Hivi nyie mna watoto? Mkirudi nyumbani watoto wenu mnawatazama vipi?

Mi mi

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
2,748
Reaction score
5,112
Hivi nyie watekaji na wauaji mna watoto ? Mkirudi nyumbani watoto zenu mnawatazama kwa macho gani ?

Watoto nao wanasema baba/mama ametoka kazini. Kazi gani ya kutesa na kuua wenzako ?

DAMU YA DEUSDEDITH SOKA (DEO)
20240826_192923.jpg

Siku ya Jumatano ya tarehe 21 August 2024 nilikuwa maeneo ya Buza pamoja na Viongozi wa CHADEMA wa Wilaya ya Tameke kukusanya taarifa kuhusu tukio la kupotea Viongozi wawili na mwanachama mmoja wa CHADEMA.

Katibu wa Wilaya Jacob Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise ambao walipotea siku ya Jumapili saa 5:00 Asubuhi maeneo ya Buza, Wilaya ya Temeke.

Nilikuwa katikati ya kazi na tayari tunapata footage na trace back za hatua za mwisho za Deusdedith Soka na wenzie kabla ya kupotea kabisa.

Ghafla nilipigiwa simu nahitajika Makao makuu ya CHADEMA ndugu zake Soka na Mlay walikuwa wamefika ofisi za Makao makuu ya CHADEMA kuulizia taarifa za ndugu zao.

Mpaka kufikia saa 8 :00 mchana mimi pia niliungana na wenzagu katika kikao kile.

Swali kutoka kwa watu wote lilikuwa.. nimefikia wapi kuhusu kutafuta habari na taarifa za walipo akina Soka?

Lakini kabla sijaongea lolote ghafla Baba Mtu mzima aliangua kilio kikubwa sana na machozi mengi yalitirika akijipiga piga kifuani kwa majuto.

Anamuomba Mungu aingilie kati wasimuue mtoto wake, anajuta anasema hatofanya tena kosa la kumuacha mtoto wake mbali.

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Martin Maranja Masese waliokuwa karibu naye walimshika mabegani kwa huzuni kubwa sana wakimsihii anyamaze, asikate tamaa, tuungane kumpigania mwanae.

Watu wote mle ndani walikuwa kimya sana kwa dakika kadhaa, niliona kila mtu anadondosha machozi kwa hisia kali za kilio cha yule Baba.

Siyo wanaume siyo, wanawake ilikuwa ni huzuni kubwa kumuona mwanaume mtu mzima akilia hadharani na kutamka maneno ya majuto.

Utulivu uliporejea, hakuna mtu aliyethubutu kunyanyua mdomo kwa dakika kadhaa, basi nikajikuta naanza kumuhoji yule Baba wewe ni nani? na Kijana wako ni yupi?

Akajitambulisha kuwa yeye ni Baba mdogo wa Deusdedith Soka, anaitwa Cyprian Soka ni Mkazi wa Wilaya ya Temeke maeneo ya Buza ila hakuwa anaishi na Deusdedith Soka nyumba moja.

Deo ambaye sisi tunamfahamu kama Soka ni mtoto wa marehemu Kaka yake Cyprian Soka.

Soka anaishi peke yake katika mji alioachiwa na marehemu Baba yake (Kaka yake Cyprian) pale Buza akiwa na wapangaji kadhaa.

Mama yake Deusdedith Soka alishafariki siku nyingi, Deusdedith Soka hana Baba wala Mama kwa sasa, wamezaliwa wawili tu yeye na dada yake ambaye ameolewa Kinyerezi, na ana familia yake.

Marehemu Kaka yangu alinikabidhi mimi na Kaka yangu mwingine aitwaye Didas Soka hawa watoto wakiwa wadogo sana niwaangalie dakika chache kabla ya kifo chake, alinisisitiza sana niwatizame hadi watakapokuwa watu wazima.

Najihisi nina hatia nimeshindwa kukamilisha kiapo cha Kaka yangu (analia tena kwa dakika kadhaa) nimeshindwa hata kwenda katika kazi zangu za Daladala, namtafuta Deusdedith Soka leo siku tatu.

Kabla hajaendelea simu yake inaita anapokea anaweka ‘loud Speaker’ anaongea mwanamke mtu mzima sana anaanza na swali “Soka Vipi..?”

Cyprian Soka anajibu “Deo bado hajapatikana” yule Mama kwenye simu anaangua Kilio kikubwa sana

“Wamemuua mjukuu wangu, Wamemuaa mjukuu wangu”

Cyprian anambembeleza lakini inashindikana kabisaaa, Cyprian anakata simu ili aendelee na mazungumzo..

Cyprian anatueleza kuwa “Huyu ni Bibi yake Deo (Soka), Aisee tutampoteza Mama yangu kama Deusdedith Soka hatopatikana..”

Cyprian anaanza kulia tena akiwaza K
Kumpoteza mtoto wa Kaka yake ambaye alikula kiapo dakika za mwisho za uhai wa Kaka yake kumtizama hadi atakapokuwa mtu mzima na pili kumpoteza Mama yake ambaye ni Bibi yake Soka.

Cyprian anatueleza anavyopataga shida akisikia Deusdedith Soka amekamatwa na Polisi na yupo mahabusu za kawaida vipi hili la Kutekwa na mupotea..?

Anaeleza hata mara ya Mwisho Deusdedith Soka alipokamatwa akiwa anataka kwenda mkoani Mbeya, Cyprian hakuwa anajua habari hiyo mpaka Deusdedith Soka alipokuja kutoka baadae.

Siku ya Safari ya Mbeya ,Deusdedith Soka alienda kuazima pikipiki kwa Baba yake Mdogo (Cyprian).

Siku hiyo Soka kabla hajaanza safari alikamatwa Mwembeyanga akiwa na Vijana wengine wa BAVICHA

Deusdedith Soka alipaki pikipiki nyumbani kwake Buza hakuirudisha kwa Baba yake mdogo Cyprian.

Baba mdogo alijua kwa kuwa bado ana pikipiki yake basi yupo jirani palepale Buza.

Leo Jumapili nimewaza endapo Wamemwaga Damu ya soka, watakuwa wamemuua damu ya bibi yake Deusdedith Soka pia.

Nikajikuta najiuliza ipo wapi "RESILIENCE" ya Mama @SuluhuSamia? Je vyombo vyake vya dola vimeshindwa Kumvumilia Deusdedith Soka?

Deusdedith Soka Soka ni Kijana mdogo machachari ambaye alikuwa anahitaji kutiwa moyo na kurekebishwa anapokosea na siyoumpoteza na kukatisha uhai wake.

Nikakumbuka kisa cha Rais Jakaya Kikwete alivyokuwa anampenda sana John Mnyika wa CHADEMA akiwa anajenga hoja na kuikosoa serikali ya CCM Mnyika akiwa mdogo sana na kabla hajawa Mbunge.

Rais Jakaya Kikwete alimfikishia ujumbe John Mnyika kuwa anampenda sana na angetamani kuona anatimiza ndoto yake ya kuwa Mbunge hapo mbeleni.

Jakaya akamuahaidi kumsaidia Mnyika kwa kumchangia fedha ili Kuwa mbunge wa kupitia CHADEMA ili akaone cheche zake Bungeni.

Baadae Mnyika alikuja mujulikana nchi nzima kwa namna alivyokuwa anaibana serikali Bungeni na kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya CCM.

Vipi kama Rais Jakaya Kikwete na vyombo vyake vya dola visingemvumilia John Mnyika vikaamua kumteka na kumpoteza sababu ya ukosoaji wake miaka ile ya 2007 hadi 2010 tungefanikiwa kuona kipaji na uwezo wa Mnyika leo hii .?

Nidhahiri nchi ingekosa huduma ya John Mnyika Bungeni na nje ya Bunge.

Masikini Damu ya Soka...!

Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority.
 
Vijana wenzangu haitokaa itokee mbowe au tundu lissu atekwe nyie vijana mnojifanya mna midomo kubwekea watu ndo zitawatokea scenario kma hizi
Ona sasa familia inapata tabu wakati mtto wa lissu yupo marekani

Akili kumkichwa
 
Hivi kwani huyu kijana alikuwa anatukana watu mitandaoni au wameamua tu kumzimisha ?
Kuna ushahidi wowote tuuone?
 
Hao wauwaji Kwa vyovyote Huwa wanavuta bangi na akili hawana.Mwenye akili timamu hawezi kuua binadamu na akaendelea kuishi Kwa amani
 
Sio hali ya kawaida
 
Hivi nyie watekaji na wauaji mna watoto ? Mkirudi nyumbani watoto zenu mnawatazama kwa macho gani ?

Watoto nao wanasema baba/mama ametoka kazini. Kazi gani ya kutesa na kuua wenzako ?

DAMU YA DEUSDEDITH SOKA (DEO)
View attachment 3079928
Siku ya Jumatano ya tarehe 21 August 2024 nilikuwa maeneo ya Buza pamoja na Viongozi wa CHADEMA wa Wilaya ya Tameke kukusanya taarifa kuhusu tukio la kupotea Viongozi wawili na mwanachama mmoja wa CHADEMA.

Katibu wa Wilaya Jacob Godwin Mlay, Deusdedith Soka na Frank Mbise ambao walipotea siku ya Jumapili saa 5:00 Asubuhi maeneo ya Buza, Wilaya ya Temeke.

Nilikuwa katikati ya kazi na tayari tunapata footage na trace back za hatua za mwisho za Deusdedith Soka na wenzie kabla ya kupotea kabisa.

Ghafla nilipigiwa simu nahitajika Makao makuu ya CHADEMA ndugu zake Soka na Mlay walikuwa wamefika ofisi za Makao makuu ya CHADEMA kuulizia taarifa za ndugu zao.

Mpaka kufikia saa 8 :00 mchana mimi pia niliungana na wenzagu katika kikao kile.

Swali kutoka kwa watu wote lilikuwa.. nimefikia wapi kuhusu kutafuta habari na taarifa za walipo akina Soka?

Lakini kabla sijaongea lolote ghafla Baba Mtu mzima aliangua kilio kikubwa sana na machozi mengi yalitirika akijipiga piga kifuani kwa majuto.

Anamuomba Mungu aingilie kati wasimuue mtoto wake, anajuta anasema hatofanya tena kosa la kumuacha mtoto wake mbali.

Mwenyekiti Freeman Mbowe na Martin Maranja Masese waliokuwa karibu naye walimshika mabegani kwa huzuni kubwa sana wakimsihii anyamaze, asikate tamaa, tuungane kumpigania mwanae.

Watu wote mle ndani walikuwa kimya sana kwa dakika kadhaa, niliona kila mtu anadondosha machozi kwa hisia kali za kilio cha yule Baba.

Siyo wanaume siyo, wanawake ilikuwa ni huzuni kubwa kumuona mwanaume mtu mzima akilia hadharani na kutamka maneno ya majuto.

Utulivu uliporejea, hakuna mtu aliyethubutu kunyanyua mdomo kwa dakika kadhaa, basi nikajikuta naanza kumuhoji yule Baba wewe ni nani? na Kijana wako ni yupi?

Akajitambulisha kuwa yeye ni Baba mdogo wa Deusdedith Soka, anaitwa Cyprian Soka ni Mkazi wa Wilaya ya Temeke maeneo ya Buza ila hakuwa anaishi na Deusdedith Soka nyumba moja.

Deo ambaye sisi tunamfahamu kama Soka ni mtoto wa marehemu Kaka yake Cyprian Soka.

Soka anaishi peke yake katika mji alioachiwa na marehemu Baba yake (Kaka yake Cyprian) pale Buza akiwa na wapangaji kadhaa.

Mama yake Deusdedith Soka alishafariki siku nyingi, Deusdedith Soka hana Baba wala Mama kwa sasa, wamezaliwa wawili tu yeye na dada yake ambaye ameolewa Kinyerezi, na ana familia yake.

Marehemu Kaka yangu alinikabidhi mimi na Kaka yangu mwingine aitwaye Didas Soka hawa watoto wakiwa wadogo sana niwaangalie dakika chache kabla ya kifo chake, alinisisitiza sana niwatizame hadi watakapokuwa watu wazima.

Najihisi nina hatia nimeshindwa kukamilisha kiapo cha Kaka yangu (analia tena kwa dakika kadhaa) nimeshindwa hata kwenda katika kazi zangu za Daladala, namtafuta Deusdedith Soka leo siku tatu.

Kabla hajaendelea simu yake inaita anapokea anaweka ‘loud Speaker’ anaongea mwanamke mtu mzima sana anaanza na swali “Soka Vipi..?”

Cyprian Soka anajibu “Deo bado hajapatikana” yule Mama kwenye simu anaangua Kilio kikubwa sana

“Wamemuua mjukuu wangu, Wamemuaa mjukuu wangu”

Cyprian anambembeleza lakini inashindikana kabisaaa, Cyprian anakata simu ili aendelee na mazungumzo..

Cyprian anatueleza kuwa “Huyu ni Bibi yake Deo (Soka), Aisee tutampoteza Mama yangu kama Deusdedith Soka hatopatikana..”

Cyprian anaanza kulia tena akiwaza K
Kumpoteza mtoto wa Kaka yake ambaye alikula kiapo dakika za mwisho za uhai wa Kaka yake kumtizama hadi atakapokuwa mtu mzima na pili kumpoteza Mama yake ambaye ni Bibi yake Soka.

Cyprian anatueleza anavyopataga shida akisikia Deusdedith Soka amekamatwa na Polisi na yupo mahabusu za kawaida vipi hili la Kutekwa na mupotea..?

Anaeleza hata mara ya Mwisho Deusdedith Soka alipokamatwa akiwa anataka kwenda mkoani Mbeya, Cyprian hakuwa anajua habari hiyo mpaka Deusdedith Soka alipokuja kutoka baadae.

Siku ya Safari ya Mbeya ,Deusdedith Soka alienda kuazima pikipiki kwa Baba yake Mdogo (Cyprian).

Siku hiyo Soka kabla hajaanza safari alikamatwa Mwembeyanga akiwa na Vijana wengine wa BAVICHA

Deusdedith Soka alipaki pikipiki nyumbani kwake Buza hakuirudisha kwa Baba yake mdogo Cyprian.

Baba mdogo alijua kwa kuwa bado ana pikipiki yake basi yupo jirani palepale Buza.

Leo Jumapili nimewaza endapo Wamemwaga Damu ya soka, watakuwa wamemuua damu ya bibi yake Deusdedith Soka pia.

Nikajikuta najiuliza ipo wapi "RESILIENCE" ya Mama @SuluhuSamia? Je vyombo vyake vya dola vimeshindwa Kumvumilia Deusdedith Soka?

Deusdedith Soka Soka ni Kijana mdogo machachari ambaye alikuwa anahitaji kutiwa moyo na kurekebishwa anapokosea na siyoumpoteza na kukatisha uhai wake.

Nikakumbuka kisa cha Rais Jakaya Kikwete alivyokuwa anampenda sana John Mnyika wa CHADEMA akiwa anajenga hoja na kuikosoa serikali ya CCM Mnyika akiwa mdogo sana na kabla hajawa Mbunge.

Rais Jakaya Kikwete alimfikishia ujumbe John Mnyika kuwa anampenda sana na angetamani kuona anatimiza ndoto yake ya kuwa Mbunge hapo mbeleni.

Jakaya akamuahaidi kumsaidia Mnyika kwa kumchangia fedha ili Kuwa mbunge wa kupitia CHADEMA ili akaone cheche zake Bungeni.

Baadae Mnyika alikuja mujulikana nchi nzima kwa namna alivyokuwa anaibana serikali Bungeni na kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya CCM.

Vipi kama Rais Jakaya Kikwete na vyombo vyake vya dola visingemvumilia John Mnyika vikaamua kumteka na kumpoteza sababu ya ukosoaji wake miaka ile ya 2007 hadi 2010 tungefanikiwa kuona kipaji na uwezo wa Mnyika leo hii .?

Nidhahiri nchi ingekosa huduma ya John Mnyika Bungeni na nje ya Bunge.

Masikini Damu ya Soka...!

Boniface Jacob
Ex-Mayor
The voice of the silenced Majority.
Magufuli na wenzake ndiyo chanzo cha ushetani huu, awamu hii imeunganisha hapohapo sasa Watanzania tumeona hili ni jambo la kawaida na sasa linaenda kuwa utamaduni wetu yaani kutekana na kuuana, mtu kuikosoa serikali inaonekana kuwa dhambi kubwa na hatimaye yake ni kuuawa, hatupaswi kuendelea kumlilia Mungu na kumpa majukumu yasiyokuwa ya lazima, ikiwezekana nchi tuigawane vipande vipande basi tu atakaye salia asalie atakaye ondoka aondoke tu
 
Back
Top Bottom