Miezi kadhaa iliyopita SUMATRA walitangaza kushuka kwa nauli za mabasi zikiwamo daladala ambapo safari zilizonyingi ndani ya Dar ni Tsh. 250/=.
Madreva wa daladala kwa kujua kwamba SUMATRA ni viongozi tu wa maofisini ambao hawatoki nje kuangalia hali ikoje wakaanza kutumia mwanya huo kujinufaisha zaidi, sasa wanachofanya ni hiki kifuatacho:
Mfano, safari ya kutoka Mwenge kwenda Tabata kwa mujibu wa SUMATRA inatakiwa kuwa Ths 250/= lakini kwa sasa ni Tsh. 600/= au zaidi. Maana kuanzia saa 11 jioni na kuendelea huwezi kupata gari la moja kwa moja (Mwenge - Tabata). Kinachofanyika ni kukatiza route, (Mwenge - Ubungo) Tsh. 200/=, gari hilo hilo likishashusha, linasogea mbele kidogo tu linaanza kupakia (Ubungo - Tabata dampo) Tsh. 200/=, baada ya kushusha linasogea mbele kidogo linaanza kupakia (Tabata dampo - Segerea/Kimanga) Ths. 250/=.
Hivyo abiria huyu aliyetoka Mwenge kwenda Tabata anajikuta ameshalipa Tsh. 650/= badala ya Tsh. 250/=. Vile vile mtu huyu anapata adha zaidi ya kutembea umbali mrefu kidogo ambao siyo wa lazima kufuata gari hilo hilo lililomshusha muda mfupi uliopita. Na pia tatizo hili limechangia kuongeza msongamano wa watu kwenye baadhi ya maeneo kama vile Ubungo, ikifika saa moja eneo la Ubungo linakuwa na watu wengi sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Nasema sasa wakati wa SUMATRA kutoka maofisini kwenda site umefika.