Hivi style ya 'kikaptula' ya wanaume wa siku hizi imekaaje?

Nyie mnaojiita wanaume wa Mikoani aliyewaroga ni nani??? Kwa miji yenye hali ya hewa ya joto hii style ya kuvaa kaptula ni kitu cha kawaida sana, binafsi yangu napendelea kuvaa kaptula siku za weeknd nikiwa kwenye mitoko yangu hasa nikiwa na private car, acheni kufananisha huo upupu wa kina James Delicious na fashion, though najua fashion ikizidi sana inakuwa issue kidogo.
 
Mkubwa huwa unapiga hivyo vikaptura vifupi vya bright colors?
Mkuu kaptura wengi wanavaa, ila kaptura ya kiume ni pana na ndefu chini ya goti. Mwanaume kuvaa kikaptura kifupi kinachobana cha rangi nyekundu inashangaza kidogo!

Mimi si mtumiaji sana wa mavazi hayo lakini nauchukulia huo kama mtazamo wangu na siwezi kumhukumu au kuchukia anachovaa mtu mwingine kwa kuwa hakina impact kwenye maisha yangu ya kila siku.......

Kama jamii tunapaswa kuishi kwa kuvumiliana ili kuleta msawazo na utengamano kwenye jamii yetu.......

Tunaishi kwenye jamii ya watu mbali mbali na wenye mitazamo tofauti tofauti.........

Kama unaona mtu wako wa karibu anakengeuka na kutoka kwenye mstari kwa busara unatakiwa kumuelekeza na kumuweka sawa kama mshauri.........na sio kumtukana

Kuna wengine wanafanya hivyo kwa kutokujua na kufuata mkumbo.........
 
Tofautisha KAPTULA na KIKAPTULA...!!!
 
Mkubwa huwa unapiga hivyo vikaptura vifupi vya bright colors?
Mkuu kaptura wengi wanavaa, ila kaptura ya kiume ni pana na ndefu chini ya goti. Mwanaume kuvaa kikaptura kifupi kinachobana cha rangi nyekundu inashangaza kidogo!

Utakuta mkaka kapiga kikaptura kifup cha rangi afu bado kakikunja na kinambana hadi akisimama inabid akivute vute ......
 
Hakika mkuu nimekubaliana nawewe... Hayo mavazi hayawezi kuzuia ujenzi wa viwanda
 
Mkubwa huwa unapiga hivyo vikaptura vifupi vya bright colors?
Mkuu kaptura wengi wanavaa, ila kaptura ya kiume ni pana na ndefu chini ya goti. Mwanaume kuvaa kikaptura kifupi kinachobana cha rangi nyekundu inashangaza kidogo!
Hakuna sheria ya kaptura mkuu.. Tafsiri ya kaptura haipo kwenye kamusi...
 
Tunako elekea sasa tutaanza pangiana mavazi
 
Nyumbani tunavaa kanga tu........
 
Siku nkimkuta my man kavaa kichupi hiko namwacha hapohapo wanaume wajinga ni wakupigwa vita
 
Kuna biashara wanakuwa wanatangaza.
 
Acha siasa kila mahali, vikaptula vya kubana, vya pink kwa wanaume ni ushoga, usipepese macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…