Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

supu ya mapupu
 
Sipendi kabisa kusikia upuuzi huo eti pizza pizza kwenda kula nakutana na chapati zilichomwa bila mafuta na ujinga gani sijui wameupaka kwa juu. Alafu kale kamuhudumu kananibania pua eti elfu 10 tu kaka,
 
Sipendi kabisa kusikia upuuzi huo eti pizza pizza kwenda kula nakutana na chapati zilichomwa bila mafuta na ujinga gani sijui wameupaka kwa juu. Alafu kale kamuhudumu kananibania pua eti elfu 10 tu kaka,
umeona eeh.. Chapati kama kaukau. Mkuu wapi wanauza Elfu kumi? dar huwa wanauza kuanzia elfu 18 hadi 25 baadhi ya sehemu, kisha wanakuuzia soda buku au buku mbili. Mimi nakunywa soda, Pizza nanunua tu. Mara nyingi nina rafiki yangu anapenda hivyo nanunua ili afurahi nami nakula kipande kimoja lakini sisikii chochote. Baga ndo poa. Halafu baga unamwambia akuwekee pilipili.
 
Mi mshamba wa Mbeya huko Pizza na Burger nazionaga tu kwenye tiviii hivi utamu wake ukoje?? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haha ha,@malyafale banah...
Ile condiment inafanana na uharo ni ufuta ule,mwanzo hata mimi ilinichanganya ila ukiizoea utaipenda tu kwani ina radha ya uchachu wala haiwezi kukutia kichefuchefu..

Ila mayonise ndo hiyo nadhani unasema inafanana na makohozi,ha ha ha.

Binafsi pizza haipandi,kitu ni burger bana
 
Mkuu wewe upo vizuri. Tutafutane tukale burger, Yule jamaa alokuwa akitengeneza pale Moroco kahamia Africa sana. Twenzetu baada ya hapo tukanywe soda pale kwenye bustani ya Ambiance. Tutakaa huku tukijadiliana fujo za akina espy kule MMU.
 
Dah! Bora nimepata mwenzangu. Haya mauchafu huwa siyafagilii hata kidogo. Huwa nashangaa sana nikiona watu wanavyohehuka nayo. Niwekee ugali wangu na samaki wa kukaanga mchicha chukuchuku au wa nazi, pilipili debe na gudulia langu la maji roho yangu KWATUU.

 
Shida kuizoea ile mayonnaise, mara ya kwanza kidogo nitapike
 
Hahahaaa...Mkuu umenichekesha sana. Mimi bado nina imani kwamba wengi wanakula kwa mkumbo tu, Hivi unaanzaje kuwa na hamu ya Pizza? Natamani Serikali ipige maarufuku.

Ulishakula ugali wa Muhogo au wa Mtama na mboga ya samaki? mchicha au hata samaki apikwe na karanga zile za kusaga. yani ni kujilamba vidole. Utashinda unakunywa maji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…