Hivi stendi ya daladala Sabasaba Dodoma wameshindwa kuwatenganisha wauza bidhaa za sokoni na parking za daladala?

Hivi stendi ya daladala Sabasaba Dodoma wameshindwa kuwatenganisha wauza bidhaa za sokoni na parking za daladala?

ryan riz

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
423
Reaction score
683
Nashindwa kuelewa, yaani eneo la nyuma ya stendi kuna soko la vyakula, ila cha ajabu sehemu zinapopark daladala zimezungukwa kwa kupangwa nyanya, viazi, machungwa nk.

Yaani njia ya kupita shida pindi unapanda daladala, hata madereva wanalalamikia hili.

Pia hupelekea watu kupigana kwa kunyaga bidhaa hizi. Yaani unakuta gari unalotaka kupanda limezungukwa na bidhaa za sokoni pande zote,hivyo uruke bidhaa ndiyo uingie ndani ya gari.
 
Picha iko wapi Sasa?unafikiri wote tunapajua huko porini?
 
Nashindwa kuelewa,yaan eneo la nyuma ya stendi kuna soko la vyakula,ila cha ajabu sehemu zinapopark daladala zimezungukwa kwa kupangwa nyanya viaz,machungwa n.k

Yaan njia ya kupita shida,pindi unapanda daladala,hata madereva wanalalamikia hili.

Pia hupelekea watu kupigana kwa kunyaga bidhaa hizi. Yaani unakuta gari unalotaka kupanda limezungukwa na bidhaa za sokoni pande zote,hivyo uruke bidhaa ndio uingie ndani ya gari
Hayati Rais Dkt. Magufuli amekufa na Nidhamu iliyokuwepo ya nchi hii na hivi sasa tumerudi kule kule kama kwa 1985 - 1995 na 2005 - 2015 ambako kila Mtanzania anaamua akitakacho, muda wowote na hakuna wa Kumhoji au Kumzuia.

R.I.P sana Dkt. John Pombe Magufuli.
 
Hayati Rais Dkt. Magufuli amekufa na Nidhamu iliyokuwepo ya nchi hii na hivi sasa tumerudi kule kule kama kwa 1985 - 1995 na 2005 - 2015 ambako kila Mtanzania anaamua akitakacho, muda wowote na hakuna wa Kumhoji au Kumzuia.

R.I.P sana Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwa hili la machinga umeongopa
JPM ndo alifanya machinga wajazane kila mahala akawapa mpaka vitambulisho eti wasibughudhiwe na mtu.

Kuna mambo alifanya mazuri ila hili la machinga alichemka
 
Mwezi huu mwisho,wafanyabiashara wote wanahamishiwa Soko jipya Bahi Road

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Bora iwe ivyo..maana hta maana ya stendi ilikuwa hamna ile mchanganyiko wa bidhaa tena vyakula na magari hatar sana..
Yaan gari likitaka kuondoka aliyepanga bidhaa zake mbele apigiwe honi azivute na gari ndio lipite..

Daladala za kwenda nanenane,swaswa imekuwa shida abiria kupita,kwa jinsi magari yalivyojibana sababu eneo karibu lote la parking limechukuliwa na hawa wauza bidhaa za sokoni katikat ya stendi na kuzizunguruka daladala..
 
Back
Top Bottom