Hivi suala la kugawa vishkwambi linahitaji sherehe kweli?

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Moja kwa Moja kwenye mada.

Sipingi kutolewa Vishikwambi ila naona sio sawa kuweka sherehe jambo la kutoa maelekezo na maagizo tu.

Kila kitu viongozi wanataka kongamano hafla nk,vya nini hivyo?

Kwamba Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Uzinduzi wa ugawaji vishikwambi. Hii Nchi haitakuja kuishiwa vituko.

Hivi suala la kugawa vishkwambi linahitaji sherehe kweli?

Wacha inyeshe tujue panapovuja, wananchi wafunge Mikanda ila wao walegeze.

Huenda Tanzania inakabiliwa na mdororo wa Brain power kwa watu wake.πŸ‘‡

 
Vishkwambi vimetumika kwenye sensa, wanaenda kupewa walimu sasa rasmi.
 
Zoezi hilo ilitakiwa lifanyike kimkoa, halafu kila RC awagawie wanaohusika kwenye mkoa wake, nahisi tunapenda sana sherehe ambazo kimsingi hua sioni kama zina kichwa wala miguu, RC anaweza akagawa na kutoa maelekezo yaliyotolewa na waziri mkuu mambo yakawa safi kabisa
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ acha nicheke tuuu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimemaliza ujenzi wa choo na jiko la kisasa kabisa, tafadhali mkuu nitafutie "muheshimiwa" yeyote huko aje kufanya uzinduzi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mimi naona hamna tatizo kwasababu hana kazi lazima atafute kitu cha kumkeep busy. Ni kama tu polisi wa Norway wakipigiwa simu mlevi kaanguka wanakuja faster kumhudumia angalau siku iyo wawe busy.
 
Hata ile ya Helcopter kupeperusha kitambaa kuonesha tupo wangapi, ilitakiwa waende chama cha riadha waombe wanariadha nane yaani hao wangepewa kila wawili wangeshika kitambaa maalumu kuonesha idadi yetu uwanja mzima kwa mwendo wa taratibu, sasa mpaka kurusha ndege kuna mambo yanafanywa na viongozi unaona kabisa hawa washafikia mwisho wa kuwaza. Na wanariadha wale ilikua wanachukuliwa wa dodoma ina maana wangepewa laki laki kama posho ingekua laki nane, kazi inaisha.
 
Hata kutangaza idadi ya watu ilikua ni kuomba vyombo vya habari saa moja kamili jioni Rais anakwenda kutangaza hiyo idadi huku tv zote na radio zikiwa hewani wananchi wasikie na, teaser ingekua Tangazo Rasmi la mama kwa watanzania tena tangazo hilo lingeenda hewani kama wiki moja hivi, sasa unashangaa gharama walizotumia wakati visima na madawati hayatoshi unaona kabisa dhamira yao kwa Taifa sii njema.
 
Walimu gani? Wa serikali au wote na wa private.
 
Eti na helikopta juu,hii haikubariki ni matumizi mabaya ya pesa za Umma..

Watu ambao hawajajiajiri hao hawaoni uchungu na pesa zetu na Hawa ndio wanadiscourage watu kulipa Kodi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…