Hivi rais kuhidhinisha pesa ili zifanye kazi ni hisani au ni wajibu?

Hivi rais kuhidhinisha pesa ili zifanye kazi ni hisani au ni wajibu?

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu Heshima mbele kwanza.

Msikilize hapa mbunge wa makambako Deo sanga👇

Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema kuwa wanamekuwa wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu yeye ndiye anayeidhinisha fedha kwenda kutekeleza miradi mbalimbali kwenye majimbo.

Sanga amesema hayo wakati akichangia hoja katika bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2024/25 ambapo amewataka wanasiasa wa upinzani kutojizima data kwa kuwashangaa wabunge wanapomshukuru Rais Samia.

Ninauliza ili kujifunza Rais kuhidhinisha pesa ni Hisani kwamba akiamua anaweza akagoma hivyo lazima kumshukuru au ni wajibu wake na ni lazima afanye hivyo sababu katiba inahitaji afanye hivyo?

 
Hakuna hisani hapo. Huo ni wajibu wake. Hata sifa wanatakiwa kupewa walipa kodi, na siyo yeye ambaye hata mshahara wake tu nasikia haukatwi kodi.
 
Back
Top Bottom