PSL god
JF-Expert Member
- Nov 18, 2023
- 12,573
- 9,076
Wakuu hii story nimeikuta huko FB kwa famous account ya iddi makengo je zinakuwaga na ukweli wowote!?
Nifanye nini nimetembea na mchumba wa wifi yangu kajaua lakini haongei chochote!
Ndoa yangu ina miaka saba, na kwa muda mrefu mimi na mume wangu tulikuwa tunaelewana vizuri. Maisha yalikuwa ya utulivu, lakini mwaka jana mambo yakaanza kubadilika baada ya wifi yangu kumleta mchumba wake kututambulisha. Kwao wako wawili na Kaka yake kwani wazazi wao wamefariki!
Nilipomuona yule mwanaume kwa mara ya kwanza, nilivutiwa naye. Kwa namna fulani, Sikutaka kujizuia, nikaamua kujaribu bahati yangu. Polepole, nikaanza kuhangaika naye mpaka mambo ya kishirikina nikafanya mwisho nikampata.
Nikaanzisha uhusiano naye kwa siri, na nilihakikisha anamuacha wifi yangu. Nilijitahidi kumpa mapenzi ya hali ya juu, nikijua kuwa nilikuwa namchukua kutoka kwa mtu ambaye tayari alikuwa amempenda kwa dhati. Wifi yangu aliachwa aliporudi, nilimpa pole na kujifanya rafiki yake wa karibu, bila yeye kujua kuwa mimi ndiye sababu ya maumivu yake.
Lakini kumbe wakati mapenzi yangu na yule mwanaume yalipokuwa yanapamba moto, walirudiana bila mimi kujua. Mwanaume hakuniambia chochote, aliendelea kuwa nami huku akimrudia wifi yangu kwa siri.
Sasa hali imebadilika kabisa. Kuna picha za uchi nilikua nikimtumia nikiamini tuko wawili tu! Wiki iliyopita, wifi yangu aliyaona yote. Lakini cha ajabu, hajaniambia chochote. Ameendelea kuishi kama kawaida, akizungumza nami kwa upole, akitabasamu kama hakuna kilichotokea, hata kaka yake ahjamuambia ila mwanaume waligombana mpaka wakachana.
Hali hii inanichanganya sana. Sijui anapanga nini kichwani mwake. Je, anasubiri muda sahihi wa kunifanyia kitu kibaya? Au anadhani hakuna maana ya kugombana na mimi kwa sababu tayari mwanaume ameshampoteza? Lakini mbona hajamwambia kaka yake? Mbona yuko kimya kabisa?
Najuta kwa kuivuruga ndoa ya wifi yangu kwa tamaa. Najuta kwa kujitengenezea aibu hii kubwa. Sasa sijui nifanye nini. Nimwambie ukweli mume wangu kabla hajapata habari kutoka kwa mtu mwingine? Nimkabili wifi yangu na kumuomba msamaha? Au nikae kimya na kujifanya sijui lolote?