Hivi sasa kwanini naamini kibwetele aliwahadaa wafuasi kanisani na kuwachoma moto

Hivi sasa kwanini naamini kibwetele aliwahadaa wafuasi kanisani na kuwachoma moto

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
9,722
Reaction score
15,117
Naona jinsi wafuasi wa Trump wanavyomuamini humu Trump kila anachosema hata wakati mwengine unajua jambo hilo halingii akilini
 
Naona jinsi wafuasi wa Trump wanavyomuamini humu Trump kila anachosema hata wakati mwengine unajua jambo hilo halingii akilini
Kuamini bila kutanguliza akili ni janga kwa kweli, ndio maana wengine huwa wanageuzwa magaidi pia.
 
1) Wafuasi wa Kibwetere na Matapeli wengine wanaofundisha uongo walishaongelewea tangu karne ya kwanza:

"Maana wakati utakuja watu watakapokataa kuyakubali mafundisho yenye uzima. Badala yake, ili kutimiza tamaa zao wenyewe, watajikusanyia idadi kubwa ya walimu watakaowaambia yale masikio yao yanatamani kusikia.

Watakataa kusikiliza kweli na kuzigeukia hadithi za uongo.

Bali wewe, vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiza wajibu wote wa huduma yako."

2Timothy.4.3-5.NENO


"Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Bwana wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka.

Nao wengi watafuata njia zao potovu, na kwa ajili yao njia ya kweli itatukanwa.

Nao katika tamaa zao mbaya, walimu hawa watajipatia faida kwenu kwa hadithi walizotunga wenyewe. Lakini hukumu imekwisha kutangazwa dhidi yao tangu zamani, wala uangamivu wao haujalala usingizi."

2Petro.2.1-3.NENO

2) Tumepewa muongozo, usipite yaliondikwa!

"Basi ndugu zangu, mambo haya nimeyafanya kwangu binafsi na Apolo kwa faida yenu, ili mweze kujifunza kutoka kwetu maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine."
1Wakorintho.4.6.NENO

Sasa leo tuna walimu wanafundisha mambo kibao very fantastic mtasikiliza story mduwae, wanasema wamefunuliwa na roho mtakatifu.

Huku Kwenye maandiko wanayosema hamna! Atalazimishia andiko liendane na mafundisho yake ukichunguza hata hayaendani! ! Mwishowe anakwambia unasoma maandiko kimazoea, hujafunuliwa na roho mtakatifu! ! !

Aisee Ndugu Watumishi, Mungu wetu si Mungu wa machafuko. Ufunuo mnaopewa huko mkiwa peke yenu haupiti maandiko hadi sisi tuwasikilize. Ni wa kwenu wenyewe!

Ndomana hata kuhusu kunena kwa lugha, mtume Paulo alisema kama hayupo wa kutafsiri unachosema ukae kimya. Tofauti kabisa na mauzauza wanayofanya makanisa flani siku hizi!

"Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu."
1Wakorintho.14.28.NENO

3) MUNGU kaagiza tumpende kwa akili yote, kwa hiyo ukiambiwe ufanye mauzauza kanisani ujiulize hapa ndo akili yangu ilipoishia? ? ?

Kuna video nimeona pastor anaogesha waumini kanisani mbele kabisa wamekaa kwenye beseni uchi kama watoto
:2Head:

Na hakuna sehemu ya kupata maakili mengi mengi kama kwenye BIBLIA.
 
Back
Top Bottom