Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Wakuu kwema?
Habari hapo kwa majirani ni mzee Odinga anadai alishinda uchaguzi na anasema ataitisha maandamano makubwa ya kwenda kumtoa Ruto Ikulu
Uchaguzi ulikuwa wa wazi na matokeo yote yaliyotoka vituoni na kusainiwa na mawakala wa pande zote yote yalikuwa uploaded online
Na kama kuna wizi wa kura ulifanyika ni rahisi kujua sababu mawakala wa pande zote wana fomu ambazo copy zake zipo online,
Odinga na timu yake ya wanasheria hawakuweza kutoa hata copy ya kituo kimoja ambayo matokeo ya mawakala wake yalitofautiana na yaliyowekwa online, na ndio maana majaji wote waliona ile kesi haikuwa na mashiko
Sasa huyu Odinga anasema aliibiwa kura, Tume ya Uchaguzi na mahakama Kuu zote zilinunuliwa na Ruto na kumpora ushindi na watu wengi sana wanamuamini,
Najiuliza huyu jamaa ametumia uchawi gani kuwashika Wakenya wengi namna hii akili?
Wanasema ndiye mlinzi wa demokrasia ila ukifuatilia utaona ndiye adui mkubwa wa demokrasia
Aliungana na Serikali ya Uhuru (aliyokuwa amedai pia ilimuibia kura na kusababisha vurugu zilizoua watu wengi) aliungana na serikali ya Uhuru kuweka maafisa wa tume ambao wangependelea chama chake, wakiongozwa na yule mama aliyeitwa Cherera
Raila pamoja na watu wa serikali ya uhuru waliwashinikiza mwenyekiti wa Tume Wafula Chebukati kumpendelea Raila na kumtishia na kumtumia maafisa wa jeshi, polisi na usalama wa Taifa, huyu ndio mtetezi wa demokrasia?
Raila anapuuza uamuzi wa mahakama, na kuchochea kuwa imenunuliwa, kabla ya hapo aliahidi kuwa ataiheshimu hata kama ikitoa uamuzi dhidi yake
Mtetezi au adui wa demokrasia?