Mbahili
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 281
- 525
Hakuiva na Manji wenye ganji akasema akabwe,
Panya wakafyata mkia wakapotea wenye ngebe,
Acha kumpinga ukimsema unanyea debe,
Hakua mlevi wa uhuru kunyata kama kalewa,
Labda kama madaraka yanalevya alolevyewa,
Sometimes hivi vyeo vina hangover,
Lake gang wakasukuma wakatakeover,
Ni yeye alileta swaga za ku-fly over,
Ila ni yeye democracy alii-bend over,
Sahani vyombo vya panga na vyombo vya dola alitumia anavyotaka kutuchapa na hii bakora,
Na si kila mfuga makucha hawezi ogopa kurarua,
Kwa Lissu aliona matunda na mwili sio chandarua,
Walojidai wazalendo waliisoma namba kirumi,
Ukikosoa miundombinu tu umehujumu uchumi,
Wakazaliwa chawa wafata upepo ka bendera,
Walojifanya sugu walienda jela,
Watu wakakiita chuma na hakikuwa na huruma,
Na hakikuwa na njia za panya mipango yote ilibuma,
Bado vita havina suluhu na kupona ni Majaliwa,
Sikuweza kuisema pombe ningejua ningepaliwa,
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba,
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba,
Siku Paka akishika mwambie Panya tunataka Katiba,
Hatuogopi hizi shida tutapita hata kama kuna miba,
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele,
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele,
Kuwatesa panya ndio sifa za paka shume,
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele,
Huyo nyau nyau nani atamfunga paka kengele,
Eyoo paka alitawala huu msitu wa serikali,
Panya ndo sisi,