Hivi South Africa ina wanamuziki ama wapiga beat?

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Mi naona muziki wao unaendeshwa na beat zaidi ndio maana unafanywa sana na madj na producers, na sijui kwanini ni nadra kuona wimbo unafanywa na mtu mmoja, ni lazima wajikusanye kuanzia watatu na kuendelea.

Wasanii wakubwa wenye nguvu ni wachache sana, sio kama Nigeria ambapo majina ya wasanii ni makubwa yakiendana na ukubwa wa muziki wao.

Muziki wao 'Amapiano' umekamata sana Africa kwasasa, cha ajabu majina ya wasanii wao sio makubwa kihivo
 
Amapiano zenyewe kutoka SA zina maneno machache,ila mdundo ndio unatawala kuliko mashairi na mashairi yake yako simple ,mafupi then vionjo na zile style za kucheza zinatawala.

Ila siku hizi kuna wimbi la wasanii wa Nigeria wanatumia bits Amapiano na wamefanikiwa kutoa hits zinazofanya vizuri kuliko wasouth wenyewe hata style za kucheza Naija washaanza kukopi kutoka SA.

Monalisa.
Sungba.
Who is your guy.
Ijo.

Hizo ni hits za Nigeria zilizo tumia Amapiano na bado kuna nyimbo nyingi zinachiwa zina tumia beat za Amapiano.Mimi mwenyewe sijajua kwa nini kwani midundo ya Amapiano asili yake SA ila Wanaija wanajua kutembea nazo na kuwaletea mafanikio.
 
Nadhani wasouth inabidi wabadilike, wao wanawekeza zaidi kwenye beat na vionjo, mashairi kwao sio kipaumbele. Hii inafanya waonekane zaidi kama beat makers kuliko wanamuziki, Asake katengeneza hits kubwa kupitia beat zao. Wao na muziki wao sidhani kama wamewahi toa hit kubwa kama 'You want to bamba'. Hata watanzania tunaweza kupita na beat zao vizuri kuliko wao wenyewe[emoji16], Refer; Marioo
 
Kuna msanii na mwanamuziki,

Wasanii wapo wengi kuliko wanamuziki...

Mwanamuziki anaweza kupiga life Band ila msanii hawezi kupiga live band

nikosoe panapo faa.....
Naomba uhusianishe na mada, sijakumanya
 
Mi naona muziki wao unaendeshwa na beat zaidi ndio maana unafanywa sana na madj na producers, na sijui kwanini ni nadra kuona wimbo unafanywa na mtu mmoja, ni lazima wajikusanye kuanzia watatu na kuendelea. Wasanii wakubwa wenye nguvu ni wachache sana, sio kama Nigeria ambapo majina ya wasanii ni makubwa yakiendana na ukubwa wa muziki wao. Muziki wao 'Amapiano' umekamata sana Africa kwasasa, cha ajabu majina ya wasanii wao sio makubwa kihivo
Walikuwa wanajitafuta sasa wamejipata

Imeanza kwenye kwaito na ni mlakati wao ndio wameweka hivyo....

DJ tira au Mapholisa walianza kitambo ila cheki kwaito ilivyowabana wakaenda nayo huku wanajitafuta na sasa Amapiano ndio new school yao

Hapa mafik zolo hawawezi ingia sababu wamejisahau kwenye hili tobo.
 
Inaonesha Dj Maphorisa ana mchango mkubwa sana kwenye muziki wao, japo Kabza DE Small anatajwa kama muanzilishi wa Amapiano, naye ni dj na sio mwanamuziki. BTW unadhani ni kwanini Amapiano yao haiimbwi na artist mmoja, ni lazima wawe walau watu watatu na pengine walioshirikishwa unaweza usione mchango wao wa maana kwenye wimbo?!
 
Bit zao lazima iwe hivyo ili mziki wa amapiano ukamilike mbali na hapo asee utaskiliza mwenyewe geto.....

Ndio mana hata Casper Nyovest nae anaingiaga huko
 
Kwa huu upepo lazima tu aingie
 
Mi naona muziki wao unaendeshwa na beat zaidi ndio maana unafanywa sana na madj na producers, na sijui kwanini ni nadra kuona wimbo unafanywa na mtu mmoja, ni lazima wajikusanye kuanzia watatu na kuendelea.

Wasanii wakubwa wenye nguvu ni wachache sana, sio kama Nigeria ambapo majina ya wasanii ni makubwa yakiendana na ukubwa wa muziki wao.

Muziki wao 'Amapiano' umekamata sana Africa kwasasa, cha ajabu majina ya wasanii wao sio makubwa kihivo

Shida yako nn? Kwani mzik wa sasa ni beat tu? Au beat na Mwanaza nyegezi, bora ujumbe wa mwanza nyegezi?
 
Repetition ( word) - Melody-Beat.
Chukua kipande cha audio kipige loop play utaona kinaleta kitu kama mziki.
Repetition na varieties ndio humkamata mtu kichwa yake mana watu Hu ignore kitu walichokuwa familiar nacho.. So varieties hufifisha akili yako kutohama.

EDM za kina Alan walker, Madeon na wengine ni km ama piano.
 
Hiyo ndio style ya muziki wao, kila mtu ashike style yake. Km style yenu mashairi mengi beat kidgo sawa kila mtu akae kwake tusiigane
Haya mambo ya kitaalam tuache kidogo, wewe subiria Sridi ya kina Juma Lokole na Hakika Reuben
 
Back
Top Bottom