za kimya kimya. Unakwama unabakia kutoa toa makauli ya kijinga.......