Kosa lake jingine ambalo linamuangamiza ni kuamini, ndoa yake na mzungu ndio kila kitu katika maisha yake huku anasahau kuendeleza kipaji chake. Sijajua kwa nn vijana wanaona deal kuoa wazungu eti kwa sababu ya kupata makaratasi ya kuishi ulaya huku wakisahau kupigania vipaji vyao, siku wakipigwa chini na hao wazungu sijui itakuwaje.
Kosa lake la pili ni kuingilia ugomvi usiowahusu (ugomvi wa sugu na ruge).Ukiangalia ugomvi wa sugu na ruge haukuwa kwa ajili ya kutetea maslai (walidhulumiana ela za wafadhili katika mradi wa marelia) ya mziki na wasanii, bali ulikuwa wa kutetea maslai yake mwenyewe sugu kwa kuwatumia wasanii wabongo fleva ili apate support, kwa kuanzisha anti-virus movement. Haya leo hii sugu na ruge wamepatana na uswahiba wao unazidi kuimarika, je wasanii bado hawanyonywi?,je wasanii hao walioanzisha hiyo movement wanapata airtime na show za kutosha?, jibu ni hapana mimi paka sasa nikiangalia mziki huu wa bongo fleva sijaiona effect yoyote ya anti-virus movement. Wasanii wote waliomsapoti sugu walitakiwa wajiulize, je hii vita tunaipigana kwa maslai ya nani, sisi pamoja na industry ya bongo fleva tutapata nini? Sasa hivi angalia mtu kama Rama dee mm mwenyewe namkubali sana na nyimbo ninayoikubali ni Ile aliyofanya na jide lkn haikupata airtime ya kutosha. Njoo kwa mapacha wako hoi wamezidiwa na msanii waliomkaribisha dar Joh makini wame kaa nae ghetto moja lkn leo wana wanalalamika njaa huku Joh anazidi kutusua. Ujue siku zote unapoingia ktk vita yoyote jiulize hii vita na pigana kwa maslai ya nani?