Hivi South Africa ina wanamuziki ama wapiga beat?

Mi naona muziki wao unaendeshwa na beat zaidi ndio maana unafanywa sana na madj na producers, na sijui kwanini ni nadra kuona wimbo unafanywa na mtu mmoja, ni lazima wajikusanye kuanzia watatu na kuendelea.

Wasanii wakubwa wenye nguvu ni wachache sana, sio kama Nigeria ambapo majina ya wasanii ni makubwa yakiendana na ukubwa wa muziki wao.

Muziki wao 'Amapiano' umekamata sana Africa kwasasa, cha ajabu majina ya wasanii wao sio makubwa kihivo
Amaliano ni staili ya muziki iliyozuka ikabamba, kama singeli huku kwetu, ila wapo wanamuziki wenye nyumbo zenye mashairi tofauti na Amapiano...ni vile tu huku kwetu nyimbo zao siku hizi hazitufikii, ila ukitafuta kupitia mtandao utazipata!
 
Walikuwa wanajitafuta sasa wamejipata

Imeanza kwenye kwaito na ni mlakati wao ndio wameweka hivyo....

DJ tira au Mapholisa walianza kitambo ila cheki kwaito ilivyowabana wakaenda nayo huku wanajitafuta na sasa Amapiano ndio new school yao

Hapa mafik zolo hawawezi ingia sababu wamejisahau kwenye hili tobo.
Hizo ni style ambazo zinaibuka na zingine zinadumu zingine zinapita na muda kama ilivyokuwa Kongo na style zao za Ndombolo, Kwasakwasa, kibindankoi n.k

Lakini kwa miaka yote, bado beat nzito inabeba muziki wao, hata kwa nyimbo za taratibu utaona zimeshiba beat, ndio style ya muziki wao.....
 
Je kwanini unafanywa na djs sanasana?
 
Mi napenda wanavyocheza aise cheza ya waafrika inavutia sana,mmeona video mpya ya costa titch na Akon?
 
Amapiano ni muziki tu unaotrend lakini haimaanishi hawana solo artists au genre zinafanya vizuri zaidi mfano kwenye kwaya SA haina mpinzani ndio maana Kwaya kama Soweto zina grammy

Kuna wasanii kama Zahra, Loyiso na marehemu thami tebede ambao ukisikia nyimbo zao kwa vocals, mashairi na hata melodies unaona kabsaa, kuna vitu unakosa ukisubiria mainstream
 
Amaliano ni staili ya muziki iliyozuka ikabamba, kama singeli huku kwetu, ila wapo wanamuziki wenye nyumbo zenye mashairi tofauti na Amapiano...ni vile tu huku kwetu nyimbo zao siku hizi hazitufikii, ila ukitafuta kupitia mtandao utazipata!
Kabisa mkuu.. Ni nyimbo chache za SA zinakuwa hits ndio maana wimbo kama I love you ya thami. Imehit bongo wakati jamaa alishafariki almost mwaka

Na hata Nigeria, watu kama Asa au chike ambao ni pure singers hawapati mafanikio makubwa kama wenzao wa afro beats..
 
Amapiano ni muziki tu unaotrend lakini haimaanishi hawana solo artists au genre zinafanya vizuri zaidi mfano kwenye kwaya SA haina mpinzani ndio maana Kwaya kama Soweto zina grammy

Kuna wasanii kama Zahra, Loyiso na marehemu thami tebede ambao ukisikia nyimbo zao kwa vocals, mashairi na hata melodies unaona kabsaa, kuna vitu unakosa ukisubiria mainstream
Duh, but kila msanii anandoto ya kuwa mainstream
 
Kabisa mkuu.. Ni nyimbo chache za SA zinakuwa hits ndio maana wimbo kama I love you ya thami. Imehit bongo wakati jamaa alishafariki almost mwaka

Na hata Nigeria, watu kama Asa au chike ambao ni pure singers hawapati mafanikio makubwa kama wenzao wa afro beats..
Enzi hizo kwaito wakina Mafikizolo walikuwa na hits. Watu wengi wanaiga muziki wao na kupata mafanikio na umaarufu mkubwa hasa wanaija, ila wao na muziki wao wanabakia kuwa wa kawaida. Mfano huyo Black Coffee anayeonekana ana mafanikio je ni dj/mwanamuziki/producer? [emoji56]. Na je kwa miaka ya hivi karibuni let's say miaka 10 iliyopita wameshawahi fanikiwa kupata msanii mkubwa anayeweza kupiga show Africa nzima akaeleweka kama ilivyo kwa wanaija?
 
Sijaelewa lengo lako unapouliza kwa nini unapigwa na Ma DJ, kama vile ni kosa kupigwa na Madj kama wakina Black Coffee... ni aina ya muziki ulivyo, lakini bado hautafsiri muziki wa SA japo unatokea huko. Huwezi kusema huo ndio muziki wa SA, nilikuambia mwanzo kuwa hiyo ni style tu imekuja na upepo wa wakati. Wewe unaongelea amapiano kama ndio style kuu ya muziki wa SA. Chukulia tu kama singeli hapa bongo.

Sasa kwa nini wanaija wanatamba zaidi kuliko wao, tujiulize kwa nini wanaija wanatamba kuliko sisi. Sababu ni zilezile, ila tu nitakuambia Muziki wa SA haujashuka, uko palepale, wanaija hawakuwa katika level waliyopo sasa ndio maana unaona kama wa SA wameshuka, hapana. Na utasikia wengine wakifanya muziki.wa SA ila hutasikia wa SA wakifanya muziki kutoka kwingine.
 
Sio kosa, ila nnapatwa na shauku la kujua kwanini madj ndio wanaufanya na sio wanamuziki kama huku kwetu ama kwingineko kama Naija, yaani tafsiri yao ni kama Amapiano kwao sio wimbo kamili bali ni beat na vionjo
 
Back
Top Bottom