Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Hivi Rais Magufuli alifanya maamuzi ya busara kwa kuwaita Wakuu wa Vyombo vya Usalama kuongelea COVID19, badala ya kuwaita Wataalamu wa Afya?

Sisi tunafanikisha tena sana tu, inategemea wewe binafsi mtazamo wako upo vipi.

Kama glass imejaa nusu kwenda juu au imepungua nusu kwenda chini, hilo ni suala la akili yako binafsi.
Mafanikio sio pesa Hadi uitoe mfukoni ndi ionekane, tofautisha kufanisha na propaganda za tbc
 
Tuliona wenyewe Rais Magufuli akiwaita wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini, wengi wakitoka jijini Dar na wengine wakitokea Dodoma, umbali mrefu wa kilometa maelfu, kuongelea ugonjwa wa corona, ambao unatikisa dunia nzima hivi sasa, ikiwemo Tanzania.

Nimekuwa nikijiuliza hivi si yeye mwenyewe ndiye aliyeunda hii Tume ya kitaifa, inayoshughulikia na kuratibu masuala yote ya ugonjwa wa corona nchini, akiwemo waziri Mkuu, Kasim Majaliwa na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, mbona sijawaona wakiwa ni miongoni ya waalikwa kwenye kikao hicho?

Hivi Mheshimiwa Rais, anadhani kuwa ugonjwa wa corona utaondoka nchini kwa vifaru vya kijeshi, au mabomu ya machozi, au bunduki "zilizokokiwa" risasi za moto, au magari ya washawasha ya IGP Sirro?

La hasha, asijidanganye, hivyo virusi haviwezi kamwe kuondoka nchini kwa nguvu za kijeshi nchini, kwa kuwa hivyo virusi vya corona ni "invicible enemy"

Kwa kuwa kama nguvu za kijeshi zingekuwa na uwezo wa kuondoa virusi hivyo, basi Taifa kama Marekani linaloongoza duniani kwa nguvu za kijeshi, lisingekuwa linapelekwa "mchakamchaka" hadi sasa hivi likiwa ndilo linaloongoza duniani kwa maambukizi mengi na vifo pia

Mimi sikuona mantiki ya kuwaita wakuu wa vyombo vya usalama wa nchini kuongelea ugonjwa wa Corona nchini, wakati akiwaacha wataalamu wa Afya,ambao hivi sasa ndiyo wako mstari wa mbele kabisa katika vita hii ya kuutokomeza ugonjwa wa Corina nchini.

Kwa kuwa tunadadavua kujua mantiki ya Mheshimiwa Rais, kuwaita wakuu hao wa vyombo vya usalama nchini kwenda kijijini kwake Chato na kwenda kuwahutubia kuhusu suala la kiafya, nawakaribisha sana wadau nanyi mtoe maoni yenu
Issue si kuitwa daktari au nesi au mkuu wa wilaya au vinginevyo iwavyo, bgali nhi ujumbge bganhi wanakwenda kupewa ama kujadili. Kikao kile hakikuhitaji dokta wala nesi kwa maudhui yake ndio maana hawakuitwa.

Nakushauri uende ukasikilize tena maudhui & ujumbe wa kikao kile + maelekezo + maagizo yaliyotolewa siku ile.
 
Back
Top Bottom