Kudoba wepo baaah
Senior Member
- May 12, 2024
- 155
- 461
Mwalimu mkuu/Mkuu wa shule anaingiziwa hela kwenye akaunti ya shule. Anaandikiwa barua ya kukaimishwa uafisa masuhuli na mkurugenzi ili asimamie kikamilifu fedha hizo zifanye kazi lengwa. Mpaka hapa, safi tu.
Anatakiwa aunde kamati mbalimbali zinazoshirikisha walimu wenzake, watendaji wa serikali, na wanakijiji ili washirikiane kusimamia mradi. Mpaka hapo, safi tu.
Linapoanza tatizo:
Fundi anatafutwa na ununuzi huku mwalimu akiambiwa tu, "Fundi wako huyu hapa na atajenga kwa kiasi hiki!" Kwisha!
Baadae tena anaitwa tu na kuambiwa vifaa utanunua kutoka kwa mzabuni fulani. Kwisha!
Vifaa vyote (materials) vinavyohitajika katika ujenzi husika lazima viingizwe kwenye mfumo wa NEST. Hii inahusisha mpaka maji, kokoto, mawe, mchanga n.k. Hapa kuna shida, na shida yenyewe ni kwamba gharama itakuwa kubwa mno kwani hata vitu ambavyo shule au kijiji kilikuwa na uwezo wa kuvipata kwa urahisi sasa mzabuni atapiga anavyotaka.
Mwishowe, mradi usipokamilika basi mwalimu ndiye atakayewajibishwa.
Au mimi sijaelewa wadau?