CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Mgombea wa CCM John Magufuli amenukuliwa siku za hivi karibuni kwenye kampeni zake kuwa alipoapishwa kuwa Rais wa Tano wa Tanzania moja ya mambo aliyoyafanya ni kutotoka nje ya nchi na hasa kutokwenda nchi za Ulaya na Marekani.
Sababu za kutokwenda Ulaya na Marekani ni kuwa yeye ni mzalendo na alitaka kuchapa kazi na kubana matumizi.
Hoja zake zote hazina mashiko na inaonesha ni kwa kiwango gani haelewi kabisa kuhusu uhusiano wa biashara ya kimataifa na diplomasia.
Kuna faida kubwa rais wa nchi kukutana na viongozi wenzake huko duniani kuliko kujifungia ndani, nitaorodhesha hapa chini.
Enjoy your lunch if you can access any maana najua wengine humu hata chakula cha mchana leo hampati hii ni kutokana na Serikali ya CCM kubana kila kona si Sekta Binafsi ama ya Umma.

- Angelipata uelewa mpana wa dunia kuhusu ushindani wa biashara na namna ya kufaidika nao. Sio porojo eti tuko kwenye vita ya kiuchumi, nani awe na vita na Tanzania kwenye vita ya kiuchumi. Vita ijulikanayo ya kiuchumi ni kati ya China na USA (Mashariki dhidi ya Magharibi), sisi wengine hatugombani na mtu bali tunagombaniwa. Angelielewa hili angejua namna ya kufaidika na pande zote mbili.
- Angeweza kushinda dili kubwa za kijamii na kiuchumi kwa kushikana mkono tu na viongozi mbalimbali, mfano kukutana tu na rais wa Marekani kungeweza kuishawishi marekani kuongeza fursa za watanzania wanaoenda Marekani kimasomo, hivyo hivyo kwa nchi za Ulaya.
- Hoja kwamba anabana matumizi ni propaganda na uongo wa wazi, kwani tunashuhudia jinsi ziara zake za ndani na hata wakati huu wa kampeni zinavyotumia rasilimali za umma kwa ajili ya ulinzi wake na kuwalipa kundi kubwa la watu anaotembea nao.
- Kazi ya urais ni kutoa dira na siyo kazi ya utendaji, hivyo haina ulazima eti lazima uwe ndani ya nchi 27/7, anayoyafanya John Magufuli ni working hard but not smart.
- Kwa kumalizia kutokuwa na exposure ya masuala ya dunia kwa John Magufuli kumelifanya Taifa kufikiri kijima, yaani ni kama tuko kwenye kupigania uhuru, si ajabu majina kama mabeberu na mengine mengi ya kibaguzi anapenda kuyatumia, akidhani bado anapigania uhuru. Dunia ya leo huwezi kufanikiwa ikiwa bado unaendekeza sera za aina ya Magufuli ambazo zinashabihiana kabisa na zile za Julius Malema wa Afrika ya Kusini ama hayati Robert Mugabe ambaye aliiharibu nchi iliyokuwa inaheshimika kiuchumi kusini mwa jangwa la Sahara.
Enjoy your lunch if you can access any maana najua wengine humu hata chakula cha mchana leo hampati hii ni kutokana na Serikali ya CCM kubana kila kona si Sekta Binafsi ama ya Umma.