Hivi serikali ya Tanzania inakusanya kiasi gani kutoka Zanzibar?

Hivi serikali ya Tanzania inakusanya kiasi gani kutoka Zanzibar?

Thailand

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2019
Posts
275
Reaction score
795
Mara zote nimekuwa nikisia pesa inatoka Tanganyika kwenda Zanzibar. Mfano soma nukuu hii kutoka kwa rais wa JMT;

”Kwa mfano mwezi huu kulikuwa na vimaneno sijui hakuna pesa serikalini pesa kwasababu mikopo tulikopa imechelewa ya kufanyia kazi hizi lakini mbili kuna mikopo iliyo ‘mature’ kwa pamoja miwili na imebidi yote tulipe lakini kuna certificate za miradi mikubwa ambayo imekuja imebidi tulipe kwahiyo kwa kuweka heshima za nchi yetu lazima tulipe mikopo.”

Hapo serikali inadai mikopo miwili ili mature hivyo ikabidi ilipwe kwa pamoja. Tunajua kwamba mikopo tunayokopa kutoka nje tunagawana na SMZ. sasa kwenye kulipa naomba nipate ufafanuzi kama kuna pesa ilitoka Zanzibar kwa ajili ya kulipa mikopo hiyo.

Madhara ya mikopo

Kwa mfano kwa kitendo cha ku declare kwa serikali haina ela kisa kulipa mikopo hii ni hatari kwa ustawi na uchumi wa wananchi kwa sababu mradi au malipo halali yaliyo paswa kwenda kwa wananchi inabidi yasimamishwe ili ku clear madeni. Sasa hapo panaitaji nyuzi nyingine kufafanua madhala ya mikopo hasa inayowafaidisha wachache kama ilivyo huko kwenye jamhuri ya kusadikika.

Turudi kwenye mada Zanzibar alichangia kiasi gani kwenye mikopo iliyolipwa mwezi dec kwa mujibu wa kauri ya rais. Isije kuwa hawa wazanzibar tunawanufaisha kwa kufanya kitu kinaitwa UPENDO WA MSHUMAA halafu wao hawana shukrani.
 
ngoja nisubscribe kabisa nielimike maana si wengine tukihoji tunaonekana tunauchukia Muungano
 
Kinachokusanywa Zanzibar kinatumika Zanzibar, Kinachokusanywa bara, ni cha wote
 
Serikali moja ndo dawa ya huu muungano
 
Back
Top Bottom