Hivi nini maana baadhi ya maghorofa kuandikwa "plaza"

Plaza ni eneo la kijamii na kibiashara lina maduka na shughuli kijamii au nyinginezo za aina hiyo, ni kama public square mara nyingi linakuwa eneo la wazi tofauti na shopping mall ambayo huwa ni jengo maalum lenye maduka na huduma za kibiashara
Huku kwetu tunachanganya ili kuonekana utofauti mwisho plaza na mall zinaonekana zote sawa
 
Plaza za kwetu kaghorofa kamoja tu mtu keshamaliza kazi anapachika jina plaza
 
Na complex
 
Complex, Plaza, Tower, Mall, Square hizi zote zina maana tofauti.

Mwanzoni nilikuwa napata ukakasi wa kutofautisha, Hostel, Hotel, Motel, Lodge, Inn na Guest. Kila kitu kina maana kulingana na muktadha wake.
 
Plaza za kwetu kaghorofa kamoja tu mtu keshamaliza kazi anapachika jina plaza
Asili ya Plaza ni Spain ni maeneo ya kawaida tu, hayana ghorofa, public square mara nyingi katikati ya majengo makubwa
 
Complex, Plaza, Tower, Mall, Square hizi zote zina maana tofauti.

Mwanzoni nilikuwa napata ukakasi wa kutofautisha, Hostel, Hotel, Motel, Lodge, Inn na Guest. Kila kitu kina maana kulingana na muktadha wake.
Mlimani city ilipaswa kuitwa Plaza kama isingejengewa kwa ndani, lakini inaitwa Complex kama Masaki Complex pia
Oysterbay centre na Slipway ni Plaza
Tower inakuwa na ofisi na residential, kama PSSF Tower na Golden Jubilee
Square kama Mnazi Mmoja au Dodoma Nyerere Square ni eneo la wazi kwa biashara na mikutano au shughuli za nje
 
Back
Top Bottom