Hivi Simba SC tutawahi tena kuja kuwa na Kikosi imara na cha kukumbukwa kama hiki?

Lakini vipi kile kikosi kilichofika fainali za kombe la shirikisho kilichokuwa chini ya king Kibadeni Mputa mwenye kukikumbuka atukumbushe wadau.
Mi nyagi imeshafuta kila kitu kichwani. Hakuna siku Simba iliniumiza kama ile. Yule jamaa anaitwa Boli Zozo... mi namwachia Mungu aseme naye mwenyewe
 
Omar mahadh
Kajole
Shaban baraza
Daud salim
Aluu Alli
Umar Gumbo
Khaidar
Athuman Mambosasa
King Kibaden
Ezekiel G Jujuman
Abbas Dilunga
Malota soma
Abdallah Mwinyimkuu
hebu endeleza

Wengi wetu humu JF katika Kikosi hiki ulichokitaja hapa tulikuwa katika ' Mabeseni ' tunapiga piga tu maji tukisubiri ' Kuogeshwa ' na kwenda kunyweshwa ' Uji ' wa ' Buruga '.
 
Wengi wetu humu JF katika Kikosi hiki ulichokitaja hapa tulikuwa katika ' Mabeseni ' tunapiga piga tu maji tukisubiri ' Kuogeshwa ' na kwenda kunyweshwa ' Uji ' wa ' Buruga '.
Samahani nimewakwaza....lakini weka historia.Wengine tulikua Form two huko Ilboru secondary....na ilikuwa Ilboru kweli kweli ya kina Tundu Lissu cha mtoto
 
5. Victor Costa "Nyumba"
 
Simba mlikuwa vizuri sana lakini umemsahau Victor Costa "Na mpoka Nyumba "
 
Samahani nimewakwaza....lakini weka historia.Wengine tulikua Form two huko Ilboru secondary....na ilikuwa Ilboru kweli kweli ya kina Tundu Lissu cha mtoto

Mkuu hapa katika huu ' uzi ' hatuongelei ' Ilboru ' ya kweli kweli ukitaka kumaanisha kuwa ' Ilboru ' ndiyo ilikuwa Shule pekee hapa Tanzania ambayo ilikuwa na Wanafunzi ' Werevu '. Acha ' Sifa ' za Kijinga na akili ya Mwanafunzi au Mtu haipimwi na Shule aliyosoma bali kuna ' Factors ' nyingi za kuonyesha kuwa Mwanafunzi au Mtu fulani ni ' Mwerevu '. Please next time use common sense.
 
Thank you.....sikutaja elimu...anyway nilikuwa namanisha Baridi ya pale shule.Samahani saana hatukuelewana.....ninakuomba radhi na msamaha wa dhati.
Imani yangu na pia za wengine zinatutaka kuombana msamaha pale tunapokoseana.
Narudia tena kuomba msamaha nilipokukwaza na waungwana hawaoni shida kuomba msamaha au kusamehe pindi mtu anapoomba.
 
Miaka hiyo nilikuw bado mdogo sana ndio nilikuwa naanza kufatilia mpira
Kumbukumbu zangu hazijakaa sawa,kikosi hicho Machupa hakuwepo?

Katika mechi nnnazokimbuka ilikuwa Kagame Cup...tulifungwa goli dakik za nyiongeza zikiwa zimebaki dakika chache ulipigwa mpira mwingi tukachomoa goli kwenye penalt tukawatoa kama sikosei walikuwa Tusker

Simba ilikuwa tishio ukanda huu wa East and Central,kikombe cha Tusker ilichukua mara 5 mfululizo
 
Hiki ndo kilikuwa kikosi imara cha Simba
 
Quresh Ufunguo, alikuwa sub kwenye kikosi kipi?

Sent from my Fero A4001 using JamiiForums mobile app
 
Ah
Salvatory Edward, waziri mahadhi ,sekilojo chambua ,Fred Mbuna,iddi moshi ,

Kiboko ya simba hiyo
 
Sio tusker ni sports club villa ya uganda...

Sent from my TECNO_P5_PLUS using JamiiForums mobile app
 

Dah, we jamaa mbona una roho mbaya hivi? Kulikuwa na umuhimu gani waturudisha kumbukumbu mubashara kama hizi wakati sasa hivi tunao akina Mavugo huku tukimtegemea "reject" Okwi?

Inauma sana mkuu, kutukumbusha wakati mtu unaenda uwanjani huku mkibisha idadi ya magoli ya kushinda, sio kushinda au kufungwa.

Damn u GENTAMYCINE kuniharibia siku ya leo. Dah haya bana.
 
Wakati huo kocha kipenzi cha mashabiki marehemu Aggrey Siang'a alikuwa anataja first eleven siku moja kabla ya mechi, wakati makocha wengine kwa kuendekeza imani za kishirikina ilikuwa ni mwiko kutangaza kikosi. Yeye alikuwa anatangaza na anazaba wapinzani bao za kutosha tu na mpira mwingi. Kweli vizuri havidumu
 
Hebu fikiria hawa wakiwa uwanjani, wenye benchi amekaa Stephen Mapunda 'Garincha', Athuman Machupa,, Amri Said, Kelvin Mhagama, Madaraka Suleiman, Victor Costa 'Nyumba', n.k

Kuna kipindi mpira umewahi kuchezwa hapa Tanzania, sasa hivi niungane na yule mdau anayesema hatuchezi mpira tena ila kabumbu
 
amna tena licha ya kwamba mie siyo shabiki wa tim za tz.kwan zilishanikatishaga tamaa.ila kwa kikos hcho ulicho kitaja walau kwa mbali nilikuwa najitokezaga kuangalia game zao.umenifanya nikumbuke mbali brodaa!.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
mkuu hapo ndipo palikuwa na mpira.siyo hvi vibana pua wa ss waenda onyesha stail za minywele tu uwanjani.

Sent from my TECNO-N8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…