Hivi shule za private kumbe ni wagumu unapotaka kuhamisha mwanao

Hivi shule za private kumbe ni wagumu unapotaka kuhamisha mwanao

GIAN JUNIOR

New Member
Joined
Mar 9, 2011
Posts
2
Reaction score
0
Wakuu habari.
Mwanangu ameingia class 4 mwaka huu. Ila shule aliyopo imekuwa na mwenendo mbaya, kiasi kwamba kwa mwaka 2023 na 2024 wazazi wanaojitambua wamehamisha sana watoto wao. Sasa huyu wa kwangu kila mara yeye huchukua namba 1 darasani.

Ila tangu tulivyoanza mwaka 2024 nikawa na mawazo ya kumuhamisha maana mtoto mwenyewe hataki kuendelea pale, sababu kubwa ilikuwa walimu wanaondoka mara kwa mara. Wakati tunaendelea kutafakari kuna mwalimu rafiki sana wa mrs wangu, akaja akamshauri kuwa kama tunamjali huyo mtoto basi tumtafutie shule nyingine.

Na sisi pia tukamwambia tulishaamua kufanya hivyo. Kwa hiyo mwezi wa 9 mwaka jana tukaanza rasmi mchakato. Mimi nilikuwa na safari ya nje ya nchi so nikamwachia majukumu wife aendelee kufuatilia uhamisho. niliporudi nikakuta kweli amefanya mchakato, amejaziwa kadi ya maendeleoila haikuwa na prem number. Mkuu akawa ameahidi atashughulikia kuhamisha kwenye mfumo sisi tuwe na amani.

Mwezi october ukaisha mtoto hajahamishwa, November nikafuatilia mimi mwenyewe, aisee nilijibizana vibaya sana na mkuu. Kwanza mkuu niliyemkuta siye aliyekuwepo September, yule wa kwanza kashasepa. na huyu niliyemkuta anasema utaratibu wa shule ni kwamba wanahamisha December. Nikambana maswali hadi ikawa kero akanikimbia ofisini akajifanya ameitwa na Director.

Mimi nikakomaa, akarudi kama baada ya nusu saa jamaa hadi akawa anatetemeka. Baada ya majibizano mengi nikaondoka kwa hasira nikaenda manispaa, nikamvaa afisa elimu. Nikamwelezea story yote. Akasema ngoja ampigie, ikawa hapokei simu ya afisa elimu.

Afisa elimu akaniambia nisijali, wao wana direct access ya kuhamisha kipindi cha kufungua shule January. Mawazo ya Afisa elimu ni kwamba huyo mkuu hataki kumhamisha mwanao kwa sababu ameshaona ana akili sana, kwamba angekuwa mtoto kilaza angemhamisha fasta.

Jana nikamtafuta afisa elimu kumwomba aingie kwenye mfumo kuangalia kama mkuu ameshamhamisha, jibu likaja bado mtoto hajahamishwa. Kumbuka mtoto yuko shule nyingine tayari, ila kwenye mfumo bado.

Hivi kisheria hii issue imekaaje, hivi haiweekani nikamshitaki mkuu wa shule kwa usumbufu anaonifanyia? Afisa elimu amenihakikishia kuwa very soon, watakuwa na access ya wao kuhamisha juu kwa juu kwenye mfumo. Ila nawaza, je asipofanya hivyo inakuwaje?

Si Mtoto atalazimika kurudi shule ambayo ameshahama? Alafu kuna mtu aliwahi kuniambia hao wakuu wa shule sometimes wanafanya lobbying na afisa elimu. Ikitokea afisa elimu hajamuhamisha mtoto nifanyeje kisheria?
 
Tuliza boli mzazi. Lazima watamhamisha tu kama umewalipa ada.

ikifika jtatu hawajahamisha umkunbushe afisa elimu tena.
 
Back
Top Bottom