Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Hivi jamani hii Serikali ya "Anayeupiga mwingi" haitambui kuwa wananchi wanateseka na hali mbaya ya maisha? mbona hatuoni juhudi za makusudi za kuwapunguzia mzigo mzito wa maisha ikiwemo mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu kama chakula na vifaa vya ujenzi?
Badala ya kuwapunguzia wananchi mzigo mzito bado serikali ya CCM imekomalia kukusanya tozo mbalimbali hata kwa masikini hata kama ilisema imepunguza lakini hizo tozo hazimsaidii chochote mwananchi wa kawaida zaidi ya kumuongezea makali ya maisha.
Cha ajabu sasa pamoja na wingi wa matozo ya ajabu ajabu bado serikali yetu inazidi kukopa kila kukicha na fedha zinaenda maeneo ambayo hayana msaada wa moja kwa moja kwa wananchi. Ifike mahali serikali ifute tozo zote ikiwa ni mpango wa kupunguza ugumu wa maisha. Ikumbukwe tayari serikali imeacha kuweka ruzuku ya mafuta na hivyo kufanya bei za mafuta kuendelea kuwa juu.
Serikali iwaonee huruma wananchi wake wanateseka sana huku mataani.