Adui wa Uonevu
New Member
- Jun 30, 2026
- 3
- 1
Kuna mambo yanaendelea chuoni hapo mpaka unajiuliza, hiki chuo kina wenyewe kweli? Na wanafunzi wamekaa kimya, mpaka unajiuliza tunazalisha wasomi wa namna gani?
Jumanne tarehe 30 June, wamefanya Uchaguzi wa Rais ukitanguliwa na uchaguzi wa wawakilishi wa "faculties" pamoja na madarasa.
Uchaguzi umefanyika kwa njia ya mtandao (yaani electronic -voting) sasa ajabu ni kwamba;
1. Katiba yao ambayo imesajiliwa ambayo kimsingi ndiyo yenye nguvu ya kisheria ya mwaka 2012 haielezi juu ya mtindo huo wa kieletroniki kwenye uchaguzi mkuu, Menejimenti, na Wanafunzi wote wapo kimya. Mfumo ambao hata udhibiti wake haupo vizuri, wanafunzi wanalalamika kupigiwa kura kwenye akaunti zao, na uongozi wa chuo upo kimya tu.
2. Upatikanani wa wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ni vichekesho, wanapatikana kwa kupigiwa simu na Dean of Students.
3. Katiba iliwataka wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wakutane kwa wiki moja kabla ya zoezi la uteuzi wa majina ya wagombea, wao wamekutana mara moja tu, kwa saa chache na wameanza mchakato siku hiyohiyo, na hakuna aliyehoji.
4. Huko ndani ya Tume ya Uchaguzi unaambiwa ni Mwenyekiti wa Tume na Dean of Students ndio waliohesabu na kujumlisha matokeo ya watia ya Urais, wajumbe wengine wa Tume ya Uchaguzi wamefaya kusomewa tu matokeo kama wanafunzi wengine.
5. Kuna mtia nia mmoja wa nafasi ya Urais aliambiwa kabisa na Dean of Students kwamba "Menejimenti ya chuo inataka Rais atoke katika fani ya Uuguzi(SONU) na kweli bhana ameshinda. Yaani Menejimenti inakaa na kuwachagulia wanafunzi kiongozi wao!!??
6. Pamoja na kwamba Dean of Students amelalamikiwa sana na wanafunzi kuvuruga na kujinufaisha na fedha za wanafunzi, Menejimenti imekaa kimya wala haioni tatizo. Katika Bunge lililoisha muda wake, Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi aligomea kusoma taarifa na ripoti ya Uongozi unaomaliza muda wake akiamini haikuwa sawa, kuna upigaji mkubwa sana, na watia sahihi ni pamoja na Dean of Students, yaani chuo kimekuwa kama shamba la Bibi.
7. Kama kuna chuo cha ovyo Tanzania na hasa kuhusu Utawala, St. John's University of Tanzania ndio mwalimu wao.