Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 72
- 261
Hivi huwa ni uwezo wenu au Kuna la ziada??
Nimewaangalia mechi yenu ya juzi,
mkapata goli dakika ya 93, yaani mlishinda kama ajali tu, au kwa bahati mbaya, hamkucheza Mpira wowote wa maana zaidi ya bora liende.
Leo Mchezo wenu huu na wana usalama wetu, inanidhihirishia hii ndio tamati ya uwezo wenu, wala sitanii!
Mmecheza Mpira Mbovu, hamkufungwa kwa sababu wanausalama wenyewe hawakuwa makini golini kwenu.
Hii inanizidishia mashaka niliyonayo juu ya matokeo yenu na timu za nje na hasa mkiwa uwanja wa nyumbani.
Wachezaji ni hao hao, makocha ni hao hao, viongozi na mashabiki ni hao hao.
Kwani Kuna lipi la ziada wenzetu huwa mnafanya nje ya misingi ya Soka kinachowafanya wageni kila siku kuchoka kipindi cha pili?
Unajua mimi nilidhani hizi mechi za nyumbani ndo zingethibitisha uwezo wenu unaosemwa kimataifa, lakini dah, najionea mangolibo tu.
Najua badala ya kutafakari na kujitathmini mtalipuka kujibu kwa ghadhabu, lakini hapana, nina haki ya kueleza mashaka yangu, Kuna kitu hakiko sawa, kuna kitu kinaendelea na ninaamini wakati utaongea punde!
Msije kunijibu kwa mifano ya Timu zingine kubwa, Timu kubwa zinafungwa na zinatoka sare ndio soka, lakini wanakuonesha Ukubwa wao bhana!
Arsenal Jana kafungwa lakini unaona namna wanavyopambana, unauona Ukubwa wao na mwisho wa siku unasema kweli kuna bahati mbaya kwenye soka.
Anyways, acha tusubiri tuone, yetu macho