Hivi soka la Ulaya limebadilika tofauti na zamani?

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Habari za masiku waungwana katika medali ya soka. Kwa ambaye amefuatilia michuano ya Uefa msimu huu atakuwa kanote kitu, mpira wa ulaya umekuwa sio kama kipindi cha zamani ambapo timu zilikuwa zinategemea matokeo zaidi inapokuwa nyumbani. Lakini tokea UEFA wafute mfumo goal la away na kuja na mfumo wa aggregate naona mpira umekuwa na matokeo yakushangaza, timu zinanyukiwa huko huko majumbani kwao

Tukio la kwanza nakumbuka kwenye group stage game ya Atalanta dhidi ya Villareal. Hii game Atalanta walikuwa wanahitaji ushindi wa magoli yoyote yale ili afuzu na walikuwa wapo nyumbani, lakini walikumbwa na msiba mzito kutoka Villareal walilambwa magoli matatu na kutolewa. Mechi nyingine inayofanana na scenario kama hiyo ni ya Wolfsburg vs lile na porto dhidi ya Atletico Madrid.

Mechi ya hatua ya mtoano kati ya Juventus vs Villareal.
Kwa hali ya kizamani kitendo cha juve kupata sare ya 1-1 away ilikuwa mechi imeisha hiyo kwa juve kupita kwavile anamaliza home. Ila Juve kachezea goli tatu kwa buyu huko huko kwao .
Mechi ya Ajax vs Benfica hivyo hivyo

Liverpool vs Intermilan, chelsea vs real Madrid hizi mechi timu zilibadilisha tu viwanja vya kushindia kila mmoja katamba nyumbani kwa mwenzie. Japo kwa Madrid ilikuwa almanusura kuaga.
Liverpool vs Benfica kila mmoja alitegemea mechi ya marudiano ingekuwa nyepese kwa Liver ila hali ilikuwa tofauti nyumbani.

Bayern Munich vs Villareal hapa kwa hali ya kizamani, ni kwamba kushinda home kwa ushindi mwembamba hivyo tena dhidi ya Munich basi uhesabie kupigwa mengi, lakini Bayern wanaagia hapo hapo kwao

Atalanta vs Leipzig na Barcelona vs Frankfurt walipata matokeo mazuri sana ya sare sare walipokuwa ugenini lakini wamekutana na vipigo vitakatifu nyumbani mwao kwenye marudiano.

Hapo nimejaribu kuchukua timu maarufu ambazo zimepata shida majumbani kwao tofauti na misimu ya nyuma ambapo unajua kabisa timu ilifungwa away inaenda kufanya come back ya hatari home. Na timu ikizingua first leg home kwake basi huyo hana chake tena ataenda kupigwa tena second leg.
 
Hua huangalii mpira wewe
Nyie ndo inaonesha hamuangalii
 
Mi nadhani, timu nyingi viwango vyao vimeongezeka. hakuna timu dhaifu, timu iliyoitoa barcelona iko nafasi ya 9 Ujerumani. Mpira umebadilika.
 
Siku hizi wale super powers wa sokanla Ulaya wamekuwa mdebwedo, timu karibu nyingi viwango vinalingana...
 
Sheria ya away goal ilifanya timu zikiwa nyumbani ziwe zinashambulia kwa tahadhari na kukaba sana kuzuia mgeni asipate goli..
Walipotoa huo mfumo watu wanacheza mpira bila tahadhari (tension) ya away goal
 
Goal la ugenini arsenal Wenger alikuwa analalamikia toka zamani hyo sheria maana lengo lilikuwa team zinatoka mbali na zinakuwa na uchovu ila sasa hivi hali ya usafiri imebadilika team zinatumia mda mchache kwenda kwa mwenyeji wake hvyo kwa sasa kuendelea na sheria,

hyo ni kama upendeleo kwa mgeni kitu kingine team zilikuwa zikipata matokeo zina paki bus hazichezi mpira kwa hyo kuna kuwa hakuna ushindani mzee Wenger ana mchango wake katika hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…