Hivi Spika Ndugai ameokoka siku hizi?

Hivi Spika Ndugai ameokoka siku hizi?

Nionyeshe mwanaume anaetembea akiburuza miguu na kichwani akawa 'smart' nami nitakuonyesha dereva wa lory la masafa mwenye mke mmoja.
 
Nchi ni yetu sote,tuipende kwa dhati wacha tukope na kulipa ni lazima kwa maendeleo yetu.Tabu ni pale wahuni wakitafuna mkopo!
 
Huruma ya mzazi ndo imemponza,sisi wapiga kelele tulimuonya mapema mwanzo tukimtakia mema,wasio watoto wako fukuza nadhani ameelewa sasa.


Kwa mtazamo wako huu…shamba angetakiwa kuachiwa mlinzi alilinde mpaka hapo bwana shamba mpya atakapopatikana…
 
Hivi nyie waswahili mnajadili utumbo mtupu humu ndani, mnafikiri hayo madeni atalipa nani? Hata kama unapewa vihela kutukana watu humu ujue hukujizaa ndugu zako including waliokuzaa watatoa jasho la damu kulipa! Mtu anakupa sh.1 ulipe baada ya miaka 20 sh.7 hiyo ni akili/ matope? Mnafikiri mtaendelea kwa kukopa?
 
Maslai ya mswahili yanapokoma akili urudi toka likizo.
Yule aliyepita aliwatuza Sana waimba kwaya.
Ilikuhitaji dakika 5 kuimba kwaya kesho asubui umeletewa v8 na barua ya uteuzi.
Chawa wameyakosa haya ndo chanzo cha makelele,mara wahuni,mara kukopa,mara sijui amaleki,nk.
kweli kabisa,asante mtu wa Mungu.
 
Hivi Ndugai si anaweza kuitisha kura ya kutokuwa na imani na Rais kisha Rais akang'oka?

Wajuvi njoo mtusaidie sisi Su-****-gang
 
Afukuzwe unachama aone kama ataendelea kuwa spika
 
Mheshimiwa Job Ndugai, umekuwa ukihaha sana kwa siku za hivi karibuni kikosoa serikali kwa Mambo menngi. Kimsingi serikali sio Mungu na huwa inakosea sana. Japo pia makosa mengi ya serikali zetu yalitokana na udhaifu na Unafiki wa Bunge ambalo wewe umekuwa sehemu ya uongozi wake kwa muda mrefu.

Ndio maana uliwahi hata kujishangaa mwenyewe ulipong'aka na kuhoji Bungeni kuwa "HIVI KWELI SHERIA HII TULIIPITISHA SISI HUMU BUNGENI"?

Lakini usisahau kuwa wale waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa na kuikumbusha serikali wajibu wake walichukiwa na kupigwa vita na cha ajabu na wewe Ndg Ndugai ukaungana kuwapiga vita kwa namna namna.

Leo unahitahidi kuwa Kiongozi wa mhimili na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa dhambi uliyoiunga mkono na kuishiriki kwa gharama zote na rasilimali za Bunge.

Wewe sio mwana CCM kuliko Hayati Mwalimu Nyerere, Lakini Mwalimu Nyerere aliona wazi bila Upinzani Nchi hii ingeenda kusiko, akasimama kidete kuunga mfumo wa vyama vyingi Nchini.

Kila serikali huja na maono yake pamojana kubeba mizigo na madudu ya watangulizi wake. Muache Mheshimiwa Samia atekeleze aliyokusudia na wakati ndio utamhukumu sio Bunge dhaifu.
Mimi siitaji stress
 
Back
Top Bottom