Hizi sarafu sh 5, 10 na 20, ( pia sh 50) zinapoteza thamani kwa sababu in one way or other mamlaka za kusimamia bei za bidhaa hazitimizi wajibu.
Wafanyabiashara wanajipangia bei watakavyo na raia wakilalamika hakuna mamlaka inayochukua hatua! Mfano ni hivi, bidhaa inayotakiwa kuuzwa kihalali Tsh 40, muuzaji atalazimisha iwe sh 50 ili asisumbuke kurudisha chenji ya sh 10 (ambapo sarafu za sh 10 zinapatikana bank ila wauzaji wa retail hawapendi kwenda kuziomba kwa hiyo zinaadimika mtaani)
Kadhalika nauli ya daladala halali ikiwa sh 450, kondakta atalazimisha iwe Tsh 500 kwa kisingizio cha kukosa change!
Hivi sasa, bidhaa ya sh 900, usishangae ukalazimishwa kulipa 1000! Au ile ya 1400 ukalazimika kulipa 1500! Kisingizio sh 100 ya kukurudishia hamna. Na kwa kuwa waTz ni wapole sana basi very soon itakuwa ni kawaida, na hatimaye sarafu za 100 nazo zitaadimika kama zile za 5, 10, 20, (na 50 baadhi ya maeneo)