Hivi Scout ya Simba sc Inawafanya Mashabiki Wa SIMBA SC ni Mambumbu sana

mchawi wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
830
Reaction score
898
Habari Ya Usiku Wana JF hivi Scout Ya simba Sc iliangalia nini zaid kwa huyu FREDI.

HIVI KUNA MTU BADO ANASHAWISHI WATU WAMUELEWE FREDY?

Unaweza kutumia Nguvu nyingi kuwashawishi mashabiki wamuelewe Fredy ili nawewe uonekane unaujua mpira Lakini ikikumbuka magoli ya Medie Kagere,Chriss Mugalu,John Bocco,Moses Phiri na Jean Baleke unaamua kukaa kimya maana kwaambia watu kuwa Fredy ni mtambo wa Magoli ni kuukosea Heshima Mpira wetu AU watu hao unaowaambia wawe hawajawahi kuwaona wakina Kagere,Mugalu, Bocco,Phiri,Jean Baleke otherwise huyu Fredy awe kapigwa Misumari haswa.

Kufunga siyo tatizo haya Yipye alifunga, Michel Sampong pia alifunga lakini viwango vyao vilikuwa chini sana hadi kuvunjiwa mikataba yao.

Fredy Michael ana negativity nyingi sana ndani ya Pitch.kuna mda najiuliza ni kweli Scout aliyeajiriwa na Club ndiye aliona kipaji hiki?

Au coach Benchikha alikubali uwezo wa Huyu mwamba??

Yaani kuna utofauti kati ya Simba iliyokuwa inasajiri bila Scout na hii simba ya sasa inayosajiri kwa kutumia scout..

Ninauhakika Simba hii hivi karibuni kuna mahali wanakwama sana especially in Recruitment of new player [emoji1666]

N:B.Wenye akili ya ziada wananielewa Sana
 
Haihitaji akili ya ziada

Akiwa Green eagles alikuwa anafunga mechi kibao ligi kuu Zambia.

Inawezekana magoli yalikuwa ni ya papatu kama haps anayofunga.

Inatakiwa umuone mchezaji kuwa hata kama ana magoli,huyafungaje?

Hata kama hukosa magoli huyakosaje?

Mwisho wa msimu utasikia "msimu huu bajeti ilikuwa bilioni 15".

Fedha ziheshimiwe
 
Sema wanangu tumepigwa pale, Msimu ujao tusajili vyuma kweli otherwise mtani atatuacha mbali sana
 
Tutafanyaje na ndiyo Mchezaji tuliyeaminishwa kwamba ana uwezo wa kufunga hata akiwa amelipa lango la mpinzani wake mgongo🙌
 
Aliachwa Moses Phiri na Baleke kwa usajili wa Coublan na Jobe 😆😆

Walau Babacar anajitahidi kucheza vizuri pamoja na mapungufu lukuki aliyonayo kwenye nafasi anayocheza
 
Kazi tunayo wana Simba.
 
Nafikiri Simba kwa sasa kinachotuumiza ktk usajili Ni upigaji au ubahili. Scout yupo vizuri isipokuwa kuna hayo mambo mawili
 
Toka medie kagere aondoke,simba haijasajili mshambuliaji aliyemzidi uwezo kagere.japo mpira una changamoto zake ila hiyo scout ya simba kama ipo nikama yenyewe inafanya mambo kwa kurudi nyuma badala yakwenda mbele.
 
Kuna shida mahali heri tungebakiwa na akina phiri, najitahd bas hata kuwa emotional na simba lakn kumtetea coublan inanishinda kwakwel hahaha
 
Itafikia mahali ataondoka mwenyewe.
 
Simba iachane na viongozi wanaosemwa wafia timu. Professionals wapewe nafasi. Imagine timu ipo kwenye uhitaji mkubwa wa strikers wewe unaenda kuleta Freddy anaishia kukenua na kushika kichwa tu.
Ni bora kuwa na wageni wachache lakini viwango hata kama ni ghali kuliko hili lundo lisilo na faida
 
Yaani hata sijui hao scout kama wanafanya kazi yao kwa uhuru bila kuingliwa na watu/mtu

Hivi mtu umesomea kazi yako na unaijua vizuri umeajiriwa kwa ajiri ya hiyo kazi unawezaje kuleta wajinga wajinga kama hao eti ndo washambuliaji,

% ni kubwa kwamba pale kuna ten pasenti

Saidoo
Louis
Jobe
Freddy n.k

Watu kibao wako pale wanakula tu mishahara upuuzi mtupu

Yaani ile simba ndo iende kimataifa
 
Mpira wa Afrika ni dhaifu mno eti hii simba ya fred ipo robo champion ligi
 
Strika hovyo huyo Bora ya Thomas Ulimwengu au Bocco, Fredy Cobra ni kama Chura tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…